Barack Obama ashauri Tanzania kutangaza Vivutio vya Utalii: Serikali yatumia Dreamliner kutangaza Kilimanjaro

Mama Tanzania atakubariki kwa kuwa umembariki!
Hiki kitendawili majamaa wengi hawaipati!
Hakika nchi yetu itaendelea sana na sky is not a limit in our country!
Majumba yanajengwa kila kona!
Investors wanafurika!
Last week nimeingia mkataba na watu wa Finland!
Big project walahi!
Focus people!
Tourism ndiyo lazima itapanda sana maana nchi zote za Africa hakuna palipo na amani kama kwa MAMA TANZANIA walahi!
 
Kufuatia kumalizika kwa Ziara ya kitalii ya siku nane (08) nchini Tanzania, Rais Mstaafu wa Marekani, Barack Obama ameishauri Tanzania kuvitangaza vivutio vyake vya kitalii. Vilevile, ameahidi kuwashawishi marafiki zake nao waje Tanzania kujionea vivutio vyake.
Ushauri huo wa Obama unaendana na jitihada za Serikali ya Rais Magufuli kukuza sekta ya utalii nchini kwa kuamua kufufua Shirika lake la Ndege - ATCL. Dreamliner mpya iliyonunuliwa hivi karibuni, ina nembo ya mnyama Twiga, pamoja na Motto "The Wings of Kilimanjaro."
Mdogo mdogo tu watatuelewa wazee. Peleka Dreamliner huko Guangzhou, Bangkok na Mumbai na uwalete Wachina, Wathailand na Wahindu, then nenda Entebbe na Bujumbura uwalete pia Waganda na Warundi kwetu. Ilete Dunia yote nchini Tanzania.

Hivi ushauri wa Obama umeendanaje na jitihada za Magu? tuna shida vichwani aisee
 
Waache kuwanyanyasa wa wekezaji wageni kunasaidia kutangaza nchi Na Hawaji kwa bahati mbaya huletwana wenyeji mkiendelea kutumia media katika mabadiliko ya sera za kibiashara bila kuwahusisa wadau mtabaki wenyewe
 
Uzi umekaa kishabiki sana
Unadhani kuandika the wings of kilimanjaro ndio kutangaza utalii ?
Hapo mass media lazima itumike pamoja na njia mbali mbali

Emu lipeleke li dream liner lenu china kama wachina watakuja bila ya kuwatangazia kwa vyombo vya habari

NB
sipingi juhudi za maendeleo,lakini inatakiwa lumumba mtumie akili kidogo

hivi ni watu wangapi wanaweza kusoma maandishi madogo kwenye ndege na wakafanya decision kuhusu likizo zao?
 
TCL. Dreamliner mpya iliyonunuliwa hivi karibuni, ina nembo ya mnyama Twiga, pamoja na Motto "The Wings of Kilimanjaro."

Vilikuwepo tangu awamu ya Mwl. JK Nyerere

Ila nimeona dreamliner moja ya Ethiopian Airline imeandikwa Ngorongoro, sijaelewa wao walilenga nini
 
Kufuatia kumalizika kwa Ziara ya kitalii ya siku nane (08) nchini Tanzania, Rais Mstaafu wa Marekani, Barack Obama ameishauri Tanzania kuvitangaza vivutio vyake vya kitalii. Vilevile, ameahidi kuwashawishi marafiki zake nao waje Tanzania kujionea vivutio vyake.
Ushauri huo wa Obama unaendana na jitihada za Serikali ya Rais Magufuli kukuza sekta ya utalii nchini kwa kuamua kufufua Shirika lake la Ndege - ATCL. Dreamliner mpya iliyonunuliwa hivi karibuni, ina nembo ya mnyama Twiga, pamoja na Motto "The Wings of Kilimanjaro."
Mdogo mdogo tu watatuelewa wazee. Peleka Dreamliner huko Guangzhou, Bangkok na Mumbai na uwalete Wachina, Wathailand na Wahindu, then nenda Entebbe na Bujumbura uwalete pia Waganda na Warundi kwetu. Ilete Dunia yote nchini Tanzania.
Binafsi sijaona efforts zozote za maana za kutangaza vivutio vyetu vya utalii.Natamani sana kila niki-tune CNN,Aljazeera,CGTN,
BBC,Sky News nione matangazo ya vivutio vyetu vya utalii.Ziko pia local channels Marekani,China,Europe,Australia,Singapore,
pelekeni matangazo huko,tuna shida gani,all is quiet.TANAPA jamani mnatuangusha sana,wake up.
 
Mama Tanzania atakubariki kwa kuwa umembariki!
Hiki kitendawili majamaa wengi hawaipati!
Hakika nchi yetu itaendelea sana na sky is not a limit in our country!
Majumba yanajengwa kila kona!
Investors wanafurika!
Last week nimeingia mkataba na watu wa Finland!
Big project walahi!
Focus people!
Tourism ndiyo lazima itapanda sana maana nchi zote za Africa hakuna palipo na amani kama kwa MAMA TANZANIA walahi!

Mkataba gani uingie wewe kiazi kojoa kalale
 
Vilikuwepo tangu awamu ya Mwl. JK Nyerere

Ila nimeona dreamliner moja ya Ethiopian Airline imeandikwa Ngorongoro, sijaelewa wao walilenga nini

Wanarangaza ngorongoro which is a good thing hata Klm unakuta imeandikwa Kilimanjaro (Mount)
Nyingine new York
Everest etc,Amazon
 
Hii ya utangazaji bado ni kitu walio na majukumu kinawashindwa sana tena sanaaaaaa kuvutia wageni wa nje kiurahisi..

Inashangaza

Hata kwa wananchi wa nchini wanaweza kutaliii pia
 
Hahahahaha nimechekaaa sana hiyo route mkuu
Yaani wanachekesha mpaka kusikitisha jumla .
Yaani mtu mzima na akili zake anaona ndege itapiga route kama DCM ya Makumbusho- Mbagala via Mawasiliano ubungo, Buguruni,sokota, Chang'ombe, Sudan , Tmk .....

Zero kabisa hii michunga ng'ombe
 
Nape aliwaita wanuka maziwa
 
Back
Top Bottom