Barabara zinazoingia kwenye Majiji ziwe njia nne

dndagula

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
1,457
1,440
Wagombeaji ni kipindi cha kuangalia upya uwezekano wa Majiji yote kuwa na barabara njia nne zinazoingia na kutoka kwenye majiji ili kuondoa msongamano wa magari lakini pia kuyafanya yawe na hadhi ya kimataifa.

Jiji la Mwanza Mbeya Tanga na Dodoma yanahitaji kwa haraka yawe na njia Nne kwani ni zaidi ya miaka 50 njia imebaki moja tu. Huu ni mtaji.

Maendeleo hayana Chama.

Changamkieni hili kwenye ahadi zenu.

Kura yangu kwa JPM.
 
Njia 4 baada ya miaka 10 hizo njia 4 zitakuwa hazitoshi tena utakuja hapa kuomba njia 6, tutafute permanent solution kama kuwa na train na usafiri wa helicopter ndani ya miji yetu, kuzuia magari kuingia mijini bila sababu za msingi, kuwe na parking za kutosha pembeni ya miji, tuboreshe usafiri wa daladala watu wengi wapande badala ya kugombania uwe ni usafiri wa kistaraabu.
 
Kwa uchumi upi tulionao kujaza njia nne ndani ya miaka kumi?

Itachukua muda sana. However na agree na suala la train. Tuwe na undergroud city trains
 
Kuna kenge flani hawataki maendeleo ya vitu lakini wamekuja kutaka ziwe njia sita na helcopters kwenye huu uzi. ebu tuache kwanza mleta mada.
 
Brother daladala zikiwa za kistaraabu watu wengi sana watapanda, shinda sasahivi ni za kihuni sana.
Daladala ni za kupangia utaratibu maalumu. Tena ndani ya miji zipungue. Ziwe zinafanyakazi nje ya miji kuepuka misongamano.
 
Bora na wewe umeliona hili,kwangu sio tuu majiji yaani kuanzia ngazi ya Mji inafaa barabara zijengwe njia nne Ili kukabiliana na ongezeko la magari na kupunguza traffic jam baadae

On top of that italeta muonekano mzuri wa miji yetu kuwa ya kuvutia na kupunguza bomoa bomoa Mji unapokua.

Ifike mahala Tanroads walione hili na sio hii staili wanayotumia saizi ya kujenga lanes nyingi lakini katikati hakuna seperatios just like hii njia ya Sumbawanga hapa chini
IMG_20210425_184134_996.jpg
IMG_20210425_183934_075.jpg
 
Back
Top Bottom