Barabara za mitaani zinazounganisha barabara kuu mbili za TANROADS zinatakiwa kuwa na upana gani?

Lyma

Member
May 9, 2017
38
25
Wapendwa,

Naomba msaada wenu,

Kuhusu barabara za mitaani zinazounganisha barabara kuu mbili za TANROADS. Je inabidi ziwe na upana kiasi gani? Nauliza hivyo kwa ajili ya kufanya ujenzi ambapo kiwanja changu kinapakana na barabara ambayo iko chini ya Manispaa mojawapo Dar inayounganisha barabara ya TANROADS kwa upande mmoja na upande mwingine.
 
Jaribu kuonana na watu wa ardhi wa manispaa yako......kama ni kiwanja cha kupimwa, zingatia vipimo vyako. Usihangaike kugombea mpaka na huyo jirani yako (barabara) maana yeye anaweza kukukaushia sasa lakini akakufanya kitu mbaya miaka 20 ijayo.
 
Kwa hayo mambo yao ya kusema 121meter kuwa makini aisee au usubir hii awamu ipite kwanza!
 
Mmmh 121 mpaka barabara za manispaa (mtaa)?
aende manispaa watamuambia, akishindwa, tafuta wapimaji waje wachukue coordinates, wao wataenda manispaa kupata copy ya ramani ya hapo ulipo, waki plot coordinates utajua upo safe kiasi gani, advantage nyingine ni kua utajua mpango wa matumizi ya hapo kiwanja chako kilipo, unaweza ukawa mbali na barabara, but eneo limetengwa kwa matumizi ya umma.
 
Back
Top Bottom