Barabara ya Morogoro yawa kero kwa watumiaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barabara ya Morogoro yawa kero kwa watumiaji

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Oct 9, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  WAKAZI wa jijini la Dar es SaLaam na wale wa mikoa mbalimbali wanaotumia barabara hiyo wanalazimika kutembea kwa miguu kutokana na kukumbwa na adha kubwa ya foleni.. Adha hii inatokea kutokana na ujenzi wa matuta katika maeneo ya StopOver na Msuguri Kimara kwa ajili ya kupunguza ajali katika barabara hiyo.

  Hii imekuja baada ya wanafunzi mwishoni mwa wiki iliyopita kulala barabarani kwa ajili ya kutaka kuwekwa matuta katika barabara hiyo.

  Kufuatia hali hiyo ya ujenzi wa matuta katika barabara hiyo imepelekea kero kubwa kwa wakazi wa maeneo hasa wale ya Kimara, Mbezi, na Kibamba na kulazimika kushuka kwenye magari na kutembea kwa miguu zaidi ya masaa matano kufika majumbani kwao kutokana na magari kukosa njia ya kupita na kutokwenda kwa ajili ya foleni kubwa.

  Hali hiyo ilileta adha kubwa kwa abiria watokao mikoni ambapo walitarajiwa kuingia jijini saa 11 jioni na kujikuta wakiingia katika stendi ya Mabasi ya Mikoani Ubungo (UBT)majira ya saa 4 za usiku na kuendelea.

  NIFAHAMISHE inashuhudia misururu ya wakazi wa maeneo hayo wakitembea kwa miguu mithili ya maandano ya hiyari katika wiki hili toka lianze katika barabara hiyo.

  Wakazi wa maeneo hayo wameilalamikia hali hii kwa sababu inawaletea usumbufu mkubwa huku wengine wakihatarisha maisha yao kwa kupita njia ambazo si salama kwa usiku na miundombinu mibovu.

  Pia hali hiyo ilisababisha abiria wengi kuporwa wakiwa kwenye foleni huku wengine wakihatarisha maisha kwa kupanda pikipiki ambazo madereva wake hawana uzoefu.

  Katika hali ya kushangaza baadhi ya abiria waliamua kuishia na kulala vituoni ili waepukane na adha ya kuchelewa kazini kwao katika siku inayofuatia.

  "Bora tulale hapa kuliko saa hizi saa mbili hadi nije kufika kibamba nitafika saa 6 halafu saa 10 niamke sasa bora nibane hapa ili kesho niweze kuwahi kibaruani" walisema baadhi ya watumaji wa barabara hiyo

  Kwa upande wa wamiliki wa magari wamesema kuwa, hali hiyo iliwasababishia kuingia hasara ya kupoteza mafuta wakiwa kwenye foleni na baadhi yao kuyaacha magari pembezoni mwa barabara kutokana na kuishiwa mafuta.
   
 2. Mutensa

  Mutensa JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2009
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 426
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Matuta barabara ya Morogoro ni kero sana. Naomba wahusika waliangalie upya. Watanzania wanapoteza masaa mengi sana ambayo yangekuwa yanasukuma gurudumu la maendeleo mbele.
   
 3. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  1. Je matuta na vifo vya wakazi Barabara Moro kwa ajali..wewe ungechagua kipi??

  2. Zijengwe tu 8 lines highway..dar hadi Chalinze kama Kenya wanavyofanya Nairobi-Thika!

  3. Hivi highway ya Bagamoyo Mkata ujenzi utaanza lini??
   
 4. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2009
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Ni kweli tuna ajali nyingi katka barabara zetu zinazosababisha vifo na madhara makubwa kwa waendao kwa miguu, lakini siamini kuwa matuta ndio jibu la tatizo hili. Kwa nini katika bajeti ya barabara isiwekwe na madaraja ya kuvuka kwa miguu kwa kila kijiji kilichoko barabarani?, au kwa nini sisi tunaoteseka na ajali hizi tusijipange na kujenga madaraja haya?. Si lazima yawe ya zege, yanaweza kuwa ya chuma na kuwa mradi mzuri kwa welders wetu. Wakati umefika sasa kuzifanya akili zetu zifikiri kwa kasi kulingana na mabadiliko ya maendeleo.
   
 5. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hii inatokana na madereva kutokuwa wastaarabu, Utakuta dereva anaendesha gari kwa spidi ya 100KPH wakati huo huo kuna kibao kinamwambia usiende zaidi ya spidi 30

  Ikiwezekana yawekwe matuta 100 kutoka Mgogoro (Morogoro) hadi Dar
   
 6. Mutensa

  Mutensa JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2009
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 426
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Athari za matuta main road:
  1. Kuongezeka ajali za magari kugonga mengine kwa nyuma
  2. Foleni za kufa mtu
  3. Kuharibika kwa magari
  4. Sio suluhisho la ajali za kugongwa watembea kwa miguu

  solution:
  "Elimu kwanza"
  Elimu ya usalama barabarani kwa wote - waendesha magari na watembeaji wa barabarani. Hajali nyingine hazitokani na uzembe wa madereva bali pia uzembe wa watembeaji, mfani ni makundi ya "marafiki zetu" wanaovuka kwa makundi, alimradi mwenzie kavuka nae anavuka bila kujali.
   
 7. Mutensa

  Mutensa JF-Expert Member

  #7
  Oct 25, 2009
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 426
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Pole mzizi mkavu.
  This is an important cry falling on deaf hears.
   
 8. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #8
  Oct 25, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kuna rafiki yangu kanambia amechelewa shughuli zake muhimu mjini leo Jumapili kutokana na foleni kubwa kwenye barabara ya Morogoro. Eti jamaa wanajenga tuta lingine maeneo ya STOPEVER. Hii maana yake ni kwamba barabara hii sasa itakuwa na foleni ya kupindukia. Kabla ya tuta hili la pili foleni ilikuwa ya kutisha hata mpaka saa 4 usiku. Nilitarajia watendaji wangeangalia namna ya kupunguza foleni barabarani, kero ambayo ni kubwa sana kwa wakazi wa Mbezi na Kimbamba, badala yake wanajenga matuta ambayo yanazidisha kero. Hivi nani kawaambia matuta yanapunguza ajali kwenye highway? Wanachotakiwa kufanya ni kuwaelimisha waenda kwa miguu na madereva jinsi ya kutumia highway. Bla shaka hii ni nchi pekee ambayo ina matuta makubwa kwenye highway... Sisi bado sana....
   
 9. C

  Chief JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2009
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,488
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Huna gari.
   
 10. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  tuseme ukweli,
  tuta lililowekwa sasa hivi pale kimara stop-over linakera linakera linakera!sipingani na aidia ya kuweka tuta,lakini lile tuta ni kubwa mno
   
 11. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Lile sio tuta mpwa umekoesa Msingi wa nyumba/chumba ....jana nimetumia masaa 3 kutokea ubungo mpaka kimara temboni
   
 12. M

  Mundu JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2009
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Kimara sasa hivi ni kero kero kero.... Sijui hata nini kifanyike. Yani unakumbaka na foleni za mjini afu waenda kuzikuta zile za karibu na home! mafuta yanaisha kinoma, muda unapotea.

  May be yale malori yaendayo mikoani na nchi jirani, yaondoke mjini kuanzia saa nne usiku. nayo ni sababu ya foleni kule... kwani njia ni moja tu ya kutokea Tanzania.
   
 13. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni kuwa barabara hiyo inafika sehemu na inakuwa MTAA. Na watu wanataka kuendesha kama wako HIGHWAY.

  Inabidi ijengwe barabara moja kubwa na pana sana inayopita maporini na watu wasiruhusiwe kujenge karibu na barabara na au kuishi. Hii iende walau hadi Kibaha na huko ndiyo iunganishwe na ile barabara iliyopo......

  Mwisho haya mambo yafanywe na Traffic Engineers na si Kikwete au Lowassa kujiamulia iwe hivi. Wanasiasa waanze kuiheshimu hii field ambayo nina imani kama ingelifanywa vizuri, basi foleni za Dar zingelipungua saana maana nyingine zinasababishwa na UJINGA wa madereva wenyewe.
   
 14. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mbuzi wanaongoza mbuzi wengine!!!.kama tumeshindwa kuwa wastaarabu barabarani, tunatanua, tunakimbia hovyo, sasa hawa mbuzi wenzetu wanafanyaje?

  Ni Mtazamo tu
   
 15. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #15
  Oct 26, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Kwa upande mwingine..........Ngoja tuone lile tuta la Stop-over litakavyo piga mwereka malori usiku!! au gari liache njia liingie stendi pale hapatakalika.
   
 16. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #16
  Oct 27, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Poleni,

  Ni tatizo la maamuzi ya kukurupuka!
   
 17. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #17
  Oct 27, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  invizibo,
  naona umeendelea kufunika na avator ya ukweli.samahani kwa kutoka nje ya mada
   
 18. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #18
  Oct 27, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,860
  Likes Received: 23,480
  Trophy Points: 280
  Hahaha! Mpwa, lile tukutuku la mpwa Fidel na matuta ya morogoro rodi + ndovu mpya tokea Salenda inakuwaje?
   
 19. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #19
  Oct 27, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hahahahahahahah!
  nimecheka hadi nimelia.matuta huwa hatuyaoni.sisi tunayeya tu.nime-mbipu invizibo tuchat nae off-points,tehe tehe tehe!sijui atakubali au najitafutia ban
   
 20. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #20
  Oct 27, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,860
  Likes Received: 23,480
  Trophy Points: 280
  Angalia kama ana mawasiliano na wale jamaa zetu wa jana, tutakula kifungo! Naona na avatar imebadilika. Hey, turudi kwenye point sasa. I miin barabara ya morogoro rodi na matuta yake. Hahaha! Leo ZD kaingia mitini, kifungo kinatisha!
   
Loading...