Barabara ya Mombasa-Moshbar ni fupa lililomshinda fisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barabara ya Mombasa-Moshbar ni fupa lililomshinda fisi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rukiko, May 11, 2011.

 1. R

  Rukiko Senior Member

  #1
  May 11, 2011
  Joined: May 5, 2009
  Messages: 199
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Habari wadau,

  Mi ni mkazi wa Dar maeneo ya Gongo la Mboto (kipunguni) ambapo kuingia huko lazima ushuke Mombasa na upande vigari vinavyoingia ndani kuelekea moshbar.

  Kwa hali ya wakazi wa maeneo hayo ni wengi sana-nafikiri ni moja kati ya maeneo yenye wakazi wengi sana hapa DAR, ikiifuatia Mbagala kwa karibu. Wakazai wa huku ndio waathirika wakubwa wa mabomu ya Gongo la mboto.

  Toka nimepahafamu mahali hapo miaka ya 2006, kero kubwa imekuwa imekuwa ni barabara. Barabara ni ya vumbi isiyofanyiwa ukarabati wa aina yoyote ile. Si wakati wa mvua ama jua.

  Kwa barabara hii ukiiona hutaamini kuwa uko mjini/jijini Dar, na kwa hapa huwa najiuliza, kama hapa-kilometa 16-18 tu hivi kutoka Ikulu panakuwa hivi, vipi huko majita -makojo Musoma kilometa zaidi ya 1000?

  Nimekuwa nikisikitika sana unaposhuka Mombasa makonda wa daladala wanasema haya wale wa visiwani (kwa kuwa inaonekana ni kisiwa kilichojitenga). Magari yenyewe yanayoenda huko ni mabovu-nani atapeleka gari yake nzima huko?

  Hata wenye magari binafsi magari hufa kila siku. Barabara hii ni chafu kwelikweli-mabonde, milima, mahandaki humo humo. Huwa najiuliza hivi huku hakuna mwenyekiti wa serikali za mitaa, diwani, mbunge, waziri na hta rais?

  Ni barabara hii liliyomfukuza Makongoro Mahanga kugombea tena jimbo la Ukonga (2010) na kuligawa kuwa sehemu mbili. Nakumbuka wananchi wa kule walimwambia hawatampa kura hata moja kwa kuwa pamoja na kuwa alikuwa mbunge wao na waziri wa miundo mbinu hakuitilia maanani barabara ya jimboni kwake.

  Sasa hivi kashika mama Eugene Mwaiposa ambaye pamoja na kumtumia rais Kikwete katika kujinadi wakati wa uchaguzi na agenda ya barabara hii kuwekwa mbele hata na rais mwenyewe-bado suala hili limekuwa ni kero-kero.

  Mwaiposa mwenyewe kama ameonekana kupwaya katika hili na kujikita katika mabonanza na kutetea mikopo ya wabunge (Maslahi binafsi) badala ya maslahi ya wale waliomchagua.

  Barabara inaendelea kuwa kero huku barabara nyingine zikiendelezwa kwa kasi ya ajabu kote jijini Dar, mfano Vingunguti, Tandika, Buza, Kipawa-Machimbo n.k.

  Kwa maneno hayo ya machungu kwelikweli, nashawishika kufikiri kuwa hili suala la barabara yenye wakazi wanaokadiriwa kufika 200,000 (sehemu hii imemeza idadi kubwa ya iliyokuwa Kipawa, Majohe, Moshibar Kipunguni, kwa Mkolemba, Moshbar kwa diwani n.k) imekuwa "fupa lililomshinda fisi mbwa ataliweza"?

  Lilimshinda mbunge wa kwanza Balozi Paul Rupia (1995-2000), mtu mwenye ushawishi mkubwa sana hapa nchini, Makongoro Mahanga (2000-2010)- waziri na mbunge na ikisemekana kuwa ni mtu wa karibu na mzee; na sasa Mama Mwaiposa ataliweza?

  Kwa ujumla wanachi wanateseka-(naombeni tu niseme ukweli), na ni kama vile wametupwa na viongozi wao, hawana mtetezi na hawana pa kusemea. Hawajui nini kinaendelea, ikiwa kuna mtu humu ndani ana tetesi zozote, au habari zozote zenye uhakika atujuze tafadhali, tumo gizani na mateso yanazidi kuwa makali kila kukicha. Ukisomasoma kwenye magazeti hupati habari yoyote kusus hili.

  Mwisho niwape pole wakazi wote wanaotegemea barabara hii, yenye umbali wa kilometa kama tatu-nne tu hivi, mwendo wa dk 5-10 tu hivi, lakini habari yake mmmh.

  Nawasalisha.
   
 2. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Ukuwa na sababu ya kujaza maandishi, hiyo ndio kata anayotoka meya wa manispaa ya Ilala Jerry Slaa, huyo ndio wa kumbana. kama sikosei hiyo barabara ni ya manispaa na sio ya TANROADS kwahiyo iko ndani ya majukumu ya Diwani ambaye kwa bahati nzuri au mbaya ndio meya wa manispaa hiyo. mwambieni aitishe mkutano wa wananchi na apunguze kuuza sura kila siku kwenye media utadhani yeye ni modeal. mpuuzi kabisa huyu dogo.
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,423
  Likes Received: 19,736
  Trophy Points: 280
  mbunge wenu ndio makongoro mahanga? kama ndio yeye mlmelamba garasa!~ yule yupo tu kusimamuia miradi yake .....mimi lile eneo nalijua toka mwaka 1998. na watu wanaongezeka sana kule kwa kasi ya ajabu
   
 4. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Jimbo limegawanywa sasa hivi, huyu mwizi wa kura Makongoro yupo Segerea na uko ukonga yupo mwanamke mmoja anaitwa Eugine Mwaiposa. lakini Jerry Silaa is responsible for this.
   
 5. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Barabara hiyo inaanzia kata ya ukonga eneo la mombasa na kuishia kata za kitunda na majohe.
  Diwani wa kata ya ukonga si Jerry Silaa, bali ni mbeijing mmoja hivi anaitwa Elizabeth Mbano. Tangu alipochaguliwa hajawahi kuonekana hadharani. Anatembelea gari yenye kioo "tinted", haijulikani anahofia nini. Lakini kwa kuwa alijinasibu kwa ahadi tele za kuwaletea maendeleo wananchi na hiyo barabara ikiwa ndo kipaumbele, sishangaa kwa tabia yake ya sasa ya kujificha kwenye gari kwakuwa kutokana na kero ya hiyo barabara, wananchi hawana jambo jengine la kumuuliza zaidi ya barabara ya mombasa-moshi bara.

  Mbunge wa ukonga ambaye naye ni mbeijing ndiye anayetakiwa haswaa kushughulikia barabara hiyo, bahati mbaya huyu mama kipaumbele chake kimekuwa ni mabonanza na upatu kwa akina mama wenzake. Hajaonekana kufuatilia suala muhimu kama hiyo barabara, sijui kesha sahau mara hii ahadi yake ama ndo yale yale ya kumuiga bosi wao kutoa miahadi isiyotekelezeka.

  Kwa upande wa pili Jerry Silaa yuko responsible as long barabara iko chini ya manispaa ya ilala, na yeye kama kiongozi wa halmashauri ya manispaa ya ilala anawajibika kuhakikisha barabara hiyo inakarabatiwa na kuifanya ipitike kipindi chote cha mwaka. Na ili azma hii ifanikiwe ni lazima, lazima mama mwaiposa aache kutumia muda wake mwingi kwa masuala binafsi ama yale yasiyo na tija kwa wananchi na badala yake ajielekeze kushughulikia kero za wananchi hasa hiyo barabara pamoja na mahitajio mengine ya maendeleo ndani ya jimbo la ukonga.
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,423
  Likes Received: 19,736
  Trophy Points: 280
  ndio hao hao wamoja
   
 7. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #7
  May 13, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Wote hao waliingia madarakani kwa kumwaga pesa zao, wanazirudisha kwanza walizotumia, harafu mambo ya barabara baadae. Wananchi wakipiga kelele kinaletwa kifusi hadi relini pale kinakaaa weee hata mwezi then kinasambazwa ndo hadi mwaka.

  Ndo maana nasema, tutaendelea kujenga barabara hadi wajukuu zetu nao wanakuja kujenga barabara kwani mipango ya muda mrefu hatuna, mwelekeo kama taifa hatuna licha ya kuwa na akili za kujua mabaya na mazuri.
   
 8. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #8
  May 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,305
  Trophy Points: 280
  CCM HOYEEEE..... Mmeyataka wenyewe na wala msilalamika....
   
 9. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #9
  May 13, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  umenitonesha kidonda, ili tatizo ni toka mwaka 1994 japo kipindi hicho hakukuwa na watu
  wengi huko, ila ilipofika mwaka 1997 watu waliongezeka maeneno ya relini, na mwaka 2000
  huku reli na kivule kulikuwa na watu wengine
  toka kipindi hicho hiyo barabara ni balaa kwa wakazi wa huku,
  kuna rafiki yangu huko wanafua mapazia mara mbili kwa wiki mafumbi
  sio mchezo
   
 10. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #10
  May 13, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,423
  Likes Received: 19,736
  Trophy Points: 280
  nilikuwa naishi relini hapo toka 1999, kipindi hicho kulikuwa na madibwi kibao na mmikorosho
   
 11. C

  Campana JF-Expert Member

  #11
  May 13, 2011
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Wakazi wa eneo hilo wanavuna walichopanda, maana wamechagua chama cha magamba ngazi zote. Walilishwa ahadi wakaziamini. Ngoja waipate
   
 12. M

  Mary Glory Senior Member

  #12
  May 13, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 126
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ni kweli kabisa barabara hiyo inatisha mno.haipitiki.we mbunge amka unafanya nini?wananchi wanapata shida.
   
Loading...