BARABARA YA MIKA MPAKA RUARI PORT

koryo

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
639
278
Barabara iliyotajwa hapo juu ujenzi wake ulianza mwaka 2008 na hadi sasa ujenzi wake hajafikia hata moja ya kumi ya urefu wa barabara ambao ni kilomita kama 80. Ujenzi huu ulianza kwa kasi chini ya Mbunge Mstaafu,kipenzi chetu Prof.Sarungi lakini alipoingia Bungeni Mhe. Lameck Airo kila kitu kilisimama na juzi tu wamediriki kujenga urefu wa mita 200 tena kwa kiwango cha chini ambacho hakijawahi kutokea. Hivi tuuulize Mhe. Lameck Airo tulikupeleka Bungeni kutuwakilisha mbona hatuoni matunda ya uwakilishi wako?. Jitahidi katika mwaka huu wa fedha ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami angalau ufike kwenye Kijiji cha Raranya.
 
Back
Top Bottom