Barabara ya lami ya Mafinga-Makambako ni hatari kwa maisha ya Abiria.

COARTEM

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
3,600
3,651
Barabara hiyo imejaa mashimo makubwa, marefu yanayohatarisha usalama wa abiria na vyombo vya usafiri.
Natambua uwepo wa mkandarasi anayeendelea na hatua za upanuzi wa barabara hiyo, lakini je hayo mashimo hayawezi kufukiwa?
Gari zinapita kwa style ya kuviziana na kuwahiana ili mmoja akikwepa shimo mwingine lazima alivae shimo hilo.
Magari yamekuwa yakikinusurika kugongana kutokana na jitihada za kila dereva kukwepa mashimo hayo.
Ninaomba Prof. Mbarawa umuagize manager wa Tanroads mkoa wa Iringa alishughulikie hili maana mpaka huo upanuzi uje kuisha, sijui nini kitatokea maeneo hayo.
Tusisubiri mpaka maafa yatokee ndiyo tuchukue hatua za kuziba mashimo hayo (Tukumbuke ile ajari ya basi la Majinja na Lori lenye container) sababu ilikuwa ni kukwepa shimo.
Kinga ni bora kuliko tiba.
Rais magufuli hii barabara ni JIPU KUBWA SANA.
 
Back
Top Bottom