Barabara ya kuelekea Rusumo

nyaishozi

Member
Dec 21, 2012
44
9
icon-77694.png

Mh Rais. Mulika barabara ya Kahama kwenda


  1. Napenda nichukue fursa hii kueleza umuhimu wa barabara ya kuelekea Rusumo, hii barabara ni muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa,na hasa kwa nchi jirani ya Rwanda ambako inaelekea. Barabara hii kuanzia Bukombe imeharibika sana ni kama mahandaki tu, na hivyo kuharibu magari yetu makubwa yanayopita kupeleka mzigo Rwanda, mkanda mkandarasi anaitwa Mulima Peter aliyepo site na consultant anaitwa Teku inaonyesha ni wababaishaji kabisa. Kwanza kazi haziendi na sanasana wanaishia kuweka matuta makubwa yasiyo na utaalam na yanayoharibu magari na hasa madogo. Naomba mheshimiwa Rais uwamulike hawa wakandarasi na Tanroads ili kuona huu ubabaishaji unakomeshwa, na barabara hii iwekewe mkandarasi ambaye yupo serious na vifaa na wateja. Hii barabara nimuhimu sana kwa Uchumi wetu. Takriban km 100 toka Rusumo ni mbaya sana. Tusaidie mh. Mizigo ya nchi jirani iweze kufika kwa usalama. Nawasilisha

 

Attachments

  • upload_2017-3-5_13-15-3.png
    upload_2017-3-5_13-15-3.png
    256 bytes · Views: 22
Back
Top Bottom