Barabara ya Chamazi Mbande inasumbua sana ina foleni ya ajabu wakati mwingine

mfichuamambo

Member
Jul 22, 2021
99
274
Hii barabara ni nyembamba halafu foleni ikitokea panakua na shida maana wanaotokea mbagala wanaingilia na hii njia ya kurudi mjini nayo wanaiendea

Maana yake njia zote mbili ya kwenda mbande upande wa left na huu wa kurudi mbagala yaani left zote zinageuzwa kuwa barabara moja tu ya kurudi mmbande maana yake gari za kuja rangi tatu na mbagala zinashindwa kurudi mjini

Huu ujinga unatokea sana, nilifika mbande saa 7 usiku juzi nikitokea rangi 3 tokea saa 1 jioni kisha ushenzi wa twabia wa hili madereva wanatumia barabara zote basi foleni ya kukata na shoka inatokea na hapo hakuna ujanja wa kuchepuka pembeni maana barabara ni nyembamba halafu huku pembeni kuna mtaro kila upande hapo ujanja unakua huna inabidi tu ubaki njia kuu

Kukaa huku ni mateso sana
 
Tumia njia ya kilungule utokee kwa mpalange, Unapandisha mpaka kwa Mama kibonge unaingia zako deviscona hapo kuna option zote kama unaenda Uhasibu au Mtoni au unaenda Tandika au katikati ya Mji.
 
Back
Top Bottom