Inanambo
JF-Expert Member
- Jun 26, 2011
- 3,985
- 2,770
Awali ya yote naipongeza serikali kwa kubuni barabara ya Bagamoyo hadi Msata. ni majuzi tulipita njia ile tukitokea dar kwenda tanzania kaskazini. nilistaajabu kuona barabara hii mpya Ina Madaraja mengi na inapita kwenye uwanda wa maji. ni kama vile wanafanya Land Reclamation kupitisha barabara. Kwa gari tuliyosafiria kutoka sehemu mabayo haina Lami hadi kwenye lami tulitumia Robo saa. Ikiisha tutakuwa tumepunguza foleni barabara kuu ya Morogoro. Ila naona serikali itatumia Gharama kubwa sana kujenga barabara hii hasa hiyo sehemu ya Uwanda wa Maji wanayoifanyia Land Reclamation. Hivi badala ya kuweka Madaraja Mengi kiasi hicho Wataalam hawawezii kujenga Daraja moja refu kama lile la Mkapa mto Rufiji au lile Jinja Uganda penye Mto Nile?