Barabara ya bagamoyo hadi msata

Inanambo

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
3,985
2,770
Awali ya yote naipongeza serikali kwa kubuni barabara ya Bagamoyo hadi Msata. ni majuzi tulipita njia ile tukitokea dar kwenda tanzania kaskazini. nilistaajabu kuona barabara hii mpya Ina Madaraja mengi na inapita kwenye uwanda wa maji. ni kama vile wanafanya Land Reclamation kupitisha barabara. Kwa gari tuliyosafiria kutoka sehemu mabayo haina Lami hadi kwenye lami tulitumia Robo saa. Ikiisha tutakuwa tumepunguza foleni barabara kuu ya Morogoro. Ila naona serikali itatumia Gharama kubwa sana kujenga barabara hii hasa hiyo sehemu ya Uwanda wa Maji wanayoifanyia Land Reclamation. Hivi badala ya kuweka Madaraja Mengi kiasi hicho Wataalam hawawezii kujenga Daraja moja refu kama lile la Mkapa mto Rufiji au lile Jinja Uganda penye Mto Nile?
 
Asante kwa taarifa hata mimi niepita juzi hiyo barabara ni shortcut kiukweli

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hii barabara ni innovation kubwa ambayo si tu inafupisha safari za kuja huku kwetu Kaskazini bali itaufufua mji wa Bagamoyo
 
Serikali inapofanya jambo lenye manufaa inabidi tuipongeze, hongera sana wizara ya ujenzi ikiongozwa na yule yule kamanda Magufuli
 
Kweli ni bararbara nzuri japo kuna maeneo ambayo bado hayajakamilika lkn inarahisisha safari sana.
 
Serikali inapofanya jambo lenye manufaa inabidi tuipongeze, hongera sana wizara ya ujenzi ikiongozwa na yule yule kamanda Magufuli

Mkuu huo ni wajibu wa serikali,unalipa kodi ili serikali itekeleze miradi ya aina hii.
 
Back
Top Bottom