Barabara ya Akachube - Kijitonyama inaharibika hata mwaka bado!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barabara ya Akachube - Kijitonyama inaharibika hata mwaka bado!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Elisha Ray, Jun 6, 2012.

 1. Elisha Ray

  Elisha Ray JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 302
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wadau, mimi ninasikitika sana na mambo ya ulipuaji katika idara za hii serikali. Hii barabara ya Akachube (inayoanzia kijitonyama off Kajenge road, kuelekea upande wa Mwananyamala) imekwishaanza kuharibika hata kabla ya mwaka kuisha toka ijengwe!! sasa hivi lami yake ina mabonde mabonde na mashimo tayari yameshaanza kutokea. Sijui ni nani wanahusika na mambo ya quality katika idara hizi zinazohusika na barabara au hawaoni/wameuchuna? Barabara ina kiwango cha hali ya chini na kodi zetu ndo zishapotea pale.. Hata barabara ya Sam Nujoma walojenga wachina imeshaaza kuwa na mabonde!!!! Wahusika hawaoni haya mambo? au ndo wamechukua cha juu???
   
 2. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,115
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  Hii barabara imeanza kuharibika toka sehemu gani mpaka wapi?
   
 3. Elisha Ray

  Elisha Ray JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 302
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  barabara yote in vibonde vidogo vidogo mwanzo hadi mwisho ingawa vingine havisumbui sana ila ukiwa pale maeneo ya yard ya magari ya Akachube na msikiti kama umetokea Kajenge road kuna mashimo tayari na vibonde vikubwa sana ambavyo ndo vinaelekea kutoa makorongo!!!
   
 4. m

  mob JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2015
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  mh kumbe watu waliona mda sana hii kitu
   
 5. Dotto Mnzava

  Dotto Mnzava R I P

  #5
  Aug 19, 2015
  Joined: Mar 6, 2014
  Messages: 865
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kumbe na hii barabara ilishawahi kuandikiwa habari eeh!
   
 6. Dotto Mnzava

  Dotto Mnzava R I P

  #6
  Aug 19, 2015
  Joined: Mar 6, 2014
  Messages: 865
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Baadhi ya watumiaji wa barabara ya Akachube iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam wameiomba manispaa ya Kinondoni kuikarabati barabara hiyo ambayo imeharibika vibaya kutokana na mvua zilizopita hali ambayo inasababisha usumbufu mkubwa kwa madereva pamoja na kuhatarisha usalama wao.

  Channel ten imetembelea barabara hiyo na kushuhudia mashimo makubwa kwenye barabara hiyo huku magari ,pikipiki na bajaji zikipita kwa shida kutokana na jitihada za madereva kukwepa mashimo hayo.
  Hawa ni baadhi ya watumiaji wa barabara hiyo kama wanavyoelezea.


  Mvua za msimu zilizonyesha hivi karibuni zimeathiri barabara nyingi katika jiji la Dar es Salaam ikiwemo barabara ya Akachube hivyo kusababisha kero kubwa kwa wakazi wa jiji hususan madereva wa vyombo vya moto

  Chanzo:
  Channel Ten
   
 7. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #7
  Aug 19, 2015
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Magufuli alilamba 10 pct hapo.....
   
 8. jMali

  jMali JF-Expert Member

  #8
  Aug 19, 2015
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 8,329
  Likes Received: 1,068
  Trophy Points: 280
  huu ndio wakati wa kulalamikia barabara. :biggrin1:
   
 9. Zanzibar Spices

  Zanzibar Spices JF-Expert Member

  #9
  Aug 19, 2015
  Joined: Jul 14, 2013
  Messages: 7,543
  Likes Received: 2,021
  Trophy Points: 280
  Picha plzzzz
   
 10. gnassingbe

  gnassingbe JF-Expert Member

  #10
  Aug 19, 2015
  Joined: Jun 14, 2015
  Messages: 3,760
  Likes Received: 1,798
  Trophy Points: 280

  ...........wameyataka wenyewe.........CCM ni ile ile oooooh!ni ile ile mbele kwa mbele mpaka kuzimu.
   
Loading...