Barabara Mwenge hadi Morocco 'Barabara ya Magufuli' hatarini kuharibika yajaa maji

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Ile barabara toka Mwenge hadi Morocco iliyojengwa kwa fedha za sherehe za Uhuru iko hatarini kuharibika kabla ya kuzinduliwa kwake,JF inaarifu. Mbele ya Jengo la LAPF,almaarufu kama Millenium Towers,maji yamejaa kwenye barabara hiyo.

Maji yaliyojaa mahali hapo,upande wa kushoto kutokea Posta,yamesababisha njia mpya ya upande huo kutotumika kwa kufukiwa na maji. Mkandarasi wa barabara hiyo ana jambo la kufanya au la kueleza. Maji hayo yaliyopo hapo yanahatarisha barabara hiyo iliyopanuliwa hata kabla ya kufunguliwa rasmi. Wenye masikio na wasikie!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Mzee haraka yanini?mambo bado hayajakamilika kwa hiyo naomba uwe na akiba ya maneno.Mtumbuaji yupo makini sana kwa kuhakikisha jasho la walala hoi halitumiwi vibaya
 
Hata daraja la kigamboni maji yanajaa kwenye maeneo ya waenda kwa miguu..ikinyesha mvua kubwa itabidi wat wapange mawe au magunia ya mchanga darajaji au wawe wanavua viatu na kupita kwenye maji
Hizi barabara mipya siku hizi zinajengwa chini ya kiwango nadhani ukanjanja umezidi kwa hawa wanaojiita maenjinia wetu.
 
Mzee haraka yanini?mambo bado hayajakamilika kwa hiyo naomba uwe na akiba ya maneno.Mtumbuaji yupo makini sana kwa kuhakikisha jasho la walala hoi halitumiwi vibaya
Hata hivyo ndo amemjulisha mtumbuaji
 
Back
Top Bottom