Barabara muhimu itakayomuondoa Halima Mdee, Makonde-Baraza la Mitihani-Goba rd

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,316
24,181
Barabara ya Makonde-Baraza la Mitihani hadi kuunga Goba rd, ni kiungo muhimu sana kwa wakazi wa Mbezi.

Barabara hii ni kubwa sana na kulu Mbezi Juu kuna vigogo muhimu kama Katibu zMkuu TAMISEMI na mkuu wa TAKUKURU,ambao kwa nyadhifa zao kukaa kule ni lazima zingepata jicho la utofauti.

Mbunge Halima Mdee hajawahi kusikika si bungeni tu hata kwenye vyombo vya habari, akipigia chapuo ujenzi wa barabara hii.
Makonda pamoja na ugeni wake jijini ingalau aliipigia debe barabara ya Afrikana-Salasala na ujenzi ulianza.

Wananchi wa sehemu hizo wameapa kumzomea Halima Mdee kila atakapokuwa kama akijidai kufika kuomba kura sehemu hizo.
Kwa sasa hivi barabara hii inatunzwa kwa kujitolea na mkazi wa sehemu hizo ambaye ni mkandarasi, na kwa kujitolea kwa zaidi ya miaka 15.

Sasa naona anaishiwa vocha!

Wananchi wanataka mbunge, na si Halima Mdee, atakaye wasiliana na TARURA kupigia chapuo ujenzi wa barabara hii.
 
Sasa halima ndo anayekusanya Kodi za wanakawe?Mimi binafsi nimeisikia akizungumzia hiyo barabara na bado serikali haijajenga.Sasa kosa la mbunge Ni Lipi?Na je ndani ya kawe hakuna barabara iliyojengwa 2015-20?Kama ipo Basi kumbe anaweza kuwasiliana na Tarura lakini so jukumu la mbunge kujenga barabara nashangaa hata wewe mabambas hujui hili
 
Kazi ya halima sio kujenga barabara kazi yake ni kuwasilisha kero zako sasa kama anaowaambia kero zako wanakwepa majukumu yao wewe na kichwa chako kibovu unamlaumu halima?? Kweli mchawi mtu paka anatumwa tuu..

Sisi huku buza barabara muhimu ya kwa mparange kwenda kitunda na mwanagati ni mbovu haifai daladala zipo nauli 500 hata kwa km 3 na mbunge ni wa ccm mbona hatumlalamikii??
 
Miaka yote Halima kakalia kiti cha ubunge imekuwa batili kwa wananchi wa Mbezi.
Ameshindwa kuhamasisha watu na hata yeye mwenyewe kushauri vyombo husika kutatua kero za wananchi wa Mbezi hususan barabara.
Halime mara zote amefungwa kutetea chama chake tu na si wananchi wa Mbezi/Kawe.
 
Kazi ya halima sio kujenga barabara kazi yake ni kuwasilisha kero zako sasa kama anaowaambia kero zako wanakwepa majukumu yao wewe na kichwa chako kibovu unamlaumu halima?? Kweli mchawi mtu paka anatumwa tuu..

Sisi huku buza barabara muhimu ya kwa mparange kwenda kitunda na mwanagati ni mbovu haifai daladala zipo nauli 500 hata kwa km 3 na mbunge ni wa ccm mbona hatumlalamikii??
Kasindwa kazi.
Akaandamane kwa ajili ya chama chake na afungwe tu.
Hana faida kwa wa anchi wa Kawe.
 
ila halima kachemka aisee , niko hapa bunju mwaka wa nne sasa sijawahi kuona ametia mguu pamoja na changamoto kibao lakini holaaa! kazi kwake aisee
Mkuu atatiaje mguu jimboni wakati yuko busy na Ester Bulaya!
Wakifungwa ,wanafungwa pamoja, selo moja, nisi kwa ajili ya wananchi wa Kawe.
 
Sisi wakazi wa Mbezi Beach hatunaga muda wa kufatilia mbunge kafanya nini ama vipi. Barabara huwa zinatengenezwa na Washua wetu hatunaga kokoro na siasa. Acha dada nae apate pate hivyo visenti vyake
 
Sisi wakazi wa Mbezi Beach hatunaga muda wa kufatilia mbunge kafanya nini ama vipi. Barabara huwa zinatengenezwa na Washua wetu hatunaga kokoro na siasa. Acha dada nae apate pate hivyo visenti vyake
Hebu tuweke wazi umeshiriki kutengeneza barabara ipi badala ya serikali na bila ufuatiliaji wa mbunge.
Tutakutajia majina tunayoyafahamu humu.
 
Hivi nyie mnapiga kula au umeamka ukaona uwongee ya mdee huyo ngwajima kwa kawe apana bora tuumpe mdee aendelee
 
Hilo ni mojawapo ya matatizo ya Halima,

Haonekanagi kwa wananchi kabisa kusikiliza kero zao na kwenda kushirikiana na Serikali katika kuzitatua.

Off course amekuwa akifanya kazi kimya kimya bila wananchi kujua mfano swala la kufuatilia maji maeneo ya Salasala, Kinzudi, Goba, mbezi juu n.k

Halima alikuwa anashinda DAWASA kwa meneja Kawe kila mara kufuatilia maji mpaka yalipopatikana ingawa ni ya mgao na mgao wenyewe ni ilimradi bado huduma ina changamoto kubwa sana.

Sasa wananchi hawajui kama mbunge wao amekua akifatilia bega kwa bega akishirikiana na DAWASA ktk kupata huduma ya maji.

Angekuwa anakutana nao mara kwa mara na kuwapa mrejesho watu wangemuelewa na kuzidi kumkubali.

Lakini sasa hivi yanahitajika mabadiliko.

Wananchi wa Kawe wanajielewa sana kwa wastani ingawa hata wanafiki wapo!

Wanafiki wanazidiwa na wale wanaojielewa huo ndiyo uzuri.
 
Wabunge wengi sana wa Tanzania ndiyo mwenendo wao huo wa kutokuonekana majimboni hadi uchaguzi utakaofuata.

Tena bora Halima kidogo hata kama haonekani kwa wananchi lakini huwa ni mfuatiliaji wa kero za wananchi Serikalini na kutoa hoja kali bungeni kama mwakikilishi wa wananchi.

Sema kwa bahati mbaya sasa wananchi wa jimbo la Kawe kwa wastani wanajielewa sana !

Hiyo ndiyo inayompa mtihani Halima. Ni bora kuwakilisha wanafiki na wajinga lakini kinyume chake inabidi ujipange

Kawe kunahitajika mabadiliko kuna kero za msingi zimekwama !

Halima amefanya alipoweza sawa palipobaki wacha aje mwingine ashieikiane na Serikali kuleta ufumbuzi wa kero wa wananchi.

Naye atakaye shinda akashirikiane na Serikali kuondoa kero za wananchi kwa bidii kinyume na hapo awamu itakayofuata hatapata!
 
Miaka mitano hatujawahi kumwona akipiga jimboni Kawe kutatua kero za barabara.
Makonda kaja na kaingilia barabara mbovu ya Salasala, ingalau inatengenezwa kiwango cha lami.
 
Back
Top Bottom