Barabara Mpya ya SERENGETI-Mbugani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barabara Mpya ya SERENGETI-Mbugani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kituku, Jun 8, 2011.

 1. Kituku

  Kituku JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 239
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  WanaJF
  Kuna mjadala unaondelea kuhusu proposed road ya serengeti mimi inanikanganya kidogo, maana naona sasa wanamazingira na wanawananyama kama kina Goodall wameingilia kati kumtaka raisi abadili root ya huko mbugani ipelekwe south ya mbuga kidogo...na ninavyosoma maoni ya wanaMara wanataka barabara ipitie serengeti. hawaoni kama kunashida yoyote.

  Mimi ninakanganyikiwa na haya hapa...

  • Je ile barabara ya mikumi -Iringa haijapita mbugani? mbona hakuna kesi kubwa hivyo za madhara ya wanyama?

  • Je hakuna taratibu zitakazowekwa hapo mbugani (mf matuta na alama) za kuepuka hayo madhara.
  • Na hao wananchi wa mara wanaolazimisha ipite mbugani je hiyo option ya pili inayopendekezwa kupitisha road ina effect yoyote?
  Naomba jamani mnisaidie hapa na kutoa mawazo yenu kwani mimi ni sijawahi kabisa kufika mikoa hiyo.
   
 2. HOMOSAPIEN

  HOMOSAPIEN JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 719
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Kwa mujibu wa viwango vya kimataifa vya hadhi za uhifadhi duniani,mbuga za Serengeti ziko katika viwango vya juu kabisa duniani UNESCO World Heritage Site ni urithi wa dunia na siyo urithi wa Tanzania,ina maana sisi hatuwezi kupanga chochote bila kuwajulisha wadau wengine ambao nao ni warithi wa hizo rasilimali.kwa maana hiyo hatuwezi kulazimisha kuharibu mbuga na mfumo mzima wa kiekologia kwa kupitisha barabara ambayo haina maslahi ya kidunia.na kwanini ipite mbugani kuna umuhimu gani wa kupita huko ambako hakuna watu ni wanyama tu wakati kuna sehemu nyingine inaweza kupita tena katika maeneo wanyoishi binadamu,barabara inafuata watu au wanyama.SERIKALI IACHE UMAGUMASHI WAKE KUTUHARIBIA URITHI WETU NA WA DUNIA KWA UJUMLA WAKE KWA KULAZIMISHA BARABARA NDANI YA SERENGETI.
   
 3. Kituku

  Kituku JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 239
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kikwete na makongoro nyerere ndo wameshaikomalia .. ipite mbugani.. haya
   
 4. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 953
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Tena acheni kabisa hiyo dharau ya kusema serengeti hakuna watu kuna wanyama kama mmeshindwa kuchangia hiyo mada mliyoianzisha acheni kabisa hizo dharau zenu kwa hiyo mnamaanisha kura alizozipata mhe,raisi toka serengeti alizipata toka kwa wanyama?
   
 5. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Wakenya hawatakiwi kutuamulia wapi pa kujenga barabara!
   
 6. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  I suggest tujenge flyover ili tusiingilie great migration.
   
 7. M

  Mafuluto JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2011
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,602
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  In short, kwanza % kubwa ya mapato yanayotokana na utalii Tanzania yanapatikana Serengeti, na wengi wa wageni wanakuja ktk package zenye kupitia circuit hiyo yaani Manyara, Ngorongoro na at times Tarangire. Yes kimataifa- through utafiti n.k kuna faida za kuwa world heritage sites.

  Kivutio kikubwa mbali na hiyo wilderness ni Migration route ya hayo madudu, takriban 1.7M. Kujenga barabara ya lami kutakuwa na ecological impact na muda mfupi na mrefu , ambayo inaweza athiri kwa kiasi kikubwa route hiyo. Kama sikosei, hiyo ni migration kubwa iliyopo sasa duniani ambayo inahusu aina nyingi za wanyama ! Pia, hii mijizi inaweza kuwa inatumiwa au imeshapiga mahesabu kuwa route ife huku, wabaki kule Maasai Mara na yenyewe ifaidike (labda wanawekeza kule au la) maana kenya sasa wamebaki na mende, kunguni, fukufuku na kenge kibao ktk parks zao, labda na fisi wawili watatu......!

  Mikumi hakuna migration km ya serengeti, na kipande kile cha barabara ni kifupi sana kama sikosei (ingawa ukichunguza utakuta ndiyo maana watu wa Mwaya, na vijiji vingine kuna wakati wanapata taabu sana ya wanyama hasa Tembo sababu ya barabara kuwatenga )

  Zipo njia mbadala ambazo kwanza barabara zipo na wanaweza kuziboresha hizo, au routes kupita sehemu nyingine LAKINI haya majizi yanalazimisha pale na inaelekea ni kwa sababu wanalazimishwa na yale majizi mengine yaliyowekeza kule- mahoteli kila kona, camps na utafiti wa wizi kila siku. Hao hao ndo walilazimisha na sasa wanajenga uwanja wa kimataifa, ili madege ya kuiba wanyama sasa yatue pale badala ya KIA....!! Hayo hayo ndo yaliosemaga kuwa kuwa na makazi ndani ya mbuga kunaathiri wanyama, serikali ikaishia kununua kambi ya jeshi Fortikoma na kuhamisha makao makuu nje- ili wajilie kiulaini. Sasa kama nyumba zinaathiri wanyama, iweje leo watake barabara...???

  Lakini nasikia Jaluo kashampiga jamaa kibuti, so hakuna barabara wala nini vinginevyo asionekane tena kule na mabakuli kuomba omba..!!
   
Loading...