Barabara Mbezi - Makabe: Waziri wa Ujenzi njoo uone TANROADS walichokifanya

Muite

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
2,320
4,751
Kuna matengenezo ya mitaro ya maji taka yalikuwa yanafanyika na yalianza kipindi cha mwishoni kabisa cha uhai wa JPM.

Na Mara tu alivyofariki jamaa hawakurudi kumalizia kazi kana kwamba waliona hakuna wakuwawajibisha tena.

Ni ngumu kuelezea kazi ilivyofanyika , lakini kwa macho tu HUWEZI KUAMINI KAMA IMEFANYWA NA MTAALAMU HATA WA NGAZI YA CHETI TU. Kazi haikukamilika kabisa. kulipotengenezwa ni chini, chini, chini ya kiwango, na kutokana na kutokukamilika kumesababisha uharibifu .

kwa mfano MTU anamimina zege kwenye mtaro na sehemu nyingine anaacha, matokeo yake maji ya mvua yamechimba sehemu zisizo na zege kisha kupita chini kwa chini na kusababisha zege kuning'inia juu kabisa.

Mfano MTU anaweka kalavati sehemu za Barbara zinazoingia mtaa halafu haweki Kingo ktk kalavati hizo matokeo yake udongo wote juu unatolewa na maji ya mvua na movement za magari na matokeo yake linabaki kalavati lenyewe lililowekwa ,mbaya zaidi kalavati halikuwekwa kwa mkadirio sahihi kwani limechimbiwa chini zaidi.

Mfano Kingo za zenge zilizojengewa katika mtaro ni fupi sana na zimeacha nafasi kubwa ya ardhi juu ambapo udongo mwingi umeingia .

Ninachoamini iwapo TAKUKURU ikifika na kuona kilichofanyika hawatawaacha hawa jamaa maana huenda ukaambiwa ni hela kubwa iliyotumika tofauti na kakazi kalivyofanyika.

Ni vema WAZIRI WA UJENZI AFIKE AJIONEE Maana huku ni kufanya wananchi waone huenda Watendaji wameanza Uzembe na ubadhirifu baada ya JPM kuondoka.

Ni bora wangeacha kama walikuwa hawajajiandaa kutengeneza mtaro huo kwani inaleta usumbufu mkubwa sana kwa waumini wanaofika ktk kanisa hilo pamoja na wanaotumia njia hiyo.

Nimeamua kufikisha ujumbe huu kwa wahusika kupitia JF nikiamini itawafikia.

Ni eneo la Barbara iliyopo Mbezi Makabe Kanisa Katoliki(RC)
 
Kuna matengenezo ya mitaro ya maji taka yalikuwa yanafanyika na yalianza kipindi cha mwishoni kabisa cha uhai wa JPM.

Na Mara tu alivyofariki jamaa hawakurudi kumalizia kazi kana kwamba waliona hakuna wakuwawajibisha tena.

)

Nimeishia hapa kusoma.

Mpaka anayetakiwa kulaumiwa ni magufuli maana aliendesha nchi katika misingi ya kumtegemea badala ya kuunda mifumo imara ambayo hata kama akiwa hayupo basi nchi itaendelea.

NB: Unadhani unajenga tu? Hujui kuna malipo na kama mkandarasi asipewa ela atasimamisha ujenzi? Sasa kama serikali ya magu haikumlipa ulitaka wajenge vipi?
 
Kuna matengenezo ya mitaro ya maji taka yalikuwa yanafanyika na yalianza kipindi cha mwishoni kabisa cha uhai wa JPM.

Na Mara tu alivyofariki jamaa hawakurudi kumalizia kazi kana kwamba waliona hakuna wakuwawajibisha tena..
U said it all kaka
 
Mkuu nimeona andiko lako limefanya kazi.. Ukarabati umeeanza tena... nimepita leo hiyo barabara mkandarasi anapiga kazi
 
Mkuu nimeona andiko lako limefanya kazi.. Ukarabati umeeanza tena... nimepita leo hiyo barabara mkandarasi anapiga kazi
Tunasubiri Ahadi ya kuweka Lami iliyotolewa na mwendazake siku anafungua Stand kuu Mbezi
 
Back
Top Bottom