Barabara Kinondoni Biafra ni jipu

monta

JF-Expert Member
May 6, 2014
1,203
1,567
Wakuu mimi sioni kazi ya serikali ya Kinondoni kwenye hili suala la barabara uliyopo mtaa wa Dunga Biafra kama unaelekea kanisani. Ni barabara kubwa tu na viongozi wengi wanapita ila imeozaa. Ni jipu ambalo linatoa usaha mwingi sana sasa sijui linasubiri nini.

Miezi kadhaa imepita barabara imekuwa mbovu kiasi cha kushindwa kupitika lakini haijafanyiwa matengenezo yoyote. Kwa kweli inasikitisha sana kuona sehemu muhimu kama Kinindoni kunakuwa na miundombinu mibovu kama hii barabara ya kanisani. Naomba viongozi husika wasikie kilio cha wananchi maana wanateseka.

Ni kero kubwa sana huku yani mtu hadi anajuta kuwa mtaa huu kisa hiyo barabara.
 
Zipo nyingi sana barabara zimeharibika kiwango cha kutisha! Anzia Kijiweni hadi Morocco hotel: ile Africasana hadi kijitonyama...akachube road nenda hiyo ya Biafra hadi kinondoni karibu na Ultimate Security....zingine Kimara na Ubungo kibangu!
 
Ile ya kwenda kwa Anna makinda/mabatini polisi,unaunganisha na Akachube road,magomeni morocco-kijiweni(sinza),angalau hiiya kijiweni morocco ina miaka mingi kuliko nilizotangulia kuzitaja,hizo watu walipeana deal,wakandarasi wabovu kuliko betri za EVER READY.
 
Mliambiwa CCM ni ileile mkajifanya kuweka pamba masikioni sasa wote tunaisoma namba.
 
Mliambiwa CCM ni ileile mkajifanya kuweka pamba masikioni sasa wote tunaisoma namba.
usiwe mjinga. kuna wabunge wa upinzani na hata Meya. madiwani upinzani wapo. wanafanya nini. hata matamko hawasemi lolote. wao wanakimbilia kwenye pesa tu kama mikataba sijui ya UDA. kwenye maslahi zaidi kwao. barabara kwao kwa sasa hazilipi. si unajua tatizo la mtu akishapata nafasi anataka kuitumia vizuri. watanzania ndio tulivyo. kwa nini hapo isisemwe ukawa nguvu ya soda.hakuna lolote la kupigania wanyonge
 
Nashukuru kilio kimesikika na mda huu barabara inatengenezwa
 
Back
Top Bottom