Barabara ya Morogoro kuanzia Kimara mpaka Kibaha, trafiki mmeshindwa kudhibiti ajali?

Isac M

Senior Member
Mar 9, 2014
113
76
Hii barabara imekithili kwa ajali zinazopoteza maisha ya watanzania, na wengine kuachwa na ulemavu.

Kwanini daladala, bajaji hazipaki kwenye sehemu ya kituo, zinapaki barabarani ilihali vituo ni vikubwa? na ajabu askari huwepo wakiangalia tu.

Leo imetokea ajali Kimara Suka iliyopoteza maisha ya raia wakiwemo wanafunzi, kwa uzembe wa kupaki barabarani Daladala na bajaji.

Ajali zimekithiri barabara hii. Wahusika waiangalie barabara hii kwa jicho la dharura.
 
Askari hawana uwezo wa kupambana na ajali hapa nchini. Jukumu la kuzuia ajali lipo kwetu sisi watumiaji wa vyombo vya moto na wapita njia.

Sheria za barabarani haziheshimiwi unategemea miujiza iwepo kusitokee ajali?

Acheni kuwabebesha hao wanyonge mizigo mikubwa kuzidi maisha yao, waacheni wapumue na wao.
 
Uko sahihi kabisa mkuu, jukumu la kulinda uhai ni letu wenyewe, bodaboda anapaki barabarani kabisa akitegemea askari aje kumzuia.
 
Nidhamu ya barabarani ni jambo nyeti sana. Madereva wengi hukokota tu vyombo vyao ili mradi waende na kurudi ila usalama hauzingatiwi kabisa.

Askari wakiamua kupambana na wavunja sheria utasikia kelele, wakiwaacha waende wenyewe utasikia ajali.

Mtanzania ni mtu mwenye IQ ndogo sana huwenda kuliko wanadamu wote duniani.
 
Askari hawana uwezo wa kupambana na ajali hapa nchini. Jukumu la kuzuia ajali lipo kwetu sisi watumiaji wa vyombo vya moto na wapita njia.

Sheria za barabarani haziheshimiwi unategemea miujiza iwepo kusitokee ajali?

Acheni kuwabebesha hao wanyonge mizigo mikubwa kuzidi maisha yao, waacheni wapumue na wao.
Kazi ya askari ni kumshurutisha asiyetaka kufuata sheria, hili halina mjadala.
 
Kazi yako wewe mtumiaji wa barabara ni kufuata sheria za barabarani uwe ni dereva au mpita kwa miguu.

Kama hamna akili ya kujiongoza wenyewe barabarani basi mna sifa ya kuwa wanyama (mifugo jamii ya punda)

Suala la kujiongoza unataka uongozwe na mwanadamu mwenzako? Ni sehemu ya upungufu wa akili.

Naendelea kuamini mtanzania ni mtu mwenye IQ ndogo sana huwenda kuliko wanadamu wote duniani.
 
Ajali nyingi za barabarani sio za asili bali ni watumia barabara kudharau tahadhari wakati wa kutumia barabara. Mtu anakaa mita 1 kutoka barabara tena anapaki bodaboda yake hapo au mtembea kwa miguu anakaa umbali wamita 1 huku akichezea simu yake huku nako dereva hazingatii tahadhari anabonyeza simu, mara ghafla kajisahau katoka nje ya barabara anapiga honi lakini mtembea kwa miguu nae yuko bize na simu yake, mara tairi hili hapa la shingo na kifo hapohapo.
 
Askari hawana uwezo wa kupambana na ajali hapa nchini. Jukumu la kuzuia ajali lipo kwetu sisi watumiaji wa vyombo vya moto na wapita njia.

Sheria za barabarani haziheshimiwi unategemea miujiza iwepo kusitokee ajali?

Acheni kuwabebesha hao wanyonge mizigo mikubwa kuzidi maisha yao, waacheni wapumue na wao.
Sasa kama sio kazi ya askari, wapo pale wanafanya nini?

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Nidhamu ya barabarani ni jambo nyeti sana. Madereva wengi hukokota tu vyombo vyao ili mradi waende na kurudi ila usalama hauzingatiwi kabisa.

Askari wakiamua kupambana na wavunja sheria utasikia kelele, wakiwaacha waende wenyewe utasikia ajali.

Mtanzania ni mtu mwenye IQ ndogo sana huwenda kuliko wanadamu wote duniani.
Kwa hiyo waenda kwa miguu wakimbizane na magari kuvuka barabara kama digidigi, hii ndio IQ kubwa kwako.

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo waenda kwa miguu wakimbizane na magari kuvuka barabara kama digidigi, hii ndio IQ kubwa kwako.

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
"Naendelea kuamini mtanzania ni mtu mwenye IQ ndogo sana huwenda kuliko wanadamu wote duniani"

Sheria za barabarani zinatakiwa kufuatwa na yeyote aliye ndani ya chombo cha moto na aliye nje ya chombo cha moto.

Kwa vile mmeshindwa kuheshimu sheria za barabarani mmesababisha walio ndani ya vyombo kusababisha ajali kwa walio nje ya vyombo kwa matumizi yasiyo sahihi ya barabara kwa muda husika ama uzembe wao.

Walio nje ya vyombo wamesababisha wimbi la ajali kwa walio ndani ya vyombo vya moto.

Barabara inahitaji mawasiliano ya waenda kwa miguu na watumiaji wa vyombo vya moto. Kama makundi haya mawili hayatii sheria kwa pamoja bado mtaendelea kuzoa miili kwenye kila kingo za barabara.

Panua ufahamu wako usiubane kama nyonga za kigori.
 
Chanzo cha ajali kwenye hiyo barabara ni usanifu mbovu...

Nenda nchi zilizoendwlea uone kama kwenye highway yoyote kubwa kama hiyo inayokatiza kwenye mji mkubwa kama watu wanavuka kwa miguu kwenye zebra...

Hii barabara imekithili kwa ajali zinazopoteza maisha ya watanzania, na wengine kuachwa na ulemavu.

Kwanini daladala, bajaji hazipaki kwenye sehemu ya kituo, zinapaki barabarani ilihali vituo ni vikubwa? na ajabu askari huwepo wakiangalia tu.

Leo imetokea ajali Kimara Suka iliyopoteza maisha ya raia wakiwemo wanafunzi, kwa uzembe wa kupaki barabarani Daladala na bajaji.

Ajali zimekithiri barabara hii. Wahusika waiangalie barabara hii kwa jicho la dharura.
 
Hii barabara imekithili kwa ajali zinazopoteza maisha ya watanzania, na wengine kuachwa na ulemavu.

Kwanini daladala, bajaji hazipaki kwenye sehemu ya kituo, zinapaki barabarani ilihali vituo ni vikubwa? na ajabu askari huwepo wakiangalia tu.

Leo imetokea ajali Kimara Suka iliyopoteza maisha ya raia wakiwemo wanafunzi, kwa uzembe wa kupaki barabarani Daladala na bajaji.

Ajali zimekithiri barabara hii. Wahusika waiangalie barabara hii kwa jicho la dharura.
Maelezo yako ni mazuri.Hii ni hatari,bodaboda,bajaji wanapaki sehemu za hatari,na ni karibia mikoa yote,sio Dar tu.Wanapaki kwenye kona,barabarani,makutano ya barabara,karibia na barabara kabisa nk
 
Askari hawana uwezo wa kupambana na ajali hapa nchini. Jukumu la kuzuia ajali lipo kwetu sisi watumiaji wa vyombo vya moto na wapita njia.

Sheria za barabarani haziheshimiwi unategemea miujiza iwepo kusitokee ajali?

Acheni kuwabebesha hao wanyonge mizigo mikubwa kuzidi maisha yao, waacheni wapumue na wao.
Kweli kabisa,kila mtu,achukuwe tahadhari.Kuanzia naenda kwa miguu,baiskeli,pikipiki,gari na kila mtumiaji wa barabara.Waendesha pikipiki,baiskeli na wenda kwa miguu,wengi hawajui kama alama za barabarani na uslama wa barabarani,wao unawahusu,wanajuwa hivyo vinawahusu madereva wa magari tu.ifike mahali askari wa barabarani,wawakamate waendesha baiskeli na wenda kwa miguu,kwa kuvunja sheria za barabarani(mimi sio mwanasheria,wanaojuwa sheria,wanielimishe,kama inawezekana hilo kufanyiwa kazi)
 
Back
Top Bottom