Barabara inayopandisha Mbezi Juu (inayopandisha kushoto juu, pale kituo cha tangi bovu) ipigwe lami mpaka inapokutana na Goba Road.
Hii itasaidia usafiri, itapunguza foleni, na itachochea kukua kwa uchumi kwenye eneo hilo zuri la kilimani lenye hewa nzuri. Vilevile barabara hii itapitika vizuri zaidi kipindi cha mvua.
Eneo hilo litakuwa mtaa mzuri wenye kupendeza, kama mitaa ya Masaki/Oysterbay.
Kama unatoka mjini, barabara hii iko kushoto (ina panda juu) opposite na kanisa la KKKT la Tangi Bovu. Inapita Enocksville, inapita mpaka kituo cha mafuta cha Matala Empire (ukicheki kwenye google map).
Vilevile nashauri barabara hii iitwe Tangi Bovu Road au Masaki Road au Rombo Road.
Barabara hii itaunganisha Bagamoyo Road na Goba Road, kupitia maeneo hayo ya ndani ndani.
Je, TANROADS au TARURA au TAMISEMI au Wizara ya Ujenzi au Serikali ya mkoa au Halmashauri ya Jiji au serikali za mitaa au Development Partners (wafadhili kama World Bank, JICA, DFID, EU delegation etc.) wanaweza kuijenga hii bara bara?
Hivi, hii barabara imeshawekwa kwenye ramani za mipango miji?