Barabara inayojengwa ya Mwenge - Morocco imefunikwa na maturubai kuzuia mvua namtafuta Mjapan kwa ufafanuzi wa kitaalamu

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,832
141,749
Sehemu ya barabara ya Mwenge - Morocco inayoendelea kujengwa imefunikwa na maturubai kuizua isilowane na maji ya mvua.

Ingekuwa ni mkandarasi mzalendo ndiye kafanya hivi ningeanza kupata mashaka juu ya ubora wa hii barabara lakini kwa sababu inajengwa na Wajapani ngoja nimtafute yule rafiki yangu Injinia wa kijapan kwa ufafanuzi.

Nitaleta mrejesho.

Maendeleo hayana vyama!
 
Nijuavyo na u layman wangu lami haipatani na unyevunyevu, ndio maana wanapoweka lami huwa wanachimba chini kuondoa udongo unaohifadhi maji, halafu wanaweka udongo wa tifutifu, udongo unaohifadhi maji usipoondolewa husababisha lami kutitia. Mara nyingine huwa wanaweka nailon chini halafu juu wanaweka udongo wa tifutifu, nailon linasaidia kuzuia unyevunyevu, hasa kipindi hiki ambacho mvua zinanyesha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ndivyo basi yule wa Kimara to Kibaha yupo juu yeye hajui turubai wala ngozi ni kazi kwenda mbele
 
Back
Top Bottom