Barabara bora kwa njia nne ni ipi kati ya hizi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barabara bora kwa njia nne ni ipi kati ya hizi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mmaroroi, Jun 17, 2009.

 1. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ndugu wana JF nauliza swali ambalo linaweza hata kuwasaidia waamuzi katika Serikali yetu. Kati ya Barabara zifuatazo ni ipi bora kiuchumi kwa njia nne kabla ya nyingine:-
  1. Kimara - Mlandizi hadi Chalinze.
  2. Mbagala hadi Mkuranga.
  3. Mwenge - Tegeta hadi Bagamoyo.
  4. Chalinze - Msata hadi Segera.
  5. Chalinze hadi Morogoro.
  6. Gongo la Mboto hadi Chanika.

  Katika majibu hayo tuzingatie vipaombele kutokana na uchumi wa Taifa letu. Nawasilisha.
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mkuu,

  Hiyo namba moja na tano ungeunganisha pamoja!

  Then kwa maoni yangu barabara hiyo kwa sasa ni muhimu sana kwa maendeleo ya taifa. Hii ndiyo kiunganishi cha nchi zote jirani i.e Zambia, Malawi, Kenya, Uganda, Kenya, Burundi etc na pia ni kiunganisha cha mikoa yote ya nyanda za juu kusini na kaskazini!

  Pili, kwa sasa barabara ya Dar- Moro ina trafic density kubwa sana kwa wale mnaosafiri mara kwa mara na barabara hii mtaniunga mkono.....so ingekuwa bora kama hawawezi kuweka njia nne hadi Moro, basi waweke hadi pale Chalinze kupunguza msongomano mkubwa wa magari toka Kimara hadi Chalinze ambapo magari hupungua kidogo kwani yanagawana njia....Arusha na Moro!
   
 3. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Kwa umasikini wetu tunatakiwa tuinvest wisely. Wajenge njia moja (mbili?) Lugoba - Bagamoyo ili ku divert magari ya mikoa ya Kaskazini mashariki/kupunguza magari kwenye barabara ya Ubungo-Chalinze. Critics watasema Kawambwa na JK wanajipedelea kupeleka maendeleo kwao lakini this make sense.
   
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Next Level,

  Mie siyo mwenyeji wa Dar kwa sasa yaani niseme wazi kuwa nimeshakuwa mshamba fulani hivi nikifika Dar. Kabla sijachangia ningelipenda kujua kama hizi foleni za magari zinakuwepo wakati wa kwenda kazini tu (asubuhi) au na wakati wa kurudi?
  Ninavyofahamu ni kuwa watu asubihi wanaenda mjini na mji si mkubwa na hapo lazima foleni iwepo na tena ya kutisha. Ila kama hata wakati wa kurudi ipo na watu wanatoka nje ya mji (mji unapanuka kwa mbele) basi lazima niseme wazi kabisa kuwa tatizo siyo barabara, ila tatizo ni Traffic movement control ni mbaya sana.
  Ngoja nitoe mfano kidogo wa maeneo ambayo mwaka jana niliyaona.
  1. Mwenge kama pangejengwa barabara ya kupita juu kwenda Tegeta, basi ile foleni kubwa ya pale kuingia kituo cha mabasi ingelipungua kwa asilimia kubwa sana.
  2. Kinondoni Morocco kama pangelikwekwa konokono, pia hali ingelikuwa nafuu.
  3. Ubungo, Buguruni, TAZARA, Kamata, uwanja wa Karume, nk....

  Hizo sehemu chache tu nina imani kama traffic flow ingelikuwa optimased, basi washikaji swala hili lingelileta ahueni.

  Ila dawa ya foleni kwa Dar ni kuweka njia za Reli (Trams, trains) na rapid buses na ukishamaliza, unatangaza kwamba, maroli yote yanaingia Posta/Kariakoo nyakati za usiku na weekend tu na vinginevyo, labda kwa kibali maalumu na hiki kiwe cha kusotea kidogo ili kuwakatisha tamaa waombaji wanaotaka kulala nyumbani usiku badala ya kufanya kazi.
  Pia ili uingie mjini (kama huishi huko) basi inabidi gari lako liwe na kibali maalumu (unalipia kwa mwezi/kwa kila unapoingia mjini. Hii watu wote wenye hela njaa basi watakimbia magari na kuja kwenye reli. Hii kitu, mtake msitake, ndiyo itakuwa solution ya matatizo ya usafiri katika nchi nyingi duniani maeneo ya MIJINI.
   
 5. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Number 1,2,3 na 9 ni muhimu sababu ndio zinatoka nje ya mkoa wa Dar es salaam. Tuanzie na hizi hata kama ni kwa awamu then tuendelee na nyingine.
   
 6. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sasa sijui ni sababu ipi iliyofanya Serikali yenu iipe kipaumbela kwa njia nne barabara ya Chalinze - Lugoba hadi Segera.
   
Loading...