Bara na Zanzibar kutofautiana kwenye suala la takwimu za Coronavirus imekaaje?

akatanyukuile

JF-Expert Member
Sep 13, 2019
314
308
Nimekaa kwa mda ninatafakari juu ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar nimeambulia manyotanyota. Nimejaribu kufuatilia tangu ugonjwa uingie nimejaribu kuangalia namna Zanzibar inavolichukulia jambo hili na inavojitahid ni tofauti sana na bara. Mbaya zaid tangu mkuu ametangaza kutokea chato kua ugonjwa huu uchukuliwe kawaida Bara hakuna report tena ya wagonjwa, waliokufa, wala waliotengwa.

Inaonesha huu ni mkakati ambao hawataki kuwapa stress raia ama kwa maana nyingine. Swali linakuja Zanzibar haijakoma kutangaza na mpaka sasa waziri mwenye dhamana katangaza yakua wamefika 105 lakini la kushangaza wakishatangaza jumla inaongezwa Tanzania sasa hapatakuwepo na msuguano hapo?

Maana Tanzania haitaki kuchafua ubao ila Wazanzibar wanaamua kuuchafua. Kama afya haipo kwenye muungano mbona inaongezwa kwenye jumla ya Tanzania?

Mimi ninaona bora wawape mamlaka yao ili wafanye mambo yao kwa uhuru. Mfano kama Tanzania ikaingia kwenye skendo ya kuficha taarifa na jumuia za kimataifa zikaamua kuwatenga hatuoni zanzibar itajumuishwa bila sababu? Ninakaribisha mawazo labda mm ninawaza kinyume.

ASANTE TUENDELEE KUPAMBANA KILA MMOJA KIVYAKE KORONA IPO KAZINI HAILALI UKISUBIR TAMUKO LINAWEZA KUKUTA KABURIN.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni hali ya kusikitisha sana siwezi kuamini. Tumekosea sana kuwa na viongozi awamu hii wanaocheza na maisha ya watu kiasi hiki. Inasikitisha sana na wataabika mno kadri siku zinavyokwenda.
 
Nimeskia wanaleta mfumo wa herd immunity

Kwamba mpaka mwakani wanataka taifa libaki na raia wenye afya njema
 
Back
Top Bottom