BARA BARA YA TABATA SEGEREA TO KIMARA via KISUKURU NI KERO

Tangasisi

Senior Member
Aug 21, 2013
116
225
Wadau ningependa kuanza na pongezi kwa idara husika ndani ya Serikali kwa kufanya ukarabati wa barabara itokayo Tabata Segerea nakuelekea maeneo ya Kimara kuputia maeneo ya Tabata Kisukuru na vitongoji kadhaa Kwani barabara hii imekuwa na matumizi makubwa hata kabra ya ukarabati huu hivyo matengenezo yake yatakuwa ni yenye manufaa kwa wakazi na watumiaji wa barabara hiyo.

Pamoja na umuhimu wake ujenzi wa mradi huu naona unadosari za kimazingira hasa kwakuzingatia barabara hiyo inapita kwenye makazi ya watu wengi. Mbali ya kuwa project inakwenda slow lakini pia Hakuna uzingatiaji wa udhibiti wa vumbi Kali la cement watumiayo kwenye ujenzi .

Sina uhakika Kama Environmental Impact Assessment (EIA) ilifanywa na mapendekezo yake yakoje Ila kwa sisi raia watumiaji tunachokiona ni kero zifuatazo:
1. Vumbi Kali la cement ambalo linaathiri afya zetu hususan watoto wadogo hivyo kutishia kupatwa na magonjwa hatarishi Kama T.B
2. Mwendo kasi wa Magari yapitayo barabara hiyo kutishia kutokea kwa ajari barabarani
3. Kuchelewa kuisha kwa barabara hiyo hivyo kuchelewesha malengo yaliyo kusudiwa.

Ningeomba mamlaka husika kuchukua hatua stahiki juu ya kandarasi hii kabra madhara makubwa zaidi hayaja jitokeza.

Wakati mwingine tunona bora wasingefanya chochote maana barabara ilikuwa mbovu lakini si hatarishi kwa kiwango hiki. Hakukuwa na vumbi wala magari kwenda kasi.

Kwa wajumbe mnao ifahamu barabara hii naomba mchango wenu katika hili.
 

Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
36,252
2,000
Kabra= kabla.

Mamlaka husika angalieni hili jambo kwa jicho la tatu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom