Bao la Mkono: Fomu za matokeo zaongezewa kipengele kipya kinyemela

nyampanaga

JF-Expert Member
Nov 16, 2012
1,104
559
Nimemuona Salumu Mwalimu akilalamika ITV kwamba NEC wamefanya marekebisho kwenye fomu za matokeo kwa kuongeza kipengele cha idadi ya wapiga kura walioongezeka kituoni.

Wakati kawaida fomu hujazwa idadi ya kura zilizopigwa na kura zilizoharibika.

Swali safari hii kutakuwa na wapiga kura watakaongezeka vituoni, je watatoka wapi? Kazi ipo.
 
Yawezekana ni wale watakaopiga kura kwenye vituo ambavyo hawajaandikishwa. Mfano,watakaopiga kura za Urais kwenye vituo vipya
 
Pengine wanamaanisha wale ambao watapigia kura nje ya vituo walivyoandikishiwa kwa sababu mbali mbali kama kuhama baada ya kuandikishwa, au kutokuwepo pahala mtu alipoandikishiwa kama vile wanafunzi walio likizo.

Ninaomba ninachokidhani kiwe sahihi kwa sababu kama kuna ujanja unafanyika, nina mashaka wanaoratibu uhuni wowote dhidi ya haki za Watanzania, watayaona mabadiliko lakini hawatayafaidi.
 
Si Wanasema Tupige Kura Tulipojiandikisha Tu Au?
 
we Petro, hakuna mtu anaruhusiwa kupiga kura kituo ambacho hajandikishwa. mm jana nimepiga cm tume na hawataki kuckia, c rais wala mjumbe wa nyumba kumi.
 
hizo ni kwa Ajili ya watu.maalumu amabao ni

kiongozi yeyote wa kisiasa ktk kata/jimbo hilo......

pia msimamizi katika kituo husika.....

ila wote wakiwa na vibar maalumu
 
Pengine wanamaanisha wale ambao watapigia kura nje ya vituo walivyoandikishiwa kwa sababu mbali mbali kama kuhama baada ya kuandikishwa, au kutokuwepo pahala mtu alipoandikishiwa kama vile wanafunzi walio likizo.

Ninaomba ninachokidhani kiwe sahihi kwa sababu kama kuna ujanja unafanyika, nina mashaka wanaoratibu uhuni wowote dhidi ya haki za Watanzania, watayaona mabadiliko lakini hawatayafaidi.

Wataongezekaje wakati hutaruhusiwa kupiga Kura ya Rais tofauti na Kituo Ulichojiandikiishia?
 
Haha na wajulikane walitokea wapi ili reconciliation ifanyike, isije wakawa yale makabati
 
Yawezekana ni wale watakaopiga kura kwenye vituo ambavyo hawajaandikishwa. Mfano,watakaopiga kura za Urais kwenye vituo vipya

chief, sidhani kama hili unalolisema litakubalika kwani ni kinyume cha mwongozo uliotolewa jana (nimeusoma kwenye gazeti la Mwananchi)......soma hapa chini sifa kuu 3 za kupiga kura:

1) Raia yoyote wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka 18 ambaye ameandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura na ana kadi ya kupigia kura, iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

2) Mkazi wa kawaida wa eneo analotaka kupiga kura.

3) Mtu ambaye jina lake limeorodheshwa katika daftari la kudumu la wapiga kura au orodha inayobandikwa katika kituo cha kupigia kura.
 
Nimemuona Salumu Mwalimu Akilalamika Itv Kwamba Nec Wamefanya Marekebisho Kwenye Fomu Za Matokeo Kwa Kuongeza Kipengele Cha Idadi Ya Wapiga Kura Walioongezeka Kituoni,wakati Kawaida Fomu Hujazwa Idadi Ya Kura Zilizopigwa Na Kura Zilizo Haribika.Swali Safari Hii Kutakuwa Na Wapiga Kura Watakaongezeka Vituoni,je Watatoka Wapi?Kazi Ipo.

kama mtakumbuka, kulikuwa na idadi ya wapiga kura walioondolewa kwenye daftari kwa sababu ya makosa mbalimbali ya kiuandishi. tayari makundi kadhaa yamelalamika kuhusu kuondolewa kwenye daftar.

Nec walichofanya, walikubaliana na vyama vya siasa watu hao, kwa kuwa ni wakazi, na walionekana wamejiandikisha lkn wamekutwa na makosa, basi waruhusiwe kuchagua.

kwa maana hiyo, kama nec ilikata watu 200, kwa utaratibu uliowekwa, hao 200 wakijitokeza wakiwa na vitambulisho vyao, wataruhusiwa kupiga kura.
 
Why 2015?

Miaka yote mgombea urais anapiga sehemu yoyote, mgombea ubunge anapiga sehemu yoyote ndani ya jimbo lake na mgombea udiwani anapiga ndani ya kata yake kituo chochote. wagombea wote wanaruhusiwa kwa kujaza fomu namba 19. Pia watendaji wa kituo kuanzia msimamizi wa kituo, wasaidizi wake wawili, karani pamoja na mawakala wa vyama wanaruhusiwa kupiga kwa kutumia fomu namba 18. Kama watendaji wanatoka nje ya kata waliyojiandikisha hawatachagua diwani wakitoka nje ya jimbo hawatapiga kura ya mbunge. Watu hawa ni wachache sana wanaweza wasifike hata 10 hivyo tusipende kulaumu na kuzusha mambo tusiyokua na uelewa nayo.
 
chief, sidhani kama hili unalolisema litakubalika kwani ni kinyume cha mwongozo uliotolewa jana (nimeusoma kwenye gazeti la Mwananchi)......soma hapa chini sifa kuu 3 za kupiga kura:

1) Raia yoyote wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka 18 ambaye ameandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura na ana kadi ya kupigia kura, iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

2) Mkazi wa kawaida wa eneo analotaka kupiga kura.

3) Mtu ambaye jina lake limeorodheshwa katika daftari la kudumu la wapiga kura au orodha inayobandikwa katika kituo cha kupigia kura.

kwa sababu ya makosa ya kiuandishi, hiyo category no 3 ihusike. wapo watu wakienda kuangalia majina hawapo, lkn ana kadi na alijiandikisha hapo na wakazi wanamjua. huyo ataruhusiwa kupiga kura
 
Uchaguzi wa mwaka huu unachanga la macho sana mimi jana nilikua naangalia majina ya wapiga kura ya mtaani kwetu nilikuta juna watu wamezaliwa mwaka 1900 wapo kama 10 wakati mtaani kwetu hamna hata mzee hata mmoja aliye zaliwa huo mwaka.
Lakini ninacho shukuru hii ni changamoto kwa chadema na inabidi wasilale na wawe makini sana kwa kila hatua wanayo kanyaga.
 
Back
Top Bottom