Bao la kwanza safe, kuna ukweli????

Habari za mishughuliko wadau?
Watu wa mitaani wanasema kuwa kufanya mapenzi bila kinga kwa bao la kwanza halina madhara yeyote kama mmojawapo kaadhirika na HIV/AIDS, Lakini sharti moja ni kuwa lazima wote kwa pamoja mmefanya romance muda wa kutosha. Hii inatokana na kuwa partners wote watakuwa wametoa majimaji ya kutosha hivyo uwezekano wa kuchubuana hakuna. Pia wanaamini kuwa maambukizi yansababoshwa na michumbuko(damu) na sio majimaji ya wawili hao.
Je wadau kuna ukweli wa kauli hii?

Asanteni kwa michango yenu mizuri ya mawazo!!!

Hayo ni maneno ya mitaani yenye lengo la kuwapotosha watu wasitumie kinga wanapofanya mahusiano yasiyo salama. Si vyema kufanya mzaha na afya yako. Hata kama ukweli ungekuwa wa kuwa kwa asilimia x, huwezi kupata UKIMWI kwa bao la kwanza, pia si justification ya mhusika kuendelea kuhatarisha maisha kwa asilimia hizo zilizotajwa.

Ni vyema kumtafuta mtu/mchumba mwaminifu ambaye hajaathirika au kwenda kupima kama lengo lako ni kushiriki tendo bila kinga. By the way, kwa nini usioe tu kuepukana na kero zote hizo?
 
Hata kabla ya hilo bao la kwanza hizo Romance zenyewe zinatosha kupata HIV.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
majibu unayopewa inaonyesha watu wamehamasika kupata elimu ya afya...very Good yo:shock:
 
Habari za mishughuliko wadau?
Watu wa mitaani wanasema kuwa kufanya mapenzi bila kinga kwa bao la kwanza halina madhara yeyote kama mmojawapo kaadhirika na HIV/AIDS, Lakini sharti moja ni kuwa lazima wote kwa pamoja mmefanya romance muda wa kutosha. Hii inatokana na kuwa partners wote watakuwa wametoa majimaji ya kutosha hivyo uwezekano wa kuchubuana hakuna. Pia wanaamini kuwa maambukizi yansababoshwa na michumbuko(damu) na sio majimaji ya wawili hao.
Je wadau kuna ukweli wa kauli hii?

Asanteni kwa michango yenu mizuri ya mawazo!!!

Ikiwa hali yenyewe ndio hii humo mitaani ukimwi na mimba ya utotoni hazitokwisha africa. halafu kuna kiongozi mzima wa nchi afrika kusini amelala na muathirika halafu anatoe excuse kuwa it ok kwa sababu alikoga baadae. Haya hebu fikiri hilo mkuu wa nchi moja ambayo imeathirika sana na ukimwi ana mentality kama hiyo ni ujumbe gani anawapa wananchi wake?

Mitaani nako utasikia eti mtu hupati mimba as long as mara tu baada ya sex ukinywa maziwa mengi. wengine mara ukismama mara tu umalizapo sex huwezi pata mimba, can you believe that?
 
Back
Top Bottom