Banyamrenge, walowezi wa Kitutsi nchini Kongo DRC ambao wanadai ardhi ili waanzishe taifa lao

BANYAMRENGE, WALOWEZI WA KITUTSI NCHINI KONGO DRC AMBAO WANADAI ARIDHI ILI WAANZISHE TAIFA LAO.

Na. Comred Mbwana Allyamtu (CMCA)
Wednesday-30/06/2021
Kilimanjaro national park Kilimanjaro Tanzania

Banyamulenge ni jamii ya watutsi wanaoishi eneo la Mulenge, eneo hili ni kiunga kilichopo wilaya ya Uvira jimboni Kivu Kusini (Sud Kivu) mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, jamii hii ya kabila la Banyamulenge wa Kivu Kusini halina tofauti yoyote ya kiutamaduni na kijamii na kabila la Watutsi wa Rwanda na Burundi wala wale wa Kivu Kaskazini.

Neno "Banyamulenge" linatafsiriwa kumanisha "watu waishio kwenye mlima Mulenge", hivyo Wanyamrenge ni kabila linolopatikana katika eneo la tambarare ya Itombwe, kusini mashariki mwa Kiunga cha Kavivira ndani ya wilaya ya Uvira, Wanyamrenge walichagua jina la "Banyamulenge" miaka ya 1970 ili kuepuka kuitwa "Banyarwanda" na kuonekana kama wageni au wahamiaji, baadhi yao pia hujiita Banya-tulambo na Banya-minembwe, yote hii ni kuepuka tu kuitwa Banyarwanda.

WaBanyamulenge hawa huzungumza Kinyamulenge, lugha hii ni mchanganyiko wa Kinyarwanda (lugha rasmi ya Rwanda) na Kirundi (inayozungumzwa haswa nchini Burundi) japo inatofautiana katika fonolojia na mofolojia kadhaa baina ya lugha hizi mbili japo kuna mwingiliano mkubwa wa tamaduni na historia.

Wanyamrenge ni kabila lilokuja kupata umaharufu kwenye Kile kilichokuja kuitwa maasi ya Banyamulenge kupitia "Operation Banyamrenge" ambayo nitaielezea huko mbeleni, maasi haya ndio yaliyokuja kusababisha Vita ya Kwanza ya Kongo ya mwaka 1996-1997 na ile Vita vya Pili ya Kongo vya mwaka 1998-2003.

Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 1990 iliyofanywa huko Kongo mashariki na mtafiti René Lemarchand anasema idadi ya Banyamulenge huko katika Jimbo la Kivu kusini ilikuwa inafika karibu watu 50,000 hadi 70,000, huku idadi ya Banyamrenge nchini Kongo kote ilikuwa inafika karibu 100,000-120,000, idadi hii ni karibu asilimia 9 ya wakazi wote wa mkoa wa Kivu kusini na 4% ya wakazi wote nchini Kongo kwa kipindi hicho.

Asili ya Wanyamrenge...............

Kabila la Banyamrenge linatokana na neno "Mulenge", neno hili mulenge ni neno ambalo kihistoria linarejelea mlima "Mulenge" uliopo katika eneo la mashariki mwa jimbo la Kivu Kusini, katika mji wa Uvira ukiwa unaelekea katika miinuko ya milima ya Katumba, eneo lenye rutuba na aridhi na mito midogo miwili, ambao ni mto Uvira na mto Mlolongo, eneo lote hilo lipo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, karibu na mpaka wa Burundi na Rwanda.

Banyamrenge ni jamii ya Bahima kutoka kabila la Watutisi, Banyamulenge ni jamii yenye uhusiano wa moja kwa moja na jamii ya Bahima, hawa Wanyamrenge pia hufahamika kama Banyarwanda, kihistoria Banyamulenge walihamia huko Kongo karne ya 17 wakitokea Rwanda na Burundi.

Kikundi cha Kwanza cha Banyarwanda kuhamia Kivu Kusini ni kile kilichofika eneo hilo la Mulenge na kuweka makazi yao mwaka 1850, kisha kikafata cha pili kilichofika mwaka 1880, Sababu zilizopelekea kuhamia huko ni kutokana na kutofautiana na Mwami Rwabugiri wa ufalme wa Rwanda juu ya ushuru uliowekwa kuwataka kulipia mifugo yao.

Kikundi cha Tatu, walikuwa ni Watutsi walio kimbia vita vikali vya urithi vilivyoibuka mwaka 1895 baada ya kifo cha Rwabugiri, Kikundi hiki kilikuwa na Watutsi na Wahutu jamii ya Abagaragu, ambao walikuwa wamekataa mvutano wa kikabila, hivyo wakaamua kuhama na kutafuta makazi mapya, hawa walihamia eneo la Bonde la Ruzizi kwenye Uwanda wa Itombwe, Uwanda huu una urefu wa mita 3000 kutoka usawa wa bahari, uwanda huu haufai kwa kilimo lakini unafaa kwa malisho ya ng'ombe, hivyo wakaweka makazi hapo.

Kikundi cha Nne, ni kile kilichopo eneo la Luberizi, hawa ni Watutsi jamii ya "Wanyakarama" waliokuwa chini ya Kingdom ya Burundi chini ya Mwami Rusizi, Ila mipaka ya WAKOLONI iliyofanywa mwaka 1899 iliwaweka hawa watutsi ndani ya Kongo DRC, hivyo eneo hili la Luberizi lipo Jimboni Kivu kusini na hawa Wanyamrenge wa nyakarama wanazungumza kirundi.

Kikundi cha Tano, ni kile kilichopo Jimbo la Ituri, hawa Wanyamrenge wa hapa hufahamika kama WAHEMA/ Wahima sawa na Wahima wa Uganda ambao huzungumza lugha Moja na wanyankole/Watoro wa Uganda, hawa waligawanywa na mpaka ulio wekwa mwaka 1884 baina ya Waingereza na Uberigiji.

Wahamiaji wengine wa Banyarwanda waliendelea kuhama na kuwasili Kongo mashariki haswa miaka ya 1925 hadi 1929, Kuanzia miaka ya 1930, wahamiaji wa Banyarwanda waliendelea kuhamia Kongo kutafuta kazi, na marisho ya Mifugo yao, utitiri mkubwa wa wahamiaji wa Kitutsi ulishuhudiwa mwaka 1959-1960 kufuatia "Mapinduzi na Uhuru wa Rwanda" ulio ongozwa na Wahutu wengi chini ya chama cha PrepeHutu chini ya Grégoire Kayibanda aliyekuja kuwa rais wa kwanza wa Rwanda.

Serikali ya kikoloni huko Kongo ya Uberigiji ilitangaza kuwatambua Wanyamrenge Mnamo mwaka 1924, iliwatambua kama wafugaji na kupewa nyanda kubwa ya Kivu kwa kulisha Mifugo yao, hii iliwafanya kujiimarisha zaidi na kuwa na himaya kubwa ukanda wa mashariki mwa Kongo, kutambuliwa huko kuliwafanywa kuingizwa kwenye sarafu ya Noti ya faranga 10 ya Kongo ya kipindi cha UKOLONI wa Wabelgiji, noti hiyo ilionyesha picha ya Watutsi wa Banyamrenge wakicheza Ngoma ya Intore.

Baada ya uhuru wa Kongo mwaka 1960 serikali ya Kasavubu na baadae ile ya Mobutu iliwafuta kuwatambua Wanyamrenge kama Makabila ya Kongo, walionwa kama wakimbizi hivyo walitakiwa kurejea kwao Rwanda, Uganda na Burundi, hatua hiyo ikapelekea Banyamulenge wengi kujiunga na Uasi wa Simba wa mwaka 1964-55, uasi huu ulikuwa ukiuunga mkono serikali ya Lumumba., na waliongozwa na Anttone Kizenga na Mulele.

Kufatia hatua hiyo jeshi chini ya Mobutu ilipogundua uhusika wa Wanyamrenge kuwasaidia waasi wa Simba, jeshi la Mobutu lilivamia kwenye makazi ya Wanyamrenge na kuua ng'ombe pamoja na kuchoma chakula chote, Watutsi hao kuona hivyo wakaamua kumuunga mkono Mobutu na kisha kupewa silaha kutoka kwa wanajeshi wanaomuunga mkono Mobutu na kusaidia kupambana na waasi, baada ya vita hivyo kumalizika Mobutu aliwahaidi kuwatambua lakini hakufanya hivyo kwa miongo kadhaa.

Hata hivyo..............

Wanyamrenge waliendelea kujipanua eneo lote la mashariki ya Kongo, Wengi wao walihamia kusini kuelekea eneo la Moba na Kalemi, ambapo kwa sasa ni jimbo la Tanganyika, wakati wengine walihamia kwenye uwanda wa Ruzizi, ambapo huko waka twaa aridhi kubwa yenye rutuba na kuwa machifu eneo hilo ambapo walichanganyikana na Wabarundi na kufuga ng'ombe ambapo huko walijishugurisha na kazi ya uuzaji wa nyama na maziwa, Wafugaji hawa walienea ndani ya wilaya tatu za Mwenga, inayokaliwa na watu wa Lega, Fizi inayokaliwa na watu wa Bembe, na Uvira, inayokaliwa na watu wa kabila la Vira, Bafuliro, Wabwale na WaBarundi.

Mvutano wa kikabila dhidi ya Watutsi wa Kinyamrenge na serikali ya Mobutu ulizidi kuongezeka kufuatia mauaji ya halaiki ya Wahutu nchini Burundi ya mwaka 1972, hatua hiyo ilipelekea Wanyamrenge kuanza kudai vitambulisho vya wakaazi wa Mulenge na kutambuliwa kama raia wa Kongo DRC, hali hii ilipelekea Mvutano wa kisiasa wa mwaka 1971-1992 baada ya kupitiswa sheria ya uraia ya mwaka 1971… kisha ukaibuka Mgogoro wa mwaka 1993-1998 kufatia sheria iliyowaruhusu kupiga kura lakini ikawazuia kuwania nafasi yoyote ile ya uongozi wa kisiasa.

Jambo hili la kuwatenga Wanyamrenge likachukua sura nyingine na kuzua kizaaza kwenye utawala wa Mobutu, unaweza kusema kuwa mwisho wa zama za Mobutu Seseseko ulichangiwa pakubwa na Wanyamrenge, ntaeleza kidogo hapa.

Wanyamrenge na kile kilichoitwa Mkataba wa Lemela...............................................

"Mkataba wa Lemela" ni mkataba ulioandaliwa na Mataifa ya Magharibi kufadhili vikosi vya waasi wa kabila la Wanyamrenge ambao ndio chanzo cha Maktaba ili kuiondoa serikali ya Mobutu na kuigawa Kongo DRC ili Wanyamrenge wapate nchi mashariki mwa Kongo.

Lakin pia kumekuwepo na dhana nyingine inayo zihusudu Rwanda na Uganda juu ya hiki kinachoitwa "mkataba wa lemela" Kwa mfano, inadaiwa kuwa Kikosi cha waasi wa M23 kinafanya kazi kwa maelekezo ya serikali ya Rwanda na kimefanikiwa kwa kiasi kuinua uchumi wa Rwanda kwa kudhibiti maeneo kadhaa ya machimbo ya madini, hofu ya mataifa makubwa juu ya M23 kutishia maslahi yao ndio iliyopelekea kuwatumia marais wa Africa kusini, Jacob Zuma na Tanzania, Jakaya Kikwete kutumiwa kwa mgongo wa AU, kupeleka majeshi yao Congo kupambana na M23 tu wakati kuna vikosi lukuki vinavyofadhiliwa na kupewa silaha kutoka magharibi.

Hapa, dhana hii ikiwa ni kweli, basi viongozi hao wa Tanzania na Africa Kusini wanaingia katika historia chafu ya kusaidia upande mmoja unaoibia Congo kwa kisingizio cha kutunza Amani. Yawezekana pia walikuwa na maslahi yao binafsi badala ya maslahi ya Congo na mataifa yao.

Turejee kwenye Makataba wa Lemela...............

Mkataba wa Lemela ni Nini? Kwa mujibu wa upembuzi wa wabobezi wanaeleza kuwa Mkataba huu ni makubaliano yaliofanywa na viongozi wa Banyamrenge, Rwanda, Uganda, Sudani kusini na Ethiopia pamoja na kiongozi wa AFDL Laulent kabila juu ya kile Kinachoitwa operesheni maalumu ya kumuondosha Mobutu kupitia utekelezaji wa “Makubaliano ya Lemera” ya mwaka 1996 yenye shabaha ya kuigawa nchi hiyo kubwa Makubaliano yalifanywa kati ya Laurent Desire Kabila, akiwa kiongozi wa chama cha “kuikomboa Kongo” kutaka kuondosha utawala wa dikteta Mobutu Sese Seko, kwa upande mmoja, na wapiganaji wa Kinyamrenge kwa ushikiano na wapiganaji wa Kinyarwanda kutoka Rwanda na Mashariki mwa Kongo.

Makubaliano ambayo yalifanyika kwenye vilima vya Lemera vilivyoko Kivu ya Kusini na kujulikana kwa jina hilo, la "mkataba wa lemela" yalitaka Kabila, baada ya kuwa rais wa Kongo, aruhusu mikoa miwili ya Kivu Kaskazini na Kusini kuwa makazi ya Watutsi wa kabila la Kitutsi, Taarifa zinaonyesha makubaliano yaliandaliwa mapema mjini Kigali na pale Lemera yalikuwa yanazinduliwa tu, Ilikubaliwa wakati huo kwamba hiyo ndiyo ingekuwa “asante” kwa Wanyamrenge ambao wamekuwa wakinyanyasika kwa miaka 40 ya kutafuta haki ya kutambuliwa kuwa raia, Wanyamrenge walisimamiwa na Rwanda katika kile kilichoitwa “ ukombozi Wanyamrenge nchini Kongo.”

Laurent Desire Kabila alikuwa tayari amechoka Kwa takriban miaka 20 alikuwa akipambana na utawala wa Mobutu Sese Seko kwa miaka mingi bila mafanikio hivyo aliamua kuungana na Wanyamrenge ili tu kutimiza ahadi yake ya kuitawala Kongo, hivyo Mwaka 1996, mjini Kigali, Rwanda kulikuwa kimeundwa kikundi cha wapiganaji waliojiita “wapinzani wa dikiteta Mobutu.” Hawa walikuwa Wakongomani na Wanyarwanda kutoka Rwanda na wengine walikuwa ni Wanyamrenge waliokuwa wakiishi mkoa wa Kivu Kusini, Mashariki mwa Kongo, Katika kundi hiki alikuwemo Mkongomani, Jenerali Andre Kisasi Ngando, askari mtaalam wa kusomea.

Huyu Jenerali Andre Kisasi anadaiwa kupata mafunzo nchini Cuba, Ujerumani na Bulgaria, alikuwa akiongoza Wakongomani wapatao 600 katika kikundi hicho, Wakati kikundi hicho kinataka kuanza vita, kilitaka kuwa na msemaji, Kikundi hicho kilikwenda Tanzania, kiliomba ushauri kwa Mwalimu Julius Nyerere “ambaye nae kwa ushauri wa TISS aliwapa Laurent Desire Kabila kuwa msemaji wa wapiganaji.”

Mwanzoni mwa vita ya kumg’oa Mobutu kikundi hiki kilijulikana kama cha Wanyamulenge, Dunia nzima ikaambiwa na kuaminishwa kuwa hayo yalikuwa “maasi ya Wanyamulenge.” Wanyamulenge walipaza sauti zao kudai haki ndani ya nchi yao kwa kudai kutambuliwa, Vita vilianza kwa propaganda kuu kwamba serikali ya Mobutu haitambui Wanyamulenge ambao walidai ni raia wa Kongo, inawanyanyasa na inawanyima uraia, Haya yalikuwa madai makubwa sana yaliyovuta hisia kali na huruma kwa wapiganaji, wapinzani, chini ya Jenerali Andre Kisasi Ngando, na msemaji mkuu wao Laurent Kabila waliteka, kama mchezo, mji mkuu wa Kivu Kaskazini, Goma.

Kama Mchezo Mapigano yakanoga...............

Wakavuka Ziwa Kivu na kuingia Kivu Kusini, ilikuwa baada ya kukamata mji wa Bukavu, makao makuu ya Kivu Kusini na sehemu nyingi za jimbo hilo, wapiganaji wa Banyamrenge na Kinyarwanda waliingiza pendekezo la rais ajaye wa Kongo, kutoa Kivu Kaskazini na Kusini, Lakini kabla suala hilo nyeti kupewa uzito unaostahili, wapiganaji wa Banyamrenge na Kinyarwanda baada ya kuteka Bukavu, wanadaiwa kuanza kupora mali, magari, vifaa vya nyumbani, dawa katika maduka, hatua ambayo ilielezwa kuwa ni kosa kubwa katika mapambano jambo ambalo litaondoa uhamishaji wa wakazi wa Bukavu na maeneo mengine kuwaunga mkono Katika kufikia azima yao.

Jenerali Ngando alipinga uporaji usiomithilika, jambo ambalo lilimletea uhasama kwa baadhi ya wapiganaji, Kuona hivyo, Laurent Kabila akamsaliti Jenerali Ngando, Ngando anasemekana kuuawa siku chache baada ya kutofautiana na wapiganaji juu ya uporaji, Inaelezwa kuwa alimiminiwa risasi na kuuawa na mwili wake kuchomwa moto katika mbuga ya wanyama ya Virunga huko Kivu kaskazini.

Kabila aliulizwa mara nyingi juu ya Ngando, alikuwa na majibu tofauti akiwa bado msituni alisema Jenerali Ngando amekamatwa na majeshi ya serikali na mara ametekwa na wanamgambo wa Mai Mai, baadaye Kabila alisema Ngando alijeruhiwa na kupelekwa Ujerumani kwa matibabu na wakati akiwa rais, aliwaambia waandishi wa habari mjini Kinshasa kuwa Ngando alikuwa askari kama askari wengine na kwamba alikufa kwenye mapambano.

Baada ya kifo cha Jenerali Ngando ndipo Kabila aliingizwa kwenye makubaliano ya kumega Kongo. Kwanza, kikundi cha wapiganaji kiligeuzwa jini ili kuakisi lengo la kitaifa na kisionekane kama kikundi cha kikabila ili kuungwa mkono na makabila yote nchi nzima, hivyo kikabadili jina na kuitwa chama cha AFDL (Alliance de front Democratique pour la Liberation du Congo).

Kabila akapanda cheo na kuwa kiongozi wa chama cha ukombozi wa Kongo kutoka kuwa msemaji tu wa wapiganaji wa Banyamrenge, Baada ya kuundwa kwa AFDL, jina la Wanyamulenge likatoweka kabisa Wapiganaji wakaitwa waasi wa Kongo, Taarifa zinasema kabla wapiganaji kutoka Bukavu na kuanza safari iliyomfikisha Kabila madarakani, waliingia katika mkataba ambao ndio umekuja kuitwa “Makubaliano ya Lemera.”

Viongozi wakuu wa wakati huo wa baadhi ya nchi walipata nakala ya makubaliano hayo ya kumega Kongo-DRC, Miongoni mwa nchi hizo ni Tanzania, Namibia, Uganda, Burundi, Zambia, Ethiopia, Eritrea, Zimbabwe, Angola, Namibia, Sudan na baadhi ya nchi za Ulaya na Marekani.

Makubaliano ilikuwa ni pamoja na kufanya mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini kutawaliwa na Wanyamrenge au Banyarwanda wa Kitutsi kwa ushirika na mataifa ya Rwanda, Burundi na Uganda, na kwamba utawala huo ambao ungefanya kazi kwa ushirikiano na serikali ya Kabila, ungetekelezwa kwa awamu tatu katika kipindi cha miaka 10 kuanzia 1998.

Chini ya mpango huo, raia wa Kongo, wakazi wa Kivu Kaskazini wangehamishiwa Kivu Kusini, “taratibu na kwa utulivu huku makazi yao yakichukuliwa” na wavamizi, Hatua ya kwanza isingekuwa ngumu kwani Rwanda ingedai kuwa inapambana na wanamgambo wa Kihutu walioitwa Interhamwe ambao itaelezwa kuwa wanatishia amani nchini Rwanda Hivyo ndivyo imekuwa ikifanya hadi sasa.

Makubaliano yalieleza kuwa kuchukuliwa kwa miji ya Goma na Butembo mkoani Kivu Kaskazini, sharti iwe hatua ya kwanza kwa kuwa hayo ndiyo maeneo yenye upinzani mkubwa, Kufanikiwa kwa awamu ya pili, kungetegemea mafanikio ya awamu ya kwanza, makubaliano yanadaiwa kueleza, Wafuatiliaji wa mahusiano ya Rwanda na Kongo wanasema ingawa mpango huo ulishindikana kutekelezwa kuanzia mwaka 1998, kuingia kwa majeshi ya Rwanda nchini humo hivi sasa, ni utekelezaji wa hatua ya kwanza ya Makubaliano ya Lemera, na tayari miji ya Goma na Butembo iko chini ya kile kinachoitwa “majeshi ya ushirikiano” ya Rwanda na Kongo.

Awamu ya pili ingekuwa kujaza wakazi wa Kaskazini katika Kivu Kusini na kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo wazawa wangeenguliwa, kukosa uongozi na hivyo kunyimwa sauti.

Hatua nyingine ilikuwa kuanzisha benki ya kusaidia wavamizi katika Kivu mbili, kujenga nyumba zipatazo 600,000 na kujiimarisha katika nchi ya kigeni Kongo, Inaaminika kuwa Kabila alikubaliana na masharti ya makubaliano kwa kuwa lengo lake lilikuwa moja tu, Kuingia ikulu ya Kinshasa kwa msaada wowote kutoka kwa yeyote, awe Mungu au shetani, Ilikuwa baada ya makubaliano hayo, Kabila alisonga mbele na hatimaye kushinda na kuingia ikulu ya Kinshasa akiwa na wapiganaji wa Rwanda, akiwemo aliyekuwa mkuu wa majeshi wa Rwanda, ambaye sasa ni wazili wa ulimzi wa Rwanda James Kabarebe.

Baada ya kuingia ikulu, Kabila aliwasiliana na Mwalimu Julius K.Nyerere mjini Dar es Salaam chini ya uratibu wa TISS, chaguo la Tanzania lilikuwa nikuzuia uuzwaji huo wa ardhi ya Kongo, Mashauriano yaliyochukua sura dhahili ya nguvu ya Tanzania katika ujasusi yalimpa nguvu Kabila na alipowarejelea wabia wake aliwageuka dhahiri shahiri.

Ilikuwa baada ya miaka miwili ya urais, alitangaza, tena kwa jeuri, kuwa wageni wote waondoke nchini Kongo aliongeza kwa kufafanua, kwamba Wanyarwanda na Wanyamrenge warudi kwao na kusema anawashukuru kwa kazi waliyofanya.

Kabila alinukuliwa akisema kuwa hayo (Makubaliano ya Lemera) ni “makubaliano ya porini” na kwamba yeye hakuwa na madaraka ya kuuza nchi, alisema hakatai kuwepo mkataba, lakini akataka hilo “lipelekwe kwa wananchi kupitia bungeni ili wananchi wenyewe waamue.”

Kilichomshangaza zaidi Kabila, baada ya kutangaza kuwa Wanyarwanda warudi kwao, ni kwamba aliyekuwa wa kwanza kuondoka na kukimbilia Afrika Kusini, alikuwa waziri wake wa mambo ya nje aliyeitwa Bizima Karaha (Bizimana Karahamuheto), Katika mshangao na labda kejeli, Kabila alisema, “Kumbe nchi ilikuwa imevamiwa! Hata waziri wangu wa mambo ya nje alikuwa Mnyarwanda?” Hiyo ilifuatiwa na kufukuzwa kwa James Kabarebe aliyekuwa mkuu wa majeshi ya Kongo na kurudi Rwanda, alipo fika Rwanda aliteuliwa kuwa mkuu wa majeshi ya Rwanda.

Kabila aliuawa kabla hajamaliza kunyukana na wanyamrenge chini ya usimamizi wa Rwanda, Kabila aliuawa na mmoja wa “watoto” wake yaani vijana wadogo waliokuwa watu wa karibu sana na waliomlinda tangu akiwa msituni, Kuna maelezo tatanishi juu ya kifo chake, Kuna wanaodai aliyemuua alitumwa na waliokuwa wakitaka atekeleze makubaliano ya Lemera, lakini wengine wanadai ni karata za nchi za Magharibi, Kwa kuwa Jonas Savimbi aliuawa katika mwaka moja tu baada ya kifo cha Kabila, inadaiwa kulikuwa na mkono wa mataifa makubwa, hili likitaka kuingia Kongo na hivyo kuomba msaada wa kuondoshwa kwa Kabila huku likiwezesha kukamatwa na kuuawa kwa Savimbi, japo hili hazijafafanuliwa mpaka Sasa.

Wanyamrenge kwenye Vita vya M-23......................................

Vita ya M23 ilipoanza Banyamulenge wengi waliunga mkono na kujiunga na kikundi hicho kilichoongozwa na Kundabatware mtutsi wa Kutoka Kivu kaskazini, Vuguvugu la Waasi la M-23, liliungwa mkono na Rwanda, Licha ya kwamba wengi wa Banyamulenge walipinga uungwaji mkono wa Rwanda huku wakitaka vuguvugu hilo kutambulika kama vita ya wanyamrenge ndani ya Kongo inayoongozwa na Banyamrenge jamii ya Banyamasisi, ambao ni jamii ya watutsi wa kaskazini mashariki mwa Kongo, aliunga mkono M23 ili kuongeza msukumo wa madai yao ya kupewa haki ya kutambuliwa na kusikilizwa madai yao.

Kupitia M23 hawakufanikiwa kwakuwa vuguvugu hilo lilibeba sura ya ujasusi wa Rwanda nchini Kongo, hivyo wanyamrenge wakawa wamefeli, japo waliendeleza madai yao yenye matakwa matatu;

Moja, wanaitaji kupatiwa jimbo la kiutawala Katika ene la mashariki mwa Kongo, yani jimbo la Kivu kusini na kaskazini yagawanywe na kupatikana jimbo lao ambapo jiji la Uvira ndio iwe makao makuu ya jimbo lao.

Pili, kutambuliwa kwenye sheria zote na kupewa haki bila kiluwepo kizuizi chochote.

Tatu, ikiwa yote yatashindikana basi eneo la mashariki mwa Kongo ligawanywe ili wao wapate nchi yao, yani nchi ya asili ya mababu zao.

Madai yote hayo serikali ya Joseph Kabila iliyapuuzia mwaka 2013 ilipo igawa upya nchi katika majimbo mapya, Kabila aliwapatia wilaya iliyoitwa Minembwe huko Kivu Kusini, na kukubali dai lao la pili japo sheria ya uraia iliyofanyiwa mabadiriko mwaka 2012 aikuwapa fully rights za uraia, ntaeleza hili huko chini.

Hata hivyo..............................

Mpaka sasa kuna idadi kubwa ya Banyamulenge wanaoishi Rwanda kama wakimbizi kutoka Kongo na wengine ni raia wa Rwanda wanao faidika na ulinzi wa serikali inayoongozwa na Watutsi nchini Rwanda, Baadhi yao wanashikilia nyadhifa za juu serikalini nchini Rwanda na wengine wamewekeza katika uchumi nchini Rwanda, hawa hutumia pesa zao kusaidia harakati za kutafuta ukombozi wao huko mashariki mwa Kongo.

Kwa sasa huko Kongo (DRC), Banyamulenge wamekuwa sehemu ya jamii ya wasomi katika siasa na jeshi, Serikali ya Joseph Kabila mwaka 2006 ilipitisha sheria ya kuwatambua kwa kupewa haki za uraia, japo ni wanyamrenge wa kuanzia mwaka 1880 mpaka mwaka 1959 tu ndio wanao tambuliwa kisheria kama RAIA wa Kongo, pia mabadiriko ya sheria ya mwaka 2012 imeongeza haki ya kuweza kugombea uongozi katika nafasi za kisiasa.

Kuwapa hadhi ya uraia wanyamrenge imesababisha kuongezeka kwa mivutano na jamii zingine za wenyeji huko Kivu kaskazini na Kusini na maeneo mengi nchini Kongo, ambapo raia wengine nchini Kongo DRC wamedai kuwa hao wanyamrenge wamekuwa wakipokea upendeleo na serikali ambapo wakipewa kipaumbele kila mahali jambo ambalo hawastahili, mtazamo huu unashikiliwa sana na makabila mengi kutoka huko Kivu Kusini ambayo daima yamekuwa yakiamini kuwa wanyamrenge ni Watutsi kutoka Rwanda na Burundi (Watutsi), hivyo hawastahili kupewa kipaumbele kuliko wao ambao ni Wakongo kiasili.

Kufatia upendeleo huo kumepelekea kuibuka machafuko ya mara kadhaa baina ya Banyamrenge na Makabila ya wenyeji huko mashariki mwa Kongo, hasa makabila yanayozunguka wilaya yao ya Minembwe, hii ni kutokana wanyamrenge kupewa eneo lao na Joseph Kabila mwaka 2013 ambapo walipewa wilaya mpya iliyoitwa Minembwe, huko Kivu Kusini,

Hata hivyo wanyamrenge au Banyamulenge wameendelea halakati zao za kuunda nchi yao ndani ya Kongo DRC ikiwa kama hawatapewa haki ya kupewa jimbo lao huko mashariki mwa Kongo, mpaka Sasa madai yao ni kupewa jimbo kamili au waendeleze vuguvugu la kuunda nchi yao huko mashariki mwa Kongo, hata hivyo wanyamrenge wanaungwa mkono na Rwanda, Uganda na Burundi kwa kipindi furani, mataifa ya Marekani na Uingereza pia huunga mkono mkono tasisi ya Banyamrenge diaspora ambayo ndio hueneza adhima ya kuwa na aridhi ndani ya Kongo DRC, hukusanya pesa kuwezesha harakati hiyo, ikiwa ni pamoja na kutafuta uungwaji mkono kimataifa, wameanzisha kikosi cha kijasusi nchini Rwanda kufadhiri harakati ya kufufua mpango mkakati wa kurejea Kongo kuunda taifa lao huko mashariki mwa Kongo DRC ambapo watapaswa kuunda taifa lao, kikosi hicho hutajwa kuwa na baraka na serikali ya Kigali.

Hawa ndio wanyamrenge, walowezi wa kitutsi nchini Kongo DRC ambao wanadai aridhi ili waanzishe taifa lao, simulizi yao ni sawa na Israel na Palestine huko mashariki ya kati.

Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
Wako Mjoli wa Historia na diplomasia ya ulimwengu.

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
Copyrights of this article reserved
written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika Kwa mawasliano
Comred Mbwana Allyamtu

Kwa Tanzania
+255679555526.
+255765026057.

Kwa Rwanda
+250733153930
+250788214234

Kwa DRC
+243 977 860 824
Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com

Copyright 2021, All Rights Reserved.

Maktaba Kuu.View attachment 1835883View attachment 1835884
hii kitu taaamu saaana kutoka maktaba za siri
 
Safi sana, M23 ndio maana tunawavuruga kwelikweli Ila sasa tunatumika bila kujua kwamba hapo tumewekwa kama chambo tu kusimamia maslahi ya wazungu wa upande mmoja maana nao M23 Wana wazungu wa upande mwingine ambao wanataka wakipewa eneo lao wawauzie madini nk.
 
Story iko pouwa ila umesahau tu kusema kua katika majeshi yaliomsaidia kulikua pia na majeshi kutoka tanzania ndio maana Rwanda walishindwa kabisa kumpandikiza mtu wao kuongoza Kongo.Na jeuri ya Laurent Kabila ililetwa kwa sababu ya majeshi ya Tanzania,.Nakumbuka walinzi wa Kabila wa mwanzo kabisa karibu wote walikua watanzania, kuna jamaa nilisoma nae UDSM alikua Tiss ndio alikua mlinzi wake mkuu wa karibu, nafikiri baadae waliondoka na ndipo Kabila alivyokuja uawa na kijana mlinzi wake Rasheed baadae .
 
Vjana wangekuwa wanaasoma mambo Kama haya yakuijua dunia

Kumbe vita hii ya bakongolee mzizi upo hapa

Swal kwa mleta mada Kuna Hawa waasi wa MAIMAI nao n moja ya jamaii za banyamulenge au ni tofauti?

Kama tofauti wao wanapigana na adui gani?

Kifupi kaz nzuri sana
 
MAI MAI ni wapiganaji wa kibembe huko kaskazini mashariki ya Kongo.ni kama waha na wamanyema tu.
 
Wale wahutu waliokimbilia DRC wanaitwaje? Rwanda haiwezim kuwa stable kama DRC itaendelea kuwa vile. Watapata tabu tu. Ni suala la muda
 
Hata Bongo huku washaanza Kudai ardhi
 
Back
Top Bottom