Banning pregnant girls from school is against the laws of Tanzania

Ulichokiandika hapa hakina ukweli wowote. Kule Zanzibar wanafunzi wajawazito wanaruhusiwa kurudi shule na hiyo dhana yako potofu kwamba utakuta shule nzima ina wazazi haina ukweli wowote ule. Wanafunzi wanaopata ujauzito ni 8% tu ya wanafunzi wote na hata katika nchi nyingine duniani ambazo zinaruhusu wanafunzi wajawazito kurudi shule hiyo dhana yako potofu kwamba shule nzima itakuwa ni ya wajawazito bado haijatokea katika nchi yoyote ile.

Nasisitiza, "Kuzuia kuendeleana shule za Serikali" kwani nchi hii waliwahi kuruhusiwa kuendelea na shule lini hata useme rais amezuia? Kauli ya Rais maana yake "kuneni vichwa" jinsi ya kuwasaidia hao wasio na uwezo sio kufikiria warudi shule za serikali madhara yake baada ya robo karne ni makubwa kuliko faida. iko siku mtajikuta shule zima ni ya wazazi mtaanza kuulizana nani aliruhusu hiyo.
 
JAMII ILIYOKOSA MAADILI INAWEZAJE KUMHUKUMU MTOTO MJAMZITO?

pregnant-teenage-300x163.png

Na Christian Bwaya,

MATUKIO ya watoto wa kike kupata ujauzito yanaongezeka. Kwa mujibu wa Takwimu za Elimu (BEST) wanafunzi 4,718 wa sekondari kwa mwaka 2012 na 3,439 mwaka 2015 walikatishwa masomo yao kwa sababu ya ujauzito. Takwimu kamili hazipatikani lakini kwa elimu ya msingi hali haina tofauti kubwa. Hata hivyo, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA) linadai kwamba msichana mmoja kati ya sita wenye umri wa miaka 15 hadi 19 wakiwamo wasiokuwapo shuleni hupata ujauzito kila mwaka hapa nchini. Ni wazi kuwa mimba za utotoni ni tatizo kubwa katika jamii yetu.

Aidha, matukio ya mimba yanakwenda sambamba na ongezeko la ngono holela miongoni mwa wanafunzi. Utafiti uliofanywa na Method Kazaura na Melkiory Masatu mwaka 2009, ulibaini kwamba asilimia 32 ya watoto na vijana wenye umri wa miaka 10 hadi 19 walikuwa wanashiriki vitendo vya ngono. Wengi wao hawana elimu ya afya ya uzazi. Jarida la African Population Studies toleo Na.29 la 2015 linathibitisha matokeo hayo.

Kwa mujibu wa Eunice Muthengi na Abebaw Ferede waliofanya utafiti uliochapishwa na Jarida hilo, idadi kubwa ya vijana hapa nchini wanakosa taarifa za msingi ambazo zingeweza kuwasaidia kufanya uamuzi unaoongozwa na uelewa. Hata hivyo, vijana hawa wanapopatiwa elimu ya afya ya uzazi mapema, asilimia 52 wanaonekana kuweza kuchelewesha uamuzi wa kuanza ngono.

Tunaishi kwenye nyakati zenye uholela mkubwa wa taarifa. Changamoto, hata hivyo, ni kukosekana kwa elimu na huduma za afya ya uzazi kwa vijana. Wazazi, kwa mfano, wameendelea kuogopa kuzungumza kwa uwazi masuala yanayohusiana na ngono kwa imani kwamba ni kinyume na utamaduni wetu. Mtoto huyu anapokwenda shuleni anakutana na walimu wasio na ujasiri wa kuyashughulikia mambo haya kwa uwazi. Katika mazingira haya ya uhaba wa taarifa sahihi katikati ya uholela wa taarifa zinazohimiza ngono, ni wazi uamuzi unaofanywa na wanafunzi utakuwa batili.

Pia, tunafahamu watu wazima wakiwamo wazazi na walimu wameshindwa kuonesha mfano mwema wa kimaadili. Maadili yamebaki kuwa hotuba za majukwaani wakati maisha ya watu faraghani ni jambo jingine kabisa. Wazazi wanaohubiri maadili hadharani, ndio hao hao wanaofuga ‘nyumba ndogo.’ Walimu waliopaswa kuwaelekeza watoto njia sahihi ya kufuata ndio wanaowashawishi wanafunzi wao kushiriki nao vitendo vya ngono. Kwa ujumla, jamii inayomzunguka mtoto inamwaminisha kuwa ngono holela ni sehemu ya maisha.

Jambo la kushangaza ni kwamba mtoto anapoiga yale anayoyaona na kujiingiza kwenye vitendo vya ngono jamii hiyo hiyo inamshangaa. Hukumu inakuwa kubwa zaidi inapotokea binti amepata mimba. Huu ndio unakuwa wakati wa kumkemea mtoto kwamba alichokifanya ni kinyume na maadili. Msichana mwenyewe wakati huo anashangaa imekuwaje kosa lake liwe kubwa kuliko yale anayoyaona yakifanywa na watu wazima wanaomzunguka.

Aliyempa mimba anaamini tatizo ni la binti mwenyewe. Kwa hiyo anamkana. Wazazi, kwa upande wao, wanachukulia mimba kama aibu mbele ya macho ya jamii. Ili kuonekana hawakuzembea, wengi wao nao humshutumu na wakati mwingine kumtenga kuonesha kwamba hawakubaliani na uvunjifu wa maadili uliofanyika.

Msichana huyu akiwa bado katika hali ya kushangaa inakuwaje tumbo linaendelea kuwa kubwa, anajikuta akikabiliana na mkono wa serikali isiyotaka kuona wajawazito wanaendelea na masomo. Watu ambao awali hawakuwa na utaratibu wowote wa kumsaidia kuufahamu mwili wake, wanakuwa wa kwanza kumfukuza ili iwe fundisho wa wanafunzi wengine wasioheshimu maadili.

Mtoto huyu anarudi mtaani akiwa hana mtu anayeweza kuvaa viatu vyake na kujaribu kumsaidia. Kila anayezungumzia tatizo lake anamlaumu yeye. Wengine watasema alijipeleka mwenyewe kwa wanaume. Wengine watasema, ni kiherehere chake kimemponza. Hatua zozote za kumsaidia binti huyu zinatafsiriwa kama kuunga mkono tabia yake mbovu. Kwa kuwa hakuna anayethubutu kuonekana hana maadili, basi kila mtu anashindana kumshambulia ili nay eye aonekane ni mlinzi wa maadili ya jamii.

Ikiwa binti huyu masikini atajifungua salama, atakabiliana na changamoto nyingine ya ndoa. Si wanaume wengi wanaweza kuwa tayari kuanza maisha na mwanamke mwenye mtoto tayari. Katika mazingira kama haya, ni wazi mzazi huyu ataishia kuwa maskini wa kweli kweli atakayelea mtoto fukara kuliko yeye. Kosa kubwa la binti huyu ni kukosa elimu ya afya ya uzazi ambayo ingemwezesha kukabiliana na shinikizo la kushiriki mapenzi kabla ya wakati wake.
 
NAFASI KWA WOTE,ndio my motto,lol

au hujaiskia kauli ya mkulu wewe kwa kebehi kasema 'hawezi kusomesha wazazi' au hukuielewa hii sentensi???

kuna hasara kuwaelimisha watu ama wazazi in this regard?,

embu zitaje hizo hasara,

kuna ubaya gani kukuta shule nzima ni wazazi?
Duuuh kama nabishana na wenye comment kama hizi niishie tu
 
CCM HAWALIONI JANGA HILI?

Magufuli--300x200.jpg

Rais Dkt. John Magufuli

Na Balinagwe Mwambungu,
Mtanzania

NCHI yetu inaonekana katika uso wa kimataifa kuwa na waoga na wanafiki, tunatumia vibaya rasilimali fedha zinazotolewa na wadau wa maendeleo ya nchi yetu.

Tamko la Rais John Magufuli la kutowasomesha watoto wanaopata ujauzito wakiwa bado wanasoma, limewaacha midomo wazi wadau wa elimu wa ndani na nje ya nchi.

Tangu tupate uhuru, nchi kadhaa duniani—hasa za Scandinavia—Sweden, Norway na Denmark, zimemwaga fedha nyingi za walipakodi wao kwa ajili ya kuinua sekta ya elimu. Mfano wa kudumu ni uwepo wa Shirika la Elimu Kibaha. Aidha, kuna shule mbalimbali za sekondari zilizojengwa kwa msaada wa nchi hizo—mfano ni Shule ya Sekondari Bagamoyo. Nchi hizo zimegharimia upanuzi na ukarabati wa shule mbalimbali, hasa wakati wa utawala wa Rais Mwalimu Julius Nyerere.

Si hivyo tu, nchi hizo zimesaidia kuendesha miradi ya elimu kwa watoto waliokosa kwenda shule kwa sababu mbalimbali, zikiwamo mimba za utotoni na zisizotarajiwa kwa wanafunzi wa kike walio sekondari.

Rais Magufuli amesema wakati wa utawala wake, watoto wa kike wanaopata ujauzito wakiwa shuleni, hawataweza kuendelea na masomo tena.

Hakuna kiongozi yeyote—kuanzia mawaziri wa elimu, afya na ustawi wa jamii—wanaoogopa kumweleza Rais Magufuli ukweli kwamba elimu ndio msingi wa maendeleo na hatutaweza kuendelea na kufikia nchi ya uchumi wa kati, kama sehemu ya jamii yetu imeachwa nje ya mfumo wa elimu na kwamba wizara zao tayari zilikuwa zinatekeleza programu iliyowalenga watoto wa kike—walioshindwa kuendelea na masomo sababu ya kupata ujauzito.

Tanzania ni kati ya nchi zinazoendelea ambazo zimesifiwa katika anga za kimataifa kuhusiana na hatua yake ya kumwelimisha mtoto wa kike na utekelezaji wa haki ya mtoto kupata elimu. Sijui wadau ambao wamekuwa bega kwa bega na nchi yetu katika kuendelea na kuboresha elimu kwa ujumla!

Inashangaza jinsi jamii ya Kitanzania ilivyobadilika ghafla na kuwa kama kondoo (ambaye hata anapopelekwa kuchinjwa, hunyaa tu). Hivi viongozi wenye dhamana ya elimu, afya na ustawi wa jamii hawana uthubutu wa kumwambia Rais kwamba tamko lake ni pigo kubwa kwao—kwa kuwa wamekuwa wakitekeleza mipango mbalimbali kuhusiana na mimba za utotoni na namna ya kumnasua mtoto wa kike aliyepata ujauzito akiwa shuleni.

Afya na Uzazi wa Mpango na ajenda ya kupunguza mimba za utotoni. Katika programu hii wabunge walipewa majukumu, pamoja na mambo mengine, kuhakikisha kuwa wanawahamasisha watoto wa kike kuendelea na masomo pindi wanapopata ujauzito.

Serikali za mitaa, mashirika ya kiraia na makundi mengine, yalikubali kutekeleza mpango huu. Wizara ya Elimu ilikuwa na programu ya MEMKWA na MMEM, zote zikiwalenga zaidi watoto wa kike waliokuwa nje ya utaratibu wa shule. ‘Mabinti Tushike Hatamu’ ni mradi uliokuwa unaendeshwa na Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), wilayani Temeke, Dar es Salaam, kwa kushirikiana na UNICEF.

Chukua hili kwa mfano, kwamba mtoto wa kike akipata ujauzito, asirudi shuleni baada ya kujifungua—kwa maelezo kwamba watoto wa kike wataona kuwa ni jambo la kawaida na wataendelea kufanya ngono zembe bila kujali kuwa kuna uwezekano wa kupata mimba.

Rais Magufuli alishangiliwa aliposema wakati wa uongozi wake, hakuna mwanafunzi atakayeruhusiwa kurejea shuleni baada ya kujifungua. Bila shaka, hili ni kama bomu kwa Mama Salma Kikwete (Mbunge), ambaye kwa mwongo mmoja, kupitia taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), amekuwa anampigania sana mtoto wa kike.

Chakushangaza zaidi ni pale viongozi wa Umoja wa Wanawake (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi, kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Amina Makilagi, anaunga mkono kauli hiyo. (Majira Julai 5, 2017). Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, alinukuliwa Aprili mwaka huu, akisema watoto wa kike warudi shuleni baada ya kujifungua.

“Tunapowakataza watoto wa kike wasiendelee na masomo pindi wanapopata ujauzito wakiwa shuleni, tunawaadhibu watoto wa masikini washindwe kutimiza malengo yao ya wakati waliotarajiwa,” alisema.

Aidha, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, Februari, 2016, alitoa mwongozo wa namna ya kumruhusu mwanafunzi wa kike kurejea shuleni baada ya kujifugua. Lakini yote haya inaelekea yamefutwa kwa kauli ya Rais Magufuli.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Unicef, Unesco, Shirika la Afya (WHO), Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya Watu (UNFPA) na Shirika la Chakula Duniani (WFP), yamekuwa yakifanya kazi na Serikali ya Tanzania kutokana na azma yake thabiti ya kutoa huduma, elimu na mafunzo mbalimbali kwa watoto na vijana.

Hii inatokana na ukweli kwamba, hata kabla ya Tanzania kuridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa kuhusu elimu, ilikwishaingiza kwenye Katiba yake na kutamka kwamba binadamu wote ni sawa, ikapiga marufuku ubaguzi wa aina yoyote, na ikaridhia Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto. Mwaka 2009, Bunge likatunga Sheria ya Mtoto ambayo inasema kuwa ni haki ya mtoto kupata elimu bila ubaguzi, ikiwa ni pamoja na wanafunzi wenye ujauzito.

Leo hii kwa tamko tu, mtoto wa kike atakayepata mimba akiwa shuleni, atakuwa amekatishwa ndoto ya ‘kuwa anachotaka’. Wabunge, hasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambacho kimekuwa madarakani kwa miongo minne, chama ambacho kiliasisi Elimu kwa Wote (UPE), kimekaa kimya! Vijana wa chama hicho—ambao suala hili linawagusa wao moja kwa moja, wamekaa kimya, badala yake wanaandama viongozi wa vyama vingine ambao wanaikosoa Serikali kwamba inatakiwa kutenda haki kwa wananchi wake wote—wadogo kwa wakubwa. Kama vijana wa CCM hawalioni hili kama ni janga la kijamii, basi wanaugua uzezeta.

Katika mwaka 2015, ambao ndio mwaka wa Uchaguzi Mkuu uliomwingiza Dk. John Magufuli madarakani, watoto wa kike 1,271 kutoka mikoa ya Mbeya (322), Morogoro (260), Mwanza (258), Kilimanjaro (235) na Dodoma (196), walikatishwa masomo kutokana na kupata ujauzito. Je, kwa nchi nzima itakuwaje—maana kama Taifa, hatujapata mwarobaini wake.

Taarifa ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, inaonyesha kuwa wasichana kati ya umri wa miaka 15 hadi 20 (umri ambao wanatakiwa wawe shuleni), wanaachishwa masomo kwa sababu ya ujauzito.

Taarifa hiyo inasema idadi ya wasichana wanaopata mimba imepanda kutoka asilima 10, mwaka 2010 na kufikia asilimia 27, mwaka 2015/16.

Hata kwa mtazamo wa juu juu tu, hali hii inatishia si tu kuongezeka kwa umasikini, bali pia kuvuruga mipango ya Serikali kwa sababu ya kuwapo duniani watoto ambao hawakuwa katika mipango ya nchi.

Serikali inapigana na umasikini kupitia Mfuko wa Kusaidia Kaya Masikini (TASAF), na mipango mingine ya kupambana na umasikini—huku kukiwa na ongezeko la watoto wasiotarajiwa. Hii ni sawa na kuchota maji na kujaza kwenye ndoo iliyotoboka chini.

Matokeo yake ni wazi—ndoo hiyo kamwe haitajaa. Mipango ya uchumi na kijamii, haitaweza kufaulu. Kutakuwa na midomo mingi ya kulisha, ongezeko la ombaomba, ‘dada poa’ mijini, na watoto wa mitaani, makundi ambayo Jeshi la Polisi linasumbuka nayo kila uchao! Matatizo haya yanatakiwa kutibiwa kwenye vyanzo vyake—si kwenye matokeo.

Vijana wa CCM wanatakiwa kujiongeza. Waache kugombana na wanasiasa ambao hawatakuwapo miaka 50 ijayo, watafute ufumbuzi wa masuala yanayowahusu vijana, hili likiwa mojawapo.

Elimu ni ufunguo wa maisha. Mnyime mtoto elimu, utakuwa umemfungia mlango wa maendeleo. Tunataka Tanzania ya viwanda, ni lazima wawepo watu—hasa vijana, ambao ndio nguvu kazi ya taifa—vijana waliojizatiti katika fani mbalimbali na watakaoweza kulisukuma gurudumu la maendeleo. Asiwepo atakayeachwa nyuma na boti ya elimu. Usiwepo ubaguzi—kuwabagua waliokoseshwa elimu (sio kwa mapenzi yao).

Kama mtoto wa kike hatapewa nafasi maalumu, basi malengo ya Elimu Bure, hayatafanikiwa.
 
Marais wengine hata bila kushauriwa walikuwa wanasoma na kuchambua mambo mbali mbali ya kimaendeleo na kijamii pamoja na sheria za kimataifa. Huyu amebakia kucrame tu kikasuku mambo yasiyo na maana, akiacha uelewa wa mambo ya kimsingi na kujifanya kuyatolea matamko ya kishamba!!
 
Suluhisho ni wanao watetea wasichana na mimba zao wajenge shule zenye wodi, na chekechea kwa watoto watakao zaliwa.

Vile vile hao wanao watetea wasichana wenye mimba hawaoni the social impact upande wa pili.
Mimba kwa watoto wadogo imekuwa legislated kuwa ni a social crime, punishable by jail time.

Sasa ukiruhusu watoto wenye mimba waone suala hili linakubalika, inabidi mtu apimwe akili.

This is a primitive argument !!

I thought, kabla hujatoa hitimisho la namna hii, ungeenda mbele na kurudi nyuma na ujiulize ni kwa nini mabinti (hata wako aweza jikuta ameingia shida hii) hupata mimba wakiwa shule ama ktk umri mdogo wa kupaswa kuwa shuleni ?

Na usiishie hapo, jiulize zaidi na zaidi, kwamba, nini jukumu la wazazi, jamii na serikali kwa ujumla ktk kuzuia hili ? Wanatekeleza wajibu wao au ndiyo kina ninyi hawa wenye majibu rahisi ktk mambo ambayo unapaswa kukuna bongo ?

Yaani, ndugu Jidu La Mambambasi akili na ufahamu wako hauna tofauti na mwenye chanzo cha kauli hii ambayo ndiyo msingi wa mjadala huu.... ndugu yako Rais J. P. Magufuli !!

Mimi nadhani tukubali tu, kuwa, Mr. President alichemka kwani wakati mwingine ukimya ni busara zaidi kuliko kupayuka hovyo bila kuwa na uhakika unachopayukia...

Sasa ona anavyokuwa exposéd....pure ignorance !!

Na sina hakika kama anatambua hata sheria za ndani ya nchi yake mwenyewe na zile za kimataifa ambazo sisi kama taifa tumeziridhia, zinasemaje kuhusu jambo hili !! ....Na ninyi ignorantly, mnaunga tela kwa nyuma eti kwa sbb Rais kasema !!

Ni yaleyale kama ya Makinikia na ishu ile ya wanafunzi wa UDOM ambao sijui ilikuwa kwa kutojua ama kwa makusudi aliishia kutukana watu wake kwa kuwaita "vilaza" kitu ambacho hata angekutumia lugha ya kawaida tu, angeeleweka na kile akitakacho kikafanyika...!!!
 
Sheria ipi ya mwaka gani?......nacho jua kuna sheria inakataza wajawazito kurudi shuleni nipe muda nikupekulie kwenye makabrasha, ila kinachonishangaza ni kwamba rais ame kazia tu ila tangu awali hatujawahi kuwa na darasa lililochangamana na waja wazito.....naomba sheria iliyopindishwa na mimi nikuletee sheria inayopiga marufuku waja wazito kuendelea na masomo kwenye shule za SERIKALI.

Hakuna sheria kuu kuliko katiba ya nchi mkubwa !!

By the way, naamini unatafuta waraka wa elimu No. 6 wa 1978 labda na sheria za shule kuwa "kosa linaloweza kumfukuzisha mwanafunzi shule, ni pamoja na..... 'kupata ama kusababisha' ujauzito !! "
 
Mkuu BAK, asante kwa uzi huu, na kwa ruhusa yako, naomba kuutumia kurutubisha bandiko langu kutoa Wito kwa Waziri wa Habari, Dr. Harrison Mwakyembe, awatimue nchini kwetu raia wote wa kigeni ambao kutwa kuchwa wanamsema vibaya rais wetu mpendwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli.

Hili gazeti la The East African lilishapigwa marufuku kusambazwa Tanzania siku nyingi kutokana na kumsema vibaya Kikwete na kumchora kwenye vikatuni, sasa limemkomalia rais Magufuli kila kukicha from time likimsema vibaya na kumchora katuni za kumdhalilisha, hivyo namshauri Waziri Mwakyembe atafute zile devices za ku block online contents kama wafanyavyo China ili tuliblock kabisa hili gazeti lisisomwe Tanzania.

Watu pekee wenye uhalali wa kumsema vibaya rais Magufuli ni sisi Watanzania wenyewe ambao ndio tulimchagua rais Magufuli kuwa rais wetu. Ilitokea sisi haturidhishwi na utendaji wake, ndio wenye haki hiyo ya kumsema vibaya kwa sababu sisi ndio waajiri wake!, na media zenye haki hiyo ni media zetu na sio media za jirani au media za nje.

Kama sisi wenyewe tunampenda rais wetu na kumkubali sana, kwa nini tusiwatimue nchini kote raia wote wa kigeni walio nchini ambao wanamsema vibaya rais wetu?.

Paskali
Sema unampenda na sio tunampenda

spend less, save more
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kilichoandikwa ni kweli tupu na hata Watanzania wengi wameyasema yote haya yaliyoandikwa humu. Kama dikteta uchwara anapindisha sheria za nchi na za kimataifa ambazo Tanzania imesaini lazima aambiwe ukweli. Kufukuza wanaomwambia ukweli dikteta uchwara si solution ya kuwanyamazisha hawa hata wakiwa nje bado wanaweza kumpa ukweli wake.
Sijui anapata wapi ujasiri wakukaa juu ya Sheria,

spend less, save more
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Sheria ipi ya mwaka gani?......nacho jua kuna sheria inakataza wajawazito kurudi shuleni nipe muda nikupekulie kwenye makabrasha, ila kinachonishangaza ni kwamba rais ame kazia tu ila tangu awali hatujawahi kuwa na darasa lililochangamana na waja wazito.....naomba sheria iliyopindishwa na mimi nikuletee sheria inayopiga marufuku waja wazito kuendelea na masomo kwenye shule za SERIKALI.
Kunatofauti kati ya wajawazito na waliozaa mashulen

spend less, save more
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Anataka matamko yake yawe sheria za nchi wakati yeye si mtunga sheria nchini. Madikteta uchwara ndivyo walivyo Mkuu.
Time will tell, nawachukia hasa wanaojifanya wanamkubali halafu wakija mtaani wanaungana nasi

spend less, save more
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Banning pregnant girls from school is against the laws of Tanzania
Tuesday July 4 2017

magufoolie.jpg

President Magufuli’s remarks indicating his intention to stop girls from going to school is in contradiction of the laws and policies of his own country and his government’s failure to fulfil its obligation to protect and safeguard the rights of its citizens, especially the rights of its vulnerable citizens. ILLUSTRATION | JOHN NYANGA

THE EAST AFRICAN

In Summary
  • In addition to the Beijing Declaration and Platform for Action, the right to education as a basic right is enshrined in several international and regional conventions and protocols

By DINAH MUSINDARWEZO

More by this Author
Only a few days after the celebration of the Day of the African Child, the President of the Republic of Tanzania, John Magufuli, victimised teen mothers by swearing that during his presidency they would not be allowed to go back to school.

The president’s remarks were disheartening and a setback for the hard-fought gains on women and girls rights, gender equality and empowerment of women and girls achieved by women’s movements including the work done by African Women’s Development and Communication Network (Femnet) members in Tanzania.

Education as a basic right

The women’s movement across Africa and globally has fought hard to guarantee girls the right to quality education.

At the Beijing International Conference on Women 31 years ago, African women championed the rights of the girl child and as a result, one of the 12 Beijing Areas of Action focused on the girl child.

In addition to the Beijing Declaration and Platform for Action, the right to education as a basic right is enshrined in several international and regional conventions and protocols including the Convention on Ending Discrimination against Women (Cedaw).

The Convention on the Rights of the Child, the African Protocol on the Rights of the Child, the African Charter on the Rights of Women in Africa (Maputo Protocol) and Goal 4 of the UN’s Sustainable Development Goals, that all focus on inclusive and equitable education for all.

All these conventions and protocols focus on the right of boys and girls to access quality and equitable education and put obligations on the States that have ratified them to protect, fulfil and uphold this human right.

A particular focus is put on girls’ education due to their vulnerabilities as a result of structural and systematic gender inequalities.

Unwanted and early pregnancies are a manifestation of such inequalities and an indication of girls’ vulnerabilities where often the blame is put on pregnant girls instead of those who made them pregnant or those who failed to put mechanisms in place to prevent unwanted pregnancies.

The Republic of Tanzania is a party to the above conventions and protocols and to some extent the government has taken steps towards implementing them.

Education Act

For example, the country has an Education Act and a Child Act, both of which aim to protect and safeguard the rights of each child including protecting them from discrimination and providing the right to services.

President Magufuli’s remarks indicating his intention to stop girls from going to school is in contradiction of the laws and policies of his own country and his government’s failure to fulfil its obligation to protect and safeguard the rights of its citizens, especially the rights of its vulnerable citizens.

His contractions are further exposed by the government of Tanzania’s guidelines on how to enable pregnant schoolgirls to return to school and resume their classes, which were adopted by his government in 2016.

These guidelines affirm the government’s commitment to reduce the high number of school dropouts caused by various factors including pregnancies among schoolgirls.

Some 4.4 per cent of girls enrolled in both primary and secondary schools dropped out due to pregnancy, according to Basic Education Statistics in Tanzania in 2014.

While Magufuli takes away the right of teen mothers to choose the type of education they want when he says in his address that teen mothers should go in for vocational training, sewing or farming, the above mentioned guidelines clearly state that the state’s goal is to provide an enabling environment for all pregnant girls to resume schooling after delivery to complete their education cycle.

Magufuli’s remarks could push girls into child labour and reinforce gender stereotypes leading to gender-segregated jobs. This goes against the African Union’s efforts to increase the number of girls in science, technology, engineering and mathematics.

When he took up the presidency, Magufuli was adamant about fighting corruption to ensure equitable development. That was before his homophobic and sexist remarks started.

What he should know is that it’s impossible to achieve development without achieving gender equality as various researches have shown.

When girls are denied the opportunity to education, it limits their access to other opportunities including decent employment, leadership and access to information and to make informed choices. Girls who drop out of schools are also likely to end up in child marriages.

Africa’s women and girls are extremely irked by President Magufuli’s utterances. He was “the president to watch” for mostly the right reasons until now. Still, President Magufuli can do the following to redeem himself from this recent retrogressive outburst:

• Retract his remarks and immediately apologise to Tanzanian women and girls

• Provide child care facilities for all teen mothers to allow them to go back to school without worrying about who will take care of their babies;

• Address stigma and discrimination towards teen mothers in schools, homes, community;

• Educate himself on the rights of girls and women and his obligation as the head of state to fulfil them;

• Ensure provision of comprehensive sexuality education as a preventive measure;

• Provide youth-friendly reproductive and sexual health services;

• Hold those who make girls pregnant accountable;

• Implement national, regional and international policies, laws and conventions/protocols on girls’ education, gender equality and women’s rights; and
• Allocate adequate national budget towards addressing gender inequalities.

We at Femnet in collaboration with our members in Tanzania and across the continent are committed to supporting President Magufuli and his government to achieve the above.

Dinah Musindarwezo is the executive director of the African Women’s Development and Communications Network, Femnet.
These are lesbian activists singing imported ideologies from the decandent West. Next time they will ask Magufuli to provide marriage parlours for lesbians and homosexuals. Go away please. You are not wanted in our country. Use the money you have to give a bible to each pregnant girl, then build schoolf for them.

Sent from my SM-G935F using JamiiForums mobile app
 
Haki ya mtoto wa kike kupata elimu ni ya kikatiba kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Baada ya Magu kusema kuwa wakati wa awamu yake ya kuliongoza Taifa hataruhusu binti yeyote aliye shule ya msingi au sekondari aliyepata mimba kuendelea na shule, inashangaza hata baadhi ya mawaziri ambao kabla ya kauli hiyo walikuwa wakisema kuwa policy ya Tanzania ni kila mtoto wa kike aliyepata mimba baada ya kujifungua waendelee na masomo yao. Baada ya kauli ya Magu nao wameamua kuufyata!

Sasa inapotokea mtu kama Halima Mdee kutamka kuwa kauli yake Magufuli anaiona kama ndiyo sheria, mtu kama DC wa Kinondoni anachachamaa na kuamuru kukamatwa kwa Halima Mdee!

Huyo DC wa Kinondoni atakuwa tu anatetea kibarua chake kwa kuwa anajua alichokisema Halima Mdee ni ukweli mtupu kuwa yeye JPM anachukulia kauli yake kuwa ndiyo sheria!
Halima Mdee alizaa shuleni? 2azazi wake si wapo mpaka leo walimtunza vizuri na serkali ya CCM ikamsomesha? Kwa nini yeye anataka iwe tafauti, kwani wazazi wake walipompa maadili walikuwa wajinga?

Sent from my SM-G935F using JamiiForums mobile app
 
Sijui anapata wapi ujasiri wakukaa juu ya Sheria,

spend less, save more
Rais ana madaraka jamani. Kule Marekani huitwa EO yaani executive orders. Rais Obama alipitisha EO kuruhusu ndoa zajinsia moja. Akapitisha EO ingine kuwasamehe wahamiaji haramu wasishitakiwe kwa vile hupigia kura democrat. Rais Trump alitoa EO kuzuia wahamiaji kutoka nchi za magaidi. Rais Nyere alitoa EO tuhamie mji mkuu Dodoma.

Sent from my SM-G935F using JamiiForums mobile app
 
Rais wa Tanzania anatoa EO lakini iko applicable Tanganyika tu lakini kule Zanzibar haitambuliki! Hii katiba ya nchi ina walakini mkubwa sana. Na hiyo EO ni ya kuwakandamiza wasichana na kuwadhulumu haki yao ya kupata elimu kama watoto wengine kwa kosa ambalo hawakujua madhara yake au kubakwa na stranger au family member.

Back
Top Bottom