Banki ya Zanzibar (PBZ) hivi mpo serious Tanzania bara?

nyiokunda

JF-Expert Member
Jun 16, 2015
1,620
826
Benki ya watu wa zanzibar mmengia kutoa mikopo kwa wafanyakazi hasa jwtz.Nilicho kishangaa ndugu yangu yupo arusha aliniambia nimchukulie loan form mwz wa kwanza ,wakaniambia hamna mpaka mwz wa pili. Sasa ndg yangu ame apply tangu mwz wa pili had leo haijatoka na hamna maelezo tosheleza. Alipoulizia wenzake eti imewachukua zaid ya miez miwili kupata.kwanza nilichokiona hata customer care ni zero.

Sasa badilikeni ushindani ni mkubwa na wateja ni walewale otherwise kama mme focus wanzibar waliopo bara ok
 
Hizo hela za kukopesha wanajeshi tu?
Benki nyingi zinakopesha kwa kubagua watumishi wa umma,wenye mishahara midogo wanapewa mikopo yenye riba kubwa,wanajeshi na wakuu wa idara wwnye mishahara mikubwa,wanapewa mikopo yenye riba ndogo!JPM atumbue na huku
 
Hizo hela za kukopesha wanajeshi tu?
Benki nyingi zinakopesha kwa kubagua watumishi wa umma,wenye mishahara midogo wanapewa mikopo yenye riba kubwa,wanajeshi na wakuu wa idara wwnye mishahara mikubwa,wanapewa mikopo yenye riba ndogo!JPM atumbue na huku

Kabla benki yoyote haijaanza kukuposha wafanyakazi wa Taasisi fulani huwa wanasaini mkataba na taasisi hiyo. Mkataba huo una vipengele muhimu vinavyohusu taasisi kama guarantor wa mkopo huo.Majukumu ya Taasisi ni kuhakikisha mshahara wa mfanyakazi unalipwa kwenye akaunti ya mfanyakazi iliyopo kwenye benki hiyo ili benki iweze kukata fedha zake kila mwezi. Pia Taasisi lazima iji- commit kwa maandishi na muhuri kama itatokea mfanyakazi ameshindwa kulipa mkopo huo aidha kwa makusudi, kuugua, kuachishwa kazi, - kampuni itatatumia mafao ya kustaafu ya mfanyakazi husika kulipa kiasi cha mkopo kilichosalia. Kama PBZ inawakopesha wanajeshi kwa sasa inawezekana hiyo ndiyo taasisi ambayo imeingia nayo mkataba. Kama unahitaji mkopo wao nenda kwao na zungumza na taasisi unayofanyia kazi ili wafuate taratibu
 
Kila mtu na zali. .kuna mwana namjua aliapply mkopo hapo faster alipata na wala hakupata complications za kipimbi kama alivyojaribu equity bank
 
Back
Top Bottom