Nchi haijawahi kuwa tajiri kwahiyo haiwezi kufilisika. Pia nchi haina uwezo wa kulipa madeni zaidi tunapunguza na wakiona tumewalipa na riba kiasi fulani wanasamehe. Ila wakikopa kwenye capital markets shughuli yake wataijua. Ingawa miaka ya sasa hivi wanaweza wasielewe, kiongozi atakayefuata ndiyo atajua joto lake.Ifilisike mara ngapi tena!? Rasilimali zetu tunazigawa bure kwa "Wachukuaji" ambao tumeamua kuwaita "Wawekezaji" kumbe hakuna chochote wanachowekeza bali ni WIZI MTUPU! Tulipunguziwa madeni kwa kiasi kubwa sana wakati wa awamu ya Mkapa sasa hii awamu ya Kikwete madeni hayo yamerudi tena kwa kiasi kikubwa. Wanaona kabisa nchi haina mapato ya kuweza kujiendesha badala ya kutafuta namna ya kubana matumizi ili kupunguza budget tegemezi sasa wameamua kuanza kukopa mikopo yenye riba kubwa sana ambayo nchi haiwezi kuimudu. Tuna vichwa vya wendawazimu ambao hawaangalii mbali na kama wasiposikia onyo la WB katika mkopo huu mkubwa wanaotaka kuchukua basi itafika wakati hata kukopa itakuwa haiwezekani tena maana nchi itakuwa imezidiwa na madeni makubwa mno.