Bank ya Equity kupata mkopo wao inachukua hadi miezi 2

wakikosi

JF-Expert Member
Feb 28, 2015
1,354
1,483
Habari za asubuhi waungwana,hii Bank ya Equity branch ya Mbagala huduma zao za kukopesha hela ni slow sana.

Yaani hawajui kuwa mtu akienda kwao kukopa ni kuwa ana matatizo na ana uharaka wa kupata pesa ili amalize shida zake.

Lakini kupata mkopo Equity Bank sana sana tawi la Mbagala ni long process aise,yaani tena mtu ni mtumishi wa serikali unakatwa kwenye mshahara wako wao wajibu wao ni kukupa mkopo wao na wao wakate pesa zao serikali huko lakini usumbufu wao hao Equity sio wa kitoto.

Sasa sijui inakuaje mtu mwezi hawampi mkopo wake? Yaani ni usumbufu tu,kama hawawezi kukopesha pesa watu bhas watoe tangazo kuwa "hawakopeshi"

Sisi tukija kwenu kukopa hela maana yake tuna matatizo na uharaka wa pesa,sasa sio muwe mnatuzungusha kupata mkopo namna hiyo.
 
Ni hatari sana kupewa mkopo ikiwa huna kitu kabisa.
Sasa hakuna uhatari wowote,maana kama kuna matatizo na makato yao watamalizana kwenye mishahara yetu huko.

Sisi watumishi wa umma tunakopesheka tu hatuna vikwazo,kikwazo ni kwao kuchelewa sana kutoa hela
 
Umewahi kukopa tena kwa dhamana hiyo ya utumishi?
 
Habari za asubuhi waungwana,hii Bank ya Equity branch ya Mbagala huduma zao za kukopesha hela ni slow sana.

Yaani hawajui kuwa mtu akienda kwao kukopa ni kuwa ana matatizo na ana uharaka wa kupata pesa ili amalize shida zake.

Lakini kupata mkopo Equity Bank sana sana tawi la Mbagala ni long process aise,yaani tena mtu ni mtumishi wa serikali unakatwa kwenye mshahara wako wao wajibu wao ni kukupa mkopo wao na wao wakate pesa zao serikali huko lakini usumbufu wao hao Equity sio wa kitoto.

Sasa sijui inakuaje mtu mwezi hawampi mkopo wake? Yaani ni usumbufu tu,kama hawawezi kukopesha pesa watu bhas watoe tangazo kuwa "hawakopeshi"

Sisi tukija kwenu kukopa hela maana yake tuna matatizo na uharaka wa pesa,sasa sio muwe mnatuzungusha kupata mkopo namna hiyo.
Njoo standard chartered mpaka 150m ndani ya 24hrs 48hrs.na mikopo mingine inanunuliwa
 
Back
Top Bottom