Bank M Kukusanya Kodi kwa niaba ya TRA - Wao wanapata nini?

Nyie watu mnatatizo la paranoia. Mkienda TRA mnalalamika mistari mirefu mkiraisishiwa mnaogopa. Chamsingi ni kuhakikisha hakuna michezo michafu lakini kiujumla hii ni service nzuri..
 
Kufanya uzinduzi ni mojawapo ya mbinu zinazotumiwa katika kujitangaza, hivyo hao jamaa wako kibiashara zaidi na mbinu za promotion wanazifahamu. Sasa ukifanya kimya kimya nani atakufahamu?

Kwa hiyo hakuna tatizo hapo!!

Hapana...uzinduzi hufanyika katika mazingira ya ushindani zaidi...kwa vile unalenga kujiweka mbele ya washindani wako...ni tatizo TRA kutumika katika ushindani wa kibenki
 
Naomba unisaidie; kuwa Bank M haitakusanya kodi kwa niaba ya TRA katika makubaliano ya aina yake? maana najua kuna utaratibu wa kawaida wa kukusanya kodi katika PoS na wachuuzi mbalimbali hukusanya kodi na wanatakiwa kuremit kwa TRA. Hili si jambo geni. Ila hili la Bank M ndio nataka kujua lina tofauti gani na hivi vingine? Nilivyoelewa mimi ni kuwa mtu akitaka kulipia ushuru au kodi fulani anaweza kwenda kwenye tawi la Bank M na kufanya malipo hayo kwendaa TRA, Bank M wanatumia miundo mbinu yao kuwasilisha fedha hizo TRA ndani ya dakika tano.

Hivi ndivyo au sivyo?
wewe kama kampuni ukishakusanya kodi (ie vat) kwenye POS zile hela zinaingia kwenye account yako na wewe unapewa 30days kuwa umeshalipa tra, kila mwisho wa mwezi unatakiwa kupeleka vat za mwezi uliopita. tra na wao kama kampuni lazima wawe na account kwa ajili ya kuweka fedha zao na account hizo ziko kwenye mabenki mbali mbali. Hata ukipeleka hela tra moja kwa moja bado tra watazipeleka hizo hela kwenye account zao zilizo kwenye bank mbali mbali. nimeshalipa vat kwenye bank ya exim najua pia crdb pia wana hii huduma. tofauti kati ya bank m na bank hizi zingine ni kujitangaza kwao. kitu kidogo lazima wao wana make a meal.

na pia hela ikiwa kubwa lazima utumie bank kuu kulipa.
hao wateja wameongea ili kuipa sifa bank m lakini karibuni kila bank ina hii huduma nothing special about what they are offering.

mteja wa bank m ataondokana na usumbufu kutoa hela zake kutoka bank mna kwenda kulipa kodi sehemu zingine.
pia wafanyabiashara wanapenda kulipa kodi siku ya mwisho kwa ajili wanazungushia zile hela kwa hiyo kama wao wataweza kulipa siku ya mwisho bila delay itawasaidia wasipigwe penalty maana yake ukichelewa kulipa kodi ni penalty.

kwa upande wa bank m wao wata keep their coustomers happy na pia kuwa na mteja wa hela nyingi kama tra ndio kitu ambacho kinawafanya bank waishi

kwa upande wa tra wao wana reduce operational cost..
 
Back
Top Bottom