Bank gani Tanzania inatoa Online Services nzuri? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bank gani Tanzania inatoa Online Services nzuri?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Consultant, Sep 16, 2010.

 1. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,804
  Likes Received: 6,314
  Trophy Points: 280
  Wakuu, msaada tafadhari!

  Ninatafuta Bank inayotoa huduma zifuatazo:

  1. Online services - kuangalia salio, kuweza kufanya transfer ya pesa kwa mtu mwenye akaunti etc

  2. VISA/Master Cards

  3. Huduma ya kufanya shopping online (amazon et la)

  4. Uwezo wa kumtumia pesa (online) mtu mwenye account na bank nyingine

  Mwenye uzoefu naomba anisaidie
   
 2. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2010
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  hakuna sababu ya wizi mkuu,walikuwa CRDB wakaona wanapata hasara wakasitisha labda uende kuna form maaalum ujaze hiyo inasema ukiibiwa ni juu yako.ndo bongo ya thithiem u
   
 3. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,804
  Likes Received: 6,314
  Trophy Points: 280
  Ninachojua kwa CRDB, online service yao ni kuangalia salio, kuangalia mlolongo mzima wa fedha yako ilivyotoka na kuingia na vile vile kufanya online transfer kwa mtu mwenye account na CRDB tu.

  Ukijaza hiyo form unayosema, unaweza kupata zile huduma zooote as specified kwenye post?
   
 4. C

  Chief JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2010
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Nafikiri CRDB wana huduma bora zaidi. Kwanza unaweza kupewa huduma ya online ya ku-access account yako popote ulipo, baada ya kujaza fomu fulani. Ukiwa Online, unaweza kufanya malipo mbalimbali, pamoja na ku-transfer fedha kwa mtu mwingine mwenye akaunti ya CRDB. Vile vile, unaweza ku-print bank statement yako kwa kipindi chochote unachotaka. Hivyo si kuangalia salio tu. Nilijaribu kuomba huduma hii Standard Chartered, wakasema wanatoa kwa Corporate customers only.

  Huduma zingine ni kuwa unaweza kutumia card yao (VISA) kufanya online shopping eg from Amazon, kununua software online, kufanya bookings za hotel unaposafiri nje ya nchi, kununua tiketi za ndege (cheaper kuliko kutumia travel agencies), kutumia kwenye shopping malls ukiwa nje ya nchi, n.k. Unaweza vile vile "kuiunganisha" kadi yao na PayPal na hivyo kutumia Paypal kwa malipo.

  Natumaini nimekusaidia kwa jibu hili
   
 5. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Usijaribu NBC. Unaweza kumaliza mwaka tangu kuijaza fomu kabla hujaweza kuitumia huduma hiyo.
   
 6. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,804
  Likes Received: 6,314
  Trophy Points: 280

  Hapa naona poa. Ubarikiwe
   
 7. M

  Mchapakazi Member

  #7
  Sep 18, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 67
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CRDB inaconnect na paypal? Mbona niliona Mkenya fulani akijisifu kuwa paypal imeingia Kenya na kuwa ipo Ke na South Africa peke yake?
  Kuna mtu ameshaunganisha Tembo card yake ba Paypal?
  Naomba kujuzwa
   
 8. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #8
  Sep 18, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,427
  Likes Received: 22,346
  Trophy Points: 280
  Hili swali lako kaulize nchi nyingine, hapa bongo ni wizi mtupu
   
 9. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #9
  Sep 21, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  wengine wanasema standard chattered, mimi sijui. crdb ni wezi tu. wameweka vile vibandiko vyao kuwa kwenye AtM zao wanatoa hela kwa mastercard, nimejaribu karibia mara tati haitoi, inatoa kwa wale wa bank za hapa nchini tu. however nilishawai kutoa hela mara mbili, lakini siku hizi naona sijui wanaona wanapata hasara gani...wale wenye account baclays naomba kujua kama nayo iko hivyo.
   
 10. C

  Chief JF-Expert Member

  #10
  Sep 26, 2010
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Nimeshawahi ku-connect card yangu na PayPal.
  Huwezi kutumia ATM card ya Standard Chartered nje ya nchi. Nimejaribu si zaidi ya wiki moja iliyopita na haikufanya kazi. Bado huduma za CRDB kwa eneo hili ni nzuri kulinganisha na benki nyingine.
   
 11. DICTATOR

  DICTATOR JF-Expert Member

  #11
  Sep 26, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi niko ughaibuni, natumia CRDB. NBC hata usijaribu kabisaaaa maana hawajui kitu kinaitwa customer care.

  CRDB popote unaweza kutumia hakuna shaka mkuu.
  Nimekuwa nikiganya manunuzi kupitia mtandao kwa kutumia VISA card ya CRDB bila matatizo,

  Onyo! password ni siri yako kama unajua wezi wa mtandao you must be carefull with the website you use. Safe website inaanza na https................., kama ni fake huwa hazina 's'.

  Last yeah nilikuwa nchi moja huku maeneo ya Asia nikaishiwa nikawa natumia CRDB Visa card bila shida.

  last week tena nilikuwa mitaa ya huku Asia, nikatumia CRDB mkuu. Nenda kajaze form tawi ulilofungulia bank account yako, after 4 days wanaactivate uanze kula isha popote.

  Karibu sana.
   
 12. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #12
  Sep 26, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  thanks kwa kutujuza. Unafanya kazi crdb nini.
   
 13. Mziba

  Mziba JF-Expert Member

  #13
  Sep 26, 2010
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 226
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Biashara ya Benki naona kijiwe kimewachanganyia. wateja mpaka waanaingaka, hii ni neema kwa biashara za benk. Mtazamo wangu umetokana na hizi posti zote zilizonitangulia. Baada ya kusoma, nimepata mtazomo hii. Tafadhali nirekebishe kama niko mbali sana mtazamo wako.

  1. Banki zote Tanzania, simeridhika sio tu, na utendaji kazi wao, bali wenye kumiliki hizi biashara pia inawezekana, hawako informed.
  2. Bado kuna wego(uga) mkubwa wa biashara za benki. Ndio maana wananchi wanapokonywa na baadhi microfinance wizi. Unamkopeshaje mtu pesa bila kumfundisha namna ya kua mwangalifu kunako deni, na kumwambia gharama zote dhahiri?.

  On this JF, People know this. We are now a capitalist country but we are not using the tools that out farthers na mothers have given us. , Mzee Musa na Mzee Ruhsa and other Wazee, were involved in a Game Changers on that regard (really smart) we moved from socialist economy to capitalist economy model , The people who made change most of them are alive today. Yani wala sio aibu kua mkapitali. Based on this new system, it is quite probable we will surpass Kenya GDP in the near future. We are about to see a barrage of wealthy in Tanzania due to New Innovations, that are about to hit the markets. Even the MGDs on Poverty will will get closer to achieve its #2 goal. Remember, now we can do as many things in business compare same as Kenya used to do in the past. We (Tanzania) are good in a few things. For, instance, we are excellent in creating and retaining relationships. This is what were told and see our parents in action. And constantly "Utu wa mtu, si kitu. Sasa wazee walipochange sysytem, based on the circumstances around the country, there were no strategic plans to teach our communities to operate the in the new system of free enterprises (it's another way of saying capitalism). But, I think that our part JF. and other volunteers. The Govenment has a Sector of miundo mbinu/ujasimali to improve our livelihood in the Free Enterprises, but i do not know the number of wajarisimalis. But, I think there is room for improvement in which entrepreneurship may lead the economy and join hands with our big banks with a lousy services, help them get more customers, while getting good customer care. see a room for business to help the society. Guess what, in this age technological and globalization, building and maintaining relationships, is a money making machine. The most important is not to be too greedy. My friends in JF Building and retaining relationship is a weapon of choice when it comes to fight chronic poverty. We were raised to be nice people. Forget all these jargons, in the textbooks and business world. take this, Customer care, Customer Service, Customer Relation, and the big one, "Public Relations" . and the list goes on. And you know what, They all means same thing, Just listen attentively, to people they will tell you what they. want. Cheka nao uwajue tabia zao. Then, after you get to know them, you will know want they want before they even say it. This is the credo of customer care. Teach that if you can, you could make tons of Shilings, wateja zako, all Banks in tanzania including Not for Profit Banks.
   
 14. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2014
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,804
  Likes Received: 6,314
  Trophy Points: 280
  Wakuu, naomba kufahamishwa ni bank gani Tanzania inayotoa mastercards zilizopewa uwezo wa kufanya manunuzi online kwa mfamo amazon, e-bay na kwingine, bila longolongo?

  Nilijaribu kuomba huduma hiyo CRDB kitambo sana na sikupata majibu
   
 15. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2014
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,037
  Trophy Points: 280
  Ni CRDB mkuu.......nenda kawaone.......kuna fomu utajaza then card yako inawezeshwa........
   
 16. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #16
  Oct 5, 2014
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,804
  Likes Received: 6,314
  Trophy Points: 280
  Preta, nilijaza kitambo sana. Nilichopata ni ''internet banking'' service tu; ambapo naweza kufanya online transfer kwenda account ya CRDB. Hiyo service ya kufanya online purchase sikupata.
   
 17. lusungo

  lusungo JF-Expert Member

  #17
  Oct 5, 2014
  Joined: Jan 4, 2014
  Messages: 18,143
  Likes Received: 9,033
  Trophy Points: 280

  Nenda kawaone tena mbona mi nafanya kupitia hao hao CRDB??
   
 18. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #18
  Oct 5, 2014
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,037
  Trophy Points: 280
  Inawezekana kwa sababu mimi pia nafanya online purchasing na card yao hao hao na sijapata tatizo lolote.........
   
 19. djcondoro

  djcondoro Member

  #19
  Oct 5, 2014
  Joined: Aug 19, 2013
  Messages: 6
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Chukua ya Barclays, inafanya kila kitu na hiyo access ni automatically provided hakuna cha kujaza form uwezeshwe. Crdb wanacomplicate mambo sana na charge Yao utajutaa!
   
 20. m

  mshewa2 Member

  #20
  Oct 27, 2014
  Joined: Oct 30, 2012
  Messages: 75
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  BancABC wala huhitaji kuwa na account unajaza tu form kwa ajili ya visa card unapata card the same day unatakiwa tu kuwa na kitambulisho na elfu 5000
   
Loading...