Bank ipi ni bora for saving na makato yake ni nafuu

kwa tanzania haipo, nakushauri pesa zako wekeza kwenye miradi au ukishindwa chimbia ndani ya nyumba yako. benki zote bongo ni maumivu tu!
 
nataka kufungua saving account tanzania,je ni bank gani nzuri kwa huduma hii na michanganuo yake kwa mwenye uelewa na hili....

Mkuu kama wadau walivyotangulia kusema hapo juu benki zote za TZ kwa customer care bado sana ila kuna unafuu wa namna fulani katika baadhi ya mabenki. CRDB ni wazuri ila wana bank charges nyingi sana. Exim hawana bank charges nyingi almost ni bure kuweka pesa zako na kuchukua na pia wana MasterCard. Interest rate ya CRDB ni 2% na Exim ni 3 %. NBM na NBC ni wabovu zaidi.
 
Mbona hii imeka ki-promo promo??

Hata kama imekaa ki-promo promo ni sawa tu maana ukilinganisha benki zote CRDB kwa kweli wako juu mimi binafsi nimewakubali na nikajuta ni kwa nini sikufungua akaunti kwao mapema? Hapa kwetu ukienda benki hukai zaidi ya dk 30. Hebu jaribu benki ya makabwela ukione cha moto, mpaka unashangaa kama hao wafanyakazi wao wanafanya kazi kwa kulipwa au wanajitolea? Yaani ni kero tupu (morale ni zero). Siku zingine ukute msitari wenyewe umepiga kona kama tano hivi na kama mko karibu na barabara basi tegemea huo msitari kuukuta uko barabarani!

Ninakubaliana na aliyesema benki zetu zote ni maumivu tu, lakini hata kwa mbumbumbu kuna mjanja wao!! Basi bila ubishi CRDB ni miongoni mwa wajanja wao!
 
Benki ya kuweka ni ku-invest pesa zako ziwe ktk mzunguko. Fungua mradi wowote na utafaidika. Savings account nyingi hazina interest na makato ni makubwa sana. Ukipiga hesabu ya mwaka ndio utaona jinsi gani unaliwa pesa zako: mf. monthly charges, ATM charges, nk.

Ukifungua mradi pesa yako ni km umeiweka bank itakuwa inazunguka hapo hapo na faida utapata. Lakini usisahau kukata BIMA maana mradi ukiteketea utakuwa na hasara kubwa.
 
Mkuu benki zote za huku wapo sawa tu. Customer care ya kwenye bank ni mbovu sana. Mteja ukiingia wanakuona kama tatizo hivi. Hata huduma ukizipata ni nusu nusu tu. Ingawa kidogo sana wanabadilika.
My take, ukija huku, punguza pressure yazoee mazingira maana bp itakupanda bure.
 
Kwa kiasi kikubwa ni kweli, benki zote maumivu. Lakini baada ya kuzunguka, nimeamua ku settle na CRDB.

Nilijaribu viji benki vingine nikashindwa (Bank of Africa, Akiba Commercial Bank etc.)

Kwanza kabisa kwa benki nyingine kupata kadi yenye visa ni ishu! Wana kitu kinaitwa Umoja ndio kama ki-visa chao cha local hapa hapa Bongo kina transact sehemu yoyote yenye nembo ya Umoja. Hiyo Umoja yenyewe nikakuta kikadi changu kinamezwa mezwa bila sababu halafu kikadi kikimezwa mfano Mlimani City unaambiwa usubiri kirudi Makao Makuu halafu wakitume branch ulipofungilia account Buguruni. Wiki tatu!

Ukipoteza kadi wanakula buku kumi kukupa kadi ingine, halafu kwa mfano Bank of Africa wanatoa kitambulisho cha benki na ATM ambayo haina picha, so utembee navyo vyote viwili. Sasa kwa nini msiweke picha kwenye ATM kama CRDB ili kupunguza vikadi vya kubeba kutunisha wallet wakati mtu huna kitu?

Haya kuna hii benki ya posta. Kuna siku tumegandishwa mda mrefu sana bila kuambiwa sababu, nje ATM ime boomer, akaja Mhindi mmoja wakatuomba tumwache apite, akawabwagia deposit ya miburungutu mikubwa pwaaaaa, ndio tukaitwa eti tu withdraw laki laki zetu, hela iliwaishia!

CRDB branch yoyote sidhani kama inaweza kuishiwa na hela wateja wakashindwa ku withdraw. Na ATM wanazo za kumwaga.

Mkubwa huko ndio kabisaaa umeingia pabaya! mm nimetoka kufunga akaunti yabgu huko recently. kama alivyosema mdau hapo juu, hiyo benki mteja akiingia unaonekana kama tatizo, weekend ndio kabisaaa ukitaka hela huwezi kupata labda ukakope kwa jirani, makato ni mengi mno, wafanyakazi wao wengi (sio wote) wana lugha mbovu sana na hawako competent. WEkeza tu kwenye miradi ndugu yangu. Anyway huu ni ushauri wangu tu!
 
jamani nimezunguka kote nashangaa ata anaefagilia crdb me nimegota azania bank ni mwisho akuna makato ya aina yoyote ile zaidiya interest alafu ukifungua acc ya usd bomba sana wana reti nzuri nawakilisha wakuu
 
kwako DRPHONE,
Unaposema wana interest nzuri ktk USD account unamaanisha ni kiasi gani? na je fees ziko vipi ktk hiyo plan?
 
Mkuu kama wadau walivyotangulia kusema hapo juu benki zote za TZ kwa customer care bado sana ila kuna unafuu wa namna fulani katika baadhi ya mabenki. CRDB ni wazuri ila wana bank charges nyingi sana. Exim hawana bank charges nyingi almost ni bure kuweka pesa zako na kuchukua na pia wana MasterCard. Interest rate ya CRDB ni 2% na Exim ni 3 %. NBM na NBC ni wabovu zaidi.

Nilikuwa na account CRDB nikaifunga! Jamaa wana huduma mbaya sijawahi kuona! Yaani hivi vinchi vyetu maskini..kila kitu ni longo longo tuu...hakuna penye unafuu! YAANI KUTAFUTA PESA NI SHIDA HATA KUITUMIA SHIDA..SASA HATA PA KUIHIFADHI NDO INAKUWA TAABU ZAIDI..TUFANYE NINI JAMANI?
 
jamani nimezunguka kote nashangaa ata anaefagilia crdb me nimegota azania bank ni mwisho akuna makato ya aina yoyote ile zaidiya interest alafu ukifungua acc ya usd bomba sana wana reti nzuri nawakilisha wakuu

Nimetembelea website yao jamaa wameficha hizo interest rates. Huenda ikawa ni njia mojawapo ya kuwaibia wateja.
 
Kama benk ni Stanbic benk tu kila kitu kipo poa tembelea upate huduma za kimataifa hakuna foleni hata siku moja,network ya kuaminika dah jamaa nawakubali sana pia wana Visa card!
 
Zote hovyo tu!CRDB wana afadhali lakini wahudumu lugha yao chafu, usiumize kichwa akikujibu hovyo mtukane kidogo halafu mtishie kumnasa vibao hapo anakua mpole na kujirudi.
 
Huyo mdau aliesema benki ni stanbic mmh inakua ngumu kumeza hiyo!mimi nilifungua USD account hapo kwao ili nitumie kama visa!ni longolongo mwanzo mwisho!kwanza huwezi kufanya online transactions!pia minimum deposit ni USD 110!na mwanzoni niliwauliza wakasema inawezekana!baada ya kupata card kuna activation number hazipo!uzushi mtupu!benki za bongo ni kizungu mkuti.
 
Hata kama imekaa ki-promo promo ni sawa tu maana ukilinganisha benki zote CRDB kwa kweli wako juu mimi binafsi nimewakubali na nikajuta ni kwa nini sikufungua akaunti kwao mapema? Hapa kwetu ukienda benki hukai zaidi ya dk 30. Hebu jaribu benki ya makabwela ukione cha moto, mpaka unashangaa kama hao wafanyakazi wao wanafanya kazi kwa kulipwa au wanajitolea? Yaani ni kero tupu (morale ni zero). Siku zingine ukute msitari wenyewe umepiga kona kama tano hivi na kama mko karibu na barabara basi tegemea huo msitari kuukuta uko barabarani!

Ninakubaliana na aliyesema benki zetu zote ni maumivu tu, lakini hata kwa mbumbumbu kuna mjanja wao!! Basi bila ubishi CRDB ni miongoni mwa wajanja wao!
Tatizo la CRDB wana charges nyingi sana kila mwezi wanakata 400, ukiwekewa mshahara wanakata commission charges, ukitumia ATM zao wanakata 500 for each withdraw. Jaribu Barclays hawana ATM withdraw charges.
 
Back
Top Bottom