Bango lililomkasirisha Magufuli huko Kasulu Kigoma na mbebaji kuishia korokoroni

Akihutubia umati mkubwa watu, Katika uzinduzi Wa Barabara ya Kidahwe - Kasulu, Rais John Pombe Magufuli ameonekana live katika vyombo vya habari akimtupia maneno Mwananchi ambaye alibeba bango na mbele ya Magufuli. Rais alisikika akisema "

"Wananchi Wengine Mnajitafutia Matatizo
Hilo Bango Lako Hata Ulionyeshe Silisomi
Haya Nimesoma Mabango Yote Ujumbe Nimeupata

Ninyi Askari Mwacheni Huyo"

Haikufahamika haraka kuwa Bango hilo lilikuwa na ujumbe gani ingawa inatafasiriwa kuwa ujumbe huo utakuwa ni dongo kwa Mheshimiwa.

kuna waanfishi Wa habari walionekana wakichukua picha katika purukushani hizo. tunaomba picha ya ujumbe huo itupiwe humu ili tuuone ujumbe huo ambao haukumpendeza Rais wetu
Wewe ni mkuda na akili yako ina uvimbe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bango lenyewe ndio hili!
FB_IMG_1500718151452.jpg
 
Mange akiongea juu ya akili ya mfalme mnamcharukia ! Sasa kama raisi anavaana na mwananchi mmojammoja,tutegemee nini hapo ?

Iko siku atatoka jukwaani na kumtwanga mtu migumi,kwakua yeye ukweli kwake ni uchochezi ! Mungu,tawala hekima ya mtu wako huyu.hakuna raisi duniani anayefikia vituko vyake,asijekua kivutio cha utalii,tutaficha wapi nyuso zetu ?

Anaona kamaliza wapinzani mitaani,sasa ana anza kupashana na wananchi katika hadhira. Hii ni zaidi ya fedheha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanahabari wetu ni waajabu sana, habari kama hiyo walipaswa waendelee kuchunguza,wamjue kijana na wamfuatilie kama bado yupo au hayupo!
Neno 'kanjanja' limekuja kitambo kielelezo kwamba kuna mtu alishaliona hili la wanahabari vilaza.
Mfano ukisomea udaktari hutakiwi kuogopa mgonjwa yeyote hata aliyekatika miguu unamsaidia.
Sasa hawa jamaa wamekuwa wakiandika habari kwa kutanguliziwa bahasha na walivyosikia kuwa walioripoti habari za TL wamehojiwa ndio kabisaa! Sasa hiyo picha ya bango huenda wanayo lakini wanaogopa kwenda kupimwa mkojo.
Wakubalii kuwa wao ni waandishi grade Q au Z kwa hiyo tukihitaji grade A au B tuimport kutoka Kenya au Ulaya!
 
Akihutubia umati mkubwa watu, Katika uzinduzi Wa Barabara ya Kidahwe - Kasulu, Rais John Pombe Magufuli ameonekana live katika vyombo vya habari akimtupia maneno Mwananchi ambaye alibeba bango na mbele ya Magufuli. Rais alisikika akisema "

"Wananchi Wengine Mnajitafutia Matatizo
Hilo Bango Lako Hata Ulionyeshe Silisomi
Haya Nimesoma Mabango Yote Ujumbe Nimeupata

Ninyi Askari Mwacheni Huyo"

Haikufahamika haraka kuwa Bango hilo lilikuwa na ujumbe gani ingawa inatafasiriwa kuwa ujumbe huo utakuwa ni dongo kwa Mheshimiwa.

kuna waanfishi Wa habari walionekana wakichukua picha katika purukushani hizo. tunaomba picha ya ujumbe huo itupiwe humu ili tuuone ujumbe huo ambao haukumpendeza Rais wetu
Ule mkutano ulijaa wanafunzi kama graduation no wonder kamera za TBC zilimulika meza kuu tu
 
Back
Top Bottom