Bango laigombanisha serikali na Kampuni! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bango laigombanisha serikali na Kampuni!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Jul 16, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Wakala wa Barabara nchini (Tanroads), imesema italing’oa bango la kampuni ya matangazo ya A1 Outdoor, lililojengwa katika hifadhi ya barabara kwenye eneo la Tazara.

  Tanroads imesema kuwa italiondoa bango hilo endapo kampuni hiyo, itashindwa kuliondoa kama ilivyoagizwa na wakala hao.

  Miezi kadhaa iliyopita, Tanroads ilisitisha mpango wa kuweka bango katika barabara zake nchini hadi itakapotoa muongozo mpya kwa wafanyabiashara wa matangazo hayo.

  Agizo hilo, limeonekana kupuuzwa na kampuni ya A1 Outdoor baada ya kuamua kuweka bango kubwa katika eneo linalodaiwa kuwa ni hifadhi ya makutano ya barabara za Mandela na Nyerere kwenye eneo la Tazara jijini Dsm.

  Meneja wa Tanroads mkoa wa Dar es Salaam, James Nyabakari alisema waliiandikia kampuni hiyo, isitishe ujenzi na kung’oa bango hilo kwa kuwa liko kwenye hifadhi ya barabara, lakini imegoma kutekeleza agizo hilo.

  "Yule jamaa baada ya kumuandikia barua alikataa kusitisha ujenzi na akajibu kuwa eneo hilo si la hifadhi ya barabara ya Mandela, bali ni la bustani ya Shirika la Reli kati ya Tanzania na Zambia (Tazara).

  "Sisi tuna uhakika eneo lile ni la hifadhi ya barabara na tulikwenda mbali zaidi tukamjibu na kumtumia nakala ya mchoro wa ramani ya barabara, ikionyesha mipaka ya hifadhi zake, lakini inaonekana hajaridhika, " alisema Nyabakari.

  Nyabakari alisema taarifa kuhusiana na tatizo hilo, wamezipeleka makao makuu ya Tanroads, ili kupata ushauri zaidi wa kisheria kabla ya kuanza kuchukua hatua zaidi.

  Alifafanua wamekuwa wakijibizana baina yao na A1 Outdoor kwa njia ya barua kuhusu bango hilo, lakini kampuni hiyo, lakini haijawa tayari kutii agizo la Tanroads.

  "Akizidi kukaidi sisi tutaling’oa halafu kama yeye hajaridhika ataenda mahakamani kwa sababu sisi tuna kanuni na sheria ambazo zinatuongoza katika kazi zetu," alisema.

  Nyabakari alisema awali A1 Outdoor haikuomba ruhusa ya kujenga bango hilo na kwamba walishtukia na kwamba baadaye walishangaa kuona bango hilo, likiwa tayari limejengwa.


  Bango laigombanisha serikali na Kampuni!
   
 2. M

  Malyamungu JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2009
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hao A1 outdor ni akina nani jamani mbona Tanzania imeshakuwa ya ***** sana. Tunataka barabara ziwe na infrustructure ya kuwalinda watumiaji na siyo vinginevyo. KAma ni matangazo wapeleke mredioni na TV magazeti ndiyo model ya sasa ili kulinda mazingira pia.
   
 3. e

  eddy JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2009
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 9,373
  Likes Received: 3,774
  Trophy Points: 280
  Jamani hawa A1 wanaweka mabango makubwa kwenye corner za barabara. hii inatupa wakati ngumu unapoenesha gari kwenye highway usiku kwani hilo bango huonekana kana kwamba kuna roli kubwa limepaki katikati ya barabara! kumbe bango.
   
 4. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2009
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Jamani kwani bango linazuia vipi hifadhi ya barabara? Bango sio permanent structure ya kusema kwamba litaleta usumbufu endapo watataka kupanua barabara. Bango linaweza kujengwa na kuondolewa wakati wowote. Kwa mawazo yangu mepesi, sioni kama kuna issues ya kupigia kelele hapa labda kama Tanroads meneja anatafuta umaarufu na kutuonyesha kwamba anafanya kazi.

  Tiba
   
 5. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #5
  Jul 16, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  TIBA JIBU LAKO HILI HAPA CHINI, sijui hukuliona?????

  Meneja katafuta umaaarufu gani? kwani hii post kaifanya yeye? achenu dharau wacha watu wafanye kazi, mkipewa mianya mtajenga mpaga maghorofa badala ya matangazo na siku ya kuondolewa mnaandamana na kuikashfu serikali, FUTAENI SHERIA na ONDOENI MABANGO YENU yanatia GIZA mpaka hatuioni vizuri barabara yetu EBO!!!


   
 6. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  A1 ni ya zadock koola
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hawa ni wale waliofadhili kuprint tshirt na picha za mgombea wa urais wa chichiemu mwaka 2005 freeee of charge..ndo maana wanakuwa na jeuri
   
 8. P

  Patrick Nyemela JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tanroads ni wababaishaji, hivi ni bango hilo tu lililopo katika hifadhi ya barabara? au kuna mabango mengi? sisi sote ni mashahidi kuwa asilimia kubwa ya mabango yapo katika hifadhi ya barabara na manispaa zote ndio zimegeuza mradi.

  Kama Tanroads wapo makini na kazi yao wahakikishe mabango yote katika hifadhi ya barabara yanatolewa. Mabango yamekuwa kero mjini na sasa ni sehemu ya uchafu wa mji.
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Jul 23, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Meneja kapeleka hizo habari magazetini - labda pia ni umaarufu, mabango yale yana taa sasa giza linatoka wapi?? na baadhi ya mitaaa imefaidika hasa nyakati za usiku kutokana na mwanga..... hayo ya road reserve ndio kasheshe itabidi walitoe tu!!
   
 10. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280

  Ukiona vyaelea vimendwa!!! Kuna nini kati ya ZK na Tanroads!!?? Ila ZK kama hukufuata taratibu za kitaalam kweka structures kwenye main road/highways 15m apart then rekebisha!!!! Au wanataka kukuvuruga usitoe tena fungu kwa 2010?? Au vipi??
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Marhabaaaaaaaaaaa.... hiyo umeiona mkuu!! maana makampuni ni mengi lakini utaskia link tu somewhere
   
 12. B

  Bunsen Burner Member

  #12
  Jul 23, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 95
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Unajua Tanzania kwasababu hatupendi kufuata sheria za mipango miji, barabara na kila kitu uwa twaja shituka wakati mambo yameshaharibikana miji na barabara zetu haziwezi tena kuwa improved because of the laxity of people who have been given power to enforce these laws! Sheria za Road reserve kwa sie wataalam ziko wazi na yeyote anayejifanya kujenga ovyo within road reserve he is doing it at his own risks provided ziko kwenye road acts za nchi and if it is a gazzeted road i.e town roads. freeways, provincial roads etc na zina kuwa na distance each side from road centre line i.e 31/25 etc. metres for type/class/category of a road of which you are not allowed to build within the road reserve unless you get a permission from the authority. The road reserve serve to allow future use of the area for road extension , servitude for services and installation of road Signs, direction signs and other road information signs for traffic/road users. No body must be allowed to be just because of being connected to who or any political affiliation be above the law and you cant break the law because others they broke the law previously, and they were left off the hook by authority. Please let us all abide the law of the land! like in Dar, TANROADS we need Direction signs and information signs and not OMO or Vaseline etc. mtu unashuka Airport ujui utafikaje Mwenge au Ubungo!!!!
   
 13. B

  Bunsen Burner Member

  #13
  Jul 23, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 95
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Unajua Tanzania kwasababu hatupendi kufuata sheria za mipango miji, barabara na kila kitu uwa twaja shituka wakati mambo yameshaharibikana miji na barabara zetu haziwezi tena kuwa improved because of the laxity of people who have been given power to enforce these laws! Sheria za Road reserve kwa sie wataalam ziko wazi na yeyote anayejifanya kujenga ovyo within road reserve he is doing it at his own risks provided ziko kwenye road acts za nchi and if it is a gazzeted road i.e town roads. freeways, provincial roads etc na zina kuwa na distance each side from road centre line i.e 31/25 etc. metres for type/class/category of a road of which you are not allowed to build within the road reserve unless you get a permission from the authority. The road reserve serve to allow future use of the area for road extension , servitude for services and installation of road Signs, direction signs and other road information signs for traffic/road users. No body must be allowed to be just because of being connected to who or any political affiliation be above the law and you cant break the law because others they broke the law previously, and they were left off the hook by authority. Please let us all abide the law of the land! like in Dar, TANROADS we need Direction signs and information signs and not OMO or Vaseline etc. mtu unashuka Airport ujui utafikaje Mwenge au Ubungo!!!!
   
 14. M

  MWENDAKULIMA JF-Expert Member

  #14
  Jul 23, 2009
  Joined: Jul 17, 2009
  Messages: 961
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Patrick,Manager anasema uwekaji wa mabango mapya ulisitishwa hadi mwongozo utakapotolewa. Hawa jamaa wame-violate hiyo order kwa sababu wameweka bango wakati tayari kuna order ya kusimamishwa uwekaji wa mabango mapya simple like that!!!!
   
 15. Robweme

  Robweme Senior Member

  #15
  Jul 24, 2009
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 178
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tatizo kubwa la viongozi wa serikalini, ni kuwa mara nyingi wanapenda sana kushugulikia vitu vidogo kwa kutumia nguvu kubwa sana hasa katika kutafuta umaharufu.
  Kama mchangiaji wa juu alivyosema mabamgo mengi 99% Dar es salaam yako kwenye ifadhi ya barabara, sasa huyu bwana kwakuwa ameona A1 ni kampuni kubwa,kwakutoa bango lao itakuwa sifa kwakwe.Taroads hawana kazi maofisini, wameshindwa kabisa kuzuia magari yanayopaki au kuaharibikia barabarani na kumwaga oil na diesel au petrol kwenye barabara za rami na kuharibu barabara sasa wanakimbilia mabango.Rami inaharibika kwa kiasi kikubwa inapokutana na mafuta ya diesel yakimwagwa barabarani, na hilo hatujaona kama wamelifanyia kazi wapo wamekaa na kukosa cha kufanya, alafu na kukimbilia mabango ambayo ni temporary structure.
  Tanroads fanyeni vitu vya manufaa kwa wananchi na kulinda barabara za serikali na wananchi wake ili zi last longer, na sio kukaa ofisini na kusema"ataona nitamkomesha", kwa namna hiyo hatuwapongezi kabisa tunawapongeza kwa sababu hamna kazi mnayoifanya, na mhangalie mtapigwa chini na bosi wenu huyo, ambaye naye ameshindwa kushughulikia barabara zinazo haribika mara kwa mara kwa sababu ya uzembe wanu nyinyi nyote, kwasababu ya kupaki magari ovyo barabarani, na kumwaga mafuta ovyo.
  Kitu kingine Tanroads, mmeshindwa kubuni road signs ambazao zitakaa barabarani bila kung'olewa, mnakaa kungoa mabango, acheni kukaa maofisini na kupiga majungu tumkomoe nani.
   
  Last edited: Jul 24, 2009
 16. U

  Umushoshoro Senior Member

  #16
  Jul 24, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 121
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  We si umeona barabara ile inakarabatiwa kuanzia Ubungo hadi bandarini.

  Pia imeshachorwa "fly over" inasubiriwa pesa tu wakati wowote ili kazi iunganishwe na ya ukarabati wa barabara.
   
 17. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #17
  Jul 24, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Tanroads Vis a Vis Manispaa. Ni nani anayelipwa kwa matangazo hayo? Nafikiri ni manispaa, na Tanroads wanaona wao ndio walipwe. Wasilete spinning zao hapa kwa kuzungumzia flimssy issues kama hizo temporary structures ambazo ziko duniani kote.

  Hawa Tanroads wanaacha kushughulika maswala muhimu ya barabara zetu --ujenzi , repea, etc wanazungumzia maswala ya kima cha chini namna hii. F*** Angalia Meneja mzima anavyotoa taswira ya kipuuzi ---BANGO LAIGOMBANISHA SERIKALI NA KAMPUNI. I hate such too low f*** ing thinking and acting of some personalities in the government who think all Tanzanians are always mbumbumbu kama walivyo wao. STOP .
   
 18. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #18
  Jul 24, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Wakishaanza hizo fly overs zao za uongo wawasiliane na AI bango litatolewa kiulaini ?
   
 19. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #19
  Jul 24, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Matangazo siku hizi ni kwenye tv radio magazetini na simu.waache mambo za kizamani ya mabango.Miji mingi dunia za watu hamna mabango
  Sana sana utayakuta kwenye barara za highway vijijini
   
 20. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #20
  Jul 24, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Matangazo siku hizi ni kwenye tv radio magazetini na simu.waache mambo za kizamani ya mabango.Miji mingi dunia za watu hamna mabango
  Sana sana utayakuta kwenye barara za highway vijijini
   
Loading...