Bango la Wafanyakazi - Wafanyakazi Tanzania tuungane! Mei 5th | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bango la Wafanyakazi - Wafanyakazi Tanzania tuungane! Mei 5th

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 3, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 3, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,387
  Trophy Points: 280
  wafanyakaziunite.jpg

  sambaza kwa email za wafanyakazi wenzako! Inaonekana serikali imeamua ubabe badala ya maelewano; hakuna serikali duniani imewahi kushindana na nguvu za wafanyakazi ikasimama!

  Mgomo: Tucta yawaonya wafanyakazi waoga, wasaliti

  Jackson Kimambo

  Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini (Tucta) limesema wafanyakazi waoga, wanafiki na wasaliti watakaoshindwa kushiriki katika mgomo Mei tano mwaka huu ni vyema wakafahamika na kushughulikiwa.
  Hayo yalisemwa na mjumbe wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi (Tucta) kutoka makao makuu, Ernest Kangwa, katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani yaliyofanyikia kimkoa katika uwanja wa Chuo cha Ushirika mjini Moshi juzi.
  Hata hivyo, Kangwa hakufafanua wafanyakazi waoga na wasaliti watashughulikuwa namna gani.
  Alisema anatambua wapo wafanyakazi wasaliti watakaoshindwa kufanya mgomo kutokana na kuwaogopa waajiri na kwamba kamwe shirikisho la vyama vya wafanyakazi haliwezi kuwavumilia wafanyakazi wasaliti.
  Kangwa alisema wafanyakazi wasikubali kugawanyika kwa vitisho toka kwa waajiri na kuwa shirikisho limeandaa mgomo wa kisheria hivyo hakuna mfanyakazi atakayechukuliwa hatua za kisheria ama kufukuzwa kazi.
  Alisema mgomo huo ni wa amani mpaka hapo madai yao yatakapotekelezwa na kwamba wafanyakazi watambue kuwa haki haiji hivi hivi hivyo ni lazima itafutwe na kudaiwa kwa namna na hali yoyote ile .
  Alisema hakuna ubishi kwamba serikali imeshindwa kutatua kero za wafanyakazi ikiwa ni pamoja na mishahara duni, makato makubwa ya kodi na malipo duni ya uzeeni.
  Alisema serikali imeshindwa kudhibiti na kuwashughulikia wahujumu wa uchumi ambao wanachangia kwa kiasi kikubwa katika kuikosesha uwezo wa kuwahudumia wafanyakazi.

  NIPASHE
   
 2. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #2
  May 3, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  HakikA huyu ni rais wa ajabu kuliko marais woote nchi hii imewahi kuwa nao tangu Uhuru....wafanyakazi nitashangaa kama wao na familia zao watavote kwa CCM, LET THEM DIE.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hii itaenda mkuu...

  Rais gani anaeringia nguvu za polisi HUYU?
  Anasahau kabisa waliomchagua!
  Amekuwa bubu kwa wanaompa hela za kampeni, anatubwatukia wafanyakazi...IHATE HIM!
   
 4. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #4
  May 3, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  nimeanza kumchukia huyu Rais siku nyingi lakini sasa akili zake halisi zinajionesha, uwezo wake umefikia mwisho, mfalme ananywea pombe kikombe cha kanisani. amejisahau sana, shame on him, i hate You.
   
 5. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2010
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Hii ni mwanzo tu subirini akishashinda muhula wa pili. TUCTA nipo pamoja nanyi
   
 6. bht

  bht JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  huyu rahisi wetu huyu jamani..........
  nilie ...........hapana
  nimtukane ..............hapana haitasaidia

  I will just do my bit............................
   
 7. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #7
  May 3, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Rais kawatisha wafanyakazi sijui kama watagoma,amewatisha kwamba watapoteza ajira zao na kwa ninavyowafahamu watanzania sijui kama watagoma.Chakushangaza amelekeza mashumbulizi kwa Mgaya pekee,nimemshangaa sana.
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  May 3, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  kwa Watanzania niwajuavyo mimi hasa wanachama wa TUGHE HAWAWEZI KUGOMA, sasa lililopo Wafanyakazi wamuoneshe onyesho la maisha yake, wamsusie ofisi yake, mbona madaktari waliweza kugoma na mishahara ikapanda ?
  wITO WANGU KWA WATANZANIA WENZANGU VITA NDO IMEANZA , JK ANAWATUSI . AMKENI
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  May 3, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,387
  Trophy Points: 280
  Hivi wafanyakazi walitarajia Rais aseme nini? Rais anataka kutumia nguvu zaidi lakini ukweli ni kuwa Kikwete siyo Mkapa! Kikwete hawezi kutumia nguvu dhidi ya wananchi. Na zaidi hataki kabisa kuwatisha wawekezaji hasa ukizingatia kuwa WEF nayo inakuja siku hiyo hiyo.. Wafanyakazi wakigangamala hasa kesho watakapotoa majibu yao yasiyo na utata basi Kikwete mwenyewe atabembeleza kukutana nao!
   
 10. M

  Marigwe JF-Expert Member

  #10
  May 3, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
 11. Mwasi

  Mwasi JF-Expert Member

  #11
  May 3, 2010
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 249
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hivi jamani, eti akilipa laki tatu kumi na tano selikari itaishiwa hela ya kutoa huduma nyingine. Hakumbuki kuwa amewaachia EPA na mfumo mbaya wa kuiba pesa , haoni kama anawadhulumu wananchi, halalamiki na haoni kuwa kuwalipa pindukia wabunge ni kuwadhulumu wananchi. Tz kweli tuna Rais, tunahitaji kubadilika na kuamka kutoka usingizini!!
   
 12. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #12
  May 3, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  .....................mnh ukisikia kwenda nje ya mada ndiyo huko sasa!!!
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  May 3, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,083
  Trophy Points: 280
  Wafanyakazi wa Tanzania hawana umoja angalia wale juzi waliandamana kwenye mei mosi pale Mnazi Mmoja. Wataburuzwa tena tu na hawatopata wanachokitaka kutokana na kutokuwa na umoja.
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  May 3, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,387
  Trophy Points: 280
  Mr. Man.. wale walilipwa kwenda kwenye mei mosi ya serikali!
   
 15. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #15
  May 3, 2010
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Walilipwa kutokana na nini?ni fungu lipi linapia maandamano ya Mei mosi?

  kuna baadhi ya maneno nimeyasoma kwenye blog ya michuzi yamenisikitisha sana..Yaani alitegemea viongozi wa TUCTA watalainishwa na posho walizokuwa wanapewa...

  Mwanakajiji fuatilia ujue ni kiasi gani walikuwa wanapewa...Hongo iliyokataliwa!

  ili tukubali yaishe?
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  May 3, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,387
  Trophy Points: 280
  aisee sijui hilo fungu wanatoa wapi, lakini wale waandamani wote walijiandikishe kule ofisini, mara ya mwisho nakumbuka mwaka jana walilipwa shilingi elfu ishirini kila mmoja (wale wa ATCL) sijui mwaka huu wamelipwa per-diem ya kiasi gani.
   
 17. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #17
  May 3, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Hawa viongozi wa TUCTA wakae chonjo......kwa jinsi muungwana anavyoashiria kutokujali sheria kuna uwezekano mkubwa wakakamatwa hata kabla ya hiyo tarehe ya mgono!
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  May 3, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,387
  Trophy Points: 280
  hawezi kuzuia kesho atajibiwa kwa maneno ambayo hayawajahi kutolewa dhidi ya mtawala!
   
 19. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #19
  May 3, 2010
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Hivi ni kwanini alichagua kuongea na wazee?

  alitakiwa awaite walimu na kuwaeleza ukweli
   
 20. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #20
  May 3, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,322
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  Unajua jamani, huwezi kumpa mtu kitu ambacho huna. Hekima ya kuongoza huja baada ya kuomba sana kama Mfalme Suleiman. Historia ya nchi yetu bado inaendelea kuandikwa. Mtu akiwa mpumbavu basi kwa hakika ajue historia itamuandika hivyo hivyo na vizazi baada ya vizazi viataendelea kusoma habari za upumbavu wake.
  Kuongoza jamani ni kazi nzito...sio kuuza sura kama tulivyokuwa tunafikiri. Watu wanataka kuona action za kuonyesha kuna sehemu nzuri tunakwenda. Sasa hivi wakati maisha yanazidi kuwa magumu, kila siku kunatoka habari za watu wachache wanaonufaika na wizi na dhuluma za mali ya umma bila kuchukuliwa hatua zozote na kibaya kabisa watu hao wako katika circles ambazo viongozi wanapitia pitia. Mnafikiri wafanyakazi watafanya nini? Wakiugua hawaendi kutibiwa nje, wakipeleka watoto shule, basi ni st Kayumba! Ni kwanini wasiseme you guys are not serious????
   
Loading...