Bangladesh: Tukio la kiwanda cha juisi kuteketea kwa moto, mmiliki akamatwa kwa mauaji

chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
7,581
15,712
Polisi nchini Bangladesh wamemkamata mfanyibiashara anayemiliki kiwanda cha kutenengeneza juisi, siku moja baada ya familia za waathiriwa wa moto uliosababisha vifo vya watu 52 kwenye kiwanda chake kudai kuwa lango la pekee la kampuni hiyo lilikuwa limewekwa kufuli wakati wa mkasa huo wa moto.

Jumla ya washukiwa 8 wamekamatwa kuhusiana na moto huo ikiwemo mwenye kampuni, wanawe wanne na washukiwa wengine 3, waziri wa mambo ya ndani Asaduzzaman Khan amesema. Miili 49, baadhi ikiwa imechomeka kaisi cha kutotambulika, ilitolewa kwenye vifuzi vya kampuni hiyo ya orofa sita ambayo ilishika moto Alhamisi jioni.

Mnamo siku ya Ijumaa, familia za waathiriwa walifanya maandamano karibu na kiwanda hicho wakilalama kuwa lango la pekee la kuingia au kuondoka kwenye kiwanda hicho lilikuwa limefungwa wakati wa tukio la moto. Washukiwa wanakabiliwa na mashitaka ya mauaji na majaribio ya mauaji kuhusiana na mkasa huo uliotokea katika kitongoji cha Narayanganj, viungani mwa mji wa Dhaka.

IMG_7654.jpg

IMG_7653.jpg

IMG_7652.jpg

IMG_7651.jpg

IMG_7650.jpg

IMG_7649.jpg
 
Pole yao
Ila matatizo mengine ya kujitakia kweli kiwanda halafu mlango mmoja tu na umepigwa kufuli

Serikali pia wangewajibishwa kuruhusu kiwanda bila fire exists
 
Back
Top Bottom