Bandari zetu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bandari zetu.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mtoto wa Mkulima, Nov 23, 2007.

 1. Mtoto wa Mkulima

  Mtoto wa Mkulima JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2007
  Joined: Apr 12, 2007
  Messages: 687
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Sasa hivi meli za nnje haziendi Tena Tanzania kwasababu bandari ya Dar imejaa sana. Nilituma mzigo wangu ilibidi ukae Mauritius mwezi mmoja kabla haujafika huko. Tunabandari ya Mtwara lakini bado haiko sawa ile ingesaidia sana mizigo ya nchi za Malawi etc laini tatizo ni miundo mbinu.

  Najiuliza jamani kwa sababu Tanga iko stategic area inabarabara safi, reli ipo population sio kubwa vile, gharama ya kuhamisha watu sio kubwa. Kwanini serikali isifanye mpango wa kuipanua hiyo bandari na ikiwezekana wajenge bandari mpya ya Tanga ambayo naamini itaweza kuipa Mombasa port competition kubwa sana naamini inawezekana kabisa. Naoamini hii ni project viable kabisa kwa simple analysis yangu. Najua inahitaji capital kubwa lakini najua makusanyo yatarudisha hizo pesa.

  Kunakipindi serikali ilikuwa na mpango wa kujenga bandari Bagamoyo sijajua hili liliishia wapi. Nadhani kuna haja zaidi ya kuboresha bandari zetu hasa ya Dar na Tanga. Tunapoeza mabilion ya pesa jamani serikali mko wapi? Tutumie hii bahati mungu aliyotupa jamani. Inauma sana kuona tunakila kitu lakini we can not make money. WHY?
   
 2. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2007
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..kweli hali sasa inatisha!mizigo imelundikana na tumebaki kupiga politik tu!

  ..mtwara ni bandari nzuri kama itaendelezwa na tanga hali kadhalika!tatizo issues kama hizi huwa hazionekani kama priority!na ndio maana hatu-develop!

  ..halafu,miundombinu ni michakavu isiyoweza kusitahimili idadi ya mizigo inayoingia kwasasa,tatizo nayo haiboreshi,basi kaazi kwelikweli!
   
 3. Mtoto wa Mkulima

  Mtoto wa Mkulima JF-Expert Member

  #3
  Nov 23, 2007
  Joined: Apr 12, 2007
  Messages: 687
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Ni kweli mkuu hiyo sio priority yetu na ukitaka kujua utaona watu hata hapa hamna mchangiaji. Nadhani priority zetu ziko kwenye kupiga umbea na siasa tuu ambazo hazisaidii.
   
 4. K

  Kasana JF-Expert Member

  #4
  Nov 23, 2007
  Joined: Apr 3, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  kuchangia kunatokana mapenzi ya mtu, issue inaweza kuwa nzuri, lakini wengi tukawa hatuna supporting evidence.

  Kuhusu Bandari ya Dar, mimi binafsi sina evidence, mara ya mwisho niliship mzigo ulichukua wiki tatu ambayo mimi niliona ni fair, tatizo lilikuja TRA na Overestimate, Shpping Comp 'na house to house', ndipo nilipoboreka zaidi.

  Kuhusu Bandari/Mtwara/Tnaga,
  Kwa Mtwara kuna taarifa kuwa Serikali inampango wa kuiinua kuweza kupokea mizigo ya nje, ndio maana wanakazana kukamilisha barabara, na kuna ule mradi wa 'MTWARA CORRIDOR' na pia kuna lile daraja linalounganisha msumbiji na Bongo linakaribia kwisha.
  Barabara kutoka Masasi hadi Mangaka inajengwa kwa msaada/mkopo/grant(wht ever) kutoka JAPAn/JICA.

  Na pia ule uwanja wa ndege baadawe utarekebishwa ili kupokea ndege zinazotoka nje.

  source: none
   
 5. C

  CHAUMBEYA Member

  #5
  Nov 26, 2007
  Joined: Nov 15, 2007
  Messages: 69
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kwa kweli tatizo la bandari ya dar es salaam si udogo wa bandari bali ni namna ya kutoa mizigo iliyolundikana pale!! kazi hiyo inafanywa na TICTS!! kwa kuwa hawa hawana vifaa vya kutosha wanfanya kazi kwa kutegea na hata waambiwe vipi hawasikii. unajua nini kinawapa kiburi? wana mkataba wa kukodishwa container terminal kwa miaka 20 ambao ukuivunja ni kama ka IPTL fulani. yaani utalipa hela mpaka uchoke!! na si unajua mmiliki wa TICTS ni yule yule mtaalamu wa maskendo kinara wa buzwagi?

  yule jamaaa ni mwisho. ndani ya ccm anaogopewa yule. EL ameshafanya ziara tatu za kushukiza pale TICTS (ingawa mzee wa buzwagi anakuwa na taarifa nazo kwa hiyo EL akifika anakuta siku hiyo kazi inapigwa kweli kweli na makontena yanamuv faster na anaambiwa tatizo ni kuwa siku hizi meli zinakuja nyingi. akiondoka ni bussiness as ussual). mitambo ya kukodishwa inarudishwa kwa wenyewe.

  ila nasikia kuna siku el alijifanya kondakta wa lori akaenda pale TICTS usiku kuobserve ila watu wa mzee wa buzwagi pale usalama wa taifa wakamtell kuhusu hiyo ishu na EL akazodoka maana mzigo wao ulikuwa cleared in a very short time.
   
 6. Mtoto wa Mkulima

  Mtoto wa Mkulima JF-Expert Member

  #6
  Dec 5, 2007
  Joined: Apr 12, 2007
  Messages: 687
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0

  Source:http://www.bdafrica.com/index.php?option=com_content&task=view&id=4702&Itemid=5810
   
 7. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #7
  Dec 5, 2007
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Zaidi ya Bandari za Dar, Tanga na MTwara, Bandari ya Zenj ambayo sasa inafanyiwa matengenezo inaweza kwa kiasi kikubwa kupunguza mlundikano wa mizigo katika bandari ya Dar.
   
 8. Mtoto wa Mkulima

  Mtoto wa Mkulima JF-Expert Member

  #8
  Dec 5, 2007
  Joined: Apr 12, 2007
  Messages: 687
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mkuu unajua hizi bandari kama zinafanya kazi vizuri na reli yetu tuliyoachiwa na mjerumani kama inafanya kazi vizuri na uhakika zitaingiza mapea mengi kuliko hata madini na impact yake kwenye uchumi ni kubwa sana. Unaona wenzetu wa Kenya wanataka Mombasa iwe kati ya bandari 20 kubwa duniani. That is gud dreams.
   
 9. m

  mwewe Senior Member

  #9
  Dec 5, 2007
  Joined: Jul 17, 2007
  Messages: 125
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  TICTS toka waingie pale hawajawekeza lo lote!

  Mishahara kwa wazalendo ni kidogo licha ya kazi nyingi kufanywa na vibarua ambao wana miaka kadhaa bila ajira ya uhakika; Vifaa vingi vinavyotumika pale ni vile vile vya THA.

  Ni moja ya mikataba inayohitaji mapitio ya kina!!
   
 10. M

  Major JF-Expert Member

  #10
  Feb 15, 2008
  Joined: Dec 20, 2007
  Messages: 1,425
  Likes Received: 1,143
  Trophy Points: 280
  Usijichoshe Ndugu Yangu Hapo Kwetu Ni Longo Tu Na Wala Usishangae Ndugu Yangu Kwani Juzi Kati Hukusikia Lowasa Ameenda Kununua Mvua Thailandi? Na Baada Ya Siku Tatu Tukasikia Rais Wa Thailand Amepinduliwa. Haya Ni Yale Mambo Ya Prof J Chemsheni Bongo Wanangu Viongozi Hamna Hapo.
   
 11. M

  Major JF-Expert Member

  #11
  Feb 15, 2008
  Joined: Dec 20, 2007
  Messages: 1,425
  Likes Received: 1,143
  Trophy Points: 280
  Wanawapiga Longo Ili Mzubae Waendelee Kuiba.kwani Kuna Haja Gani Ya Kujenga Bandari Bagamoyo Wakati Kuna Bandari Ya Tanga Ambayo Inahitaji Tu Ukarabati Kidogo Pamoja Na Nyongeza Ya Wafanyakazi?huu Ni Uenda Wazimu
   
 12. M

  Major JF-Expert Member

  #12
  Feb 15, 2008
  Joined: Dec 20, 2007
  Messages: 1,425
  Likes Received: 1,143
  Trophy Points: 280
  Sasa Hivi Ktk Maisha Yangu Kitu Kinachoniuma Sana Roho Ni Pale Ninapofikiri Tu Juu Viongozi Wetu Tuliona Serikalini, Uwezo Wao Wa Kufikiri Na Maamuzi Yao Yananitia Presha Na Sijui Tutafanyaje Maana Ni Bomu Na Hawana Mbinu Na Hii Ndiyo Maana Wamefikia Mahala Mgonjwa Wa Tumbo Wanamfunga P.o.p
   
Loading...