Bandari za Tanzania bado zitabaki kuwa suluhisho kwa waagizaji wa mafuta Afrika

cheusimangala_

Senior Member
Dec 1, 2018
114
174
Mamlaka ya Bandari Tanzania (Tanzania Ports Authority) ni shirika la umma linalofanya kazi zake chini ya Wizara ya Miundombinu. Na ina jukumu zima la kuongoza na kuendesha bandari za bahari na maziwa ya nchini Tanzania. Mamlaka hiyo ipo mjini Dar es Salaam na ni bandari mwanachama wa Jumuia ya Uongozaji wa Bandari za Kusini na Mashariki mwa Afrika.

Baadhi ya nchi zimepunguza gharama za usafirishaji pamoja na gharama za mafuta na sababu za kupunguza? Ni Waagizaji waliamua kutumia bandari ya Dar kwa sababu ya efficiency na charges ni reasonable efficient na well organised on oil issues kwa sababu ya mfumo wa bulk imports pamoja na kuwepo na ulinzi mzuri na imara, tofauti na nchi za wenzetu ambazo waigizaji imewapa ugumu sana ikiwepo nchi ya Kenya ambapo waagizaji wa mafuta wanapata ugumu kutokana na kuwa umbali mkubwa kwa kuwa wasafirisha hadi Kisumu jetty.

Hivyo bandari za Tanzania bado zitabaki kuwa bora katika nchi Afrika
 
Nijuze! Mbona nasikia Rwanda na Zambia mafuta ya Petrol na Diesel ni cheap kuliko TZ? Ingawa mafuta yanapita hapa hapa DSM? Nilitegemea hapa tununue rahisi zaidi! Naomba nieleweze !
 
cheusimangala,

Bandari haipanuki kwa kiwango cha kutoa huduma inayohitajika.
Berth 12 kwa miaka 60 ni utani mkubwa sana tunataka berth 100 na zaidi ndio mje na majigambo. Kichefuchefu tembelea nchi kama Singapore ujue ninalosema.
 
Mafuta NI raisi Sana. Wabunge wameongeza ili kupata pesa za kutandaza Umeme na barabara kwa wengine
 
Kama Kenya kapunguza tozo kwa 50% hata ukileta uzi hapa mara mia hauwezi kuzuia hizo nchi kutumia bandari ya Kenya.
 
cheusimangala,

Bandari haipanuki kwa kiwango cha kutoa huduma inayohitajika.
Berth 12 kwa miaka 60 ni utani mkubwa sana tunataka berth 100 na zaidi ndio mje na majigambo. Kichefuchefu tembelea nchi kama Singapore ujue ninalosema.
Eenh, Sblandes Bhwanah,. Eti "tembelea...." si heri ungemwagika tu hapa tukusome jinsi ulivyoshuhudia mwenyewe ulipotembelea...! Sasa sote kweli tutaweza kwenda huko Singapore na kujionea wenyewe?

Ninakubaliana sana nawe kuhusu hali ya Bandari yetu ya Dar es Salaam. Kwa sasa imejitahidi sana kujaribu kunyoosha mambo yake ya kiutendaji; lakini pamoja na juhudi hizi nzuri, maumbile yake hayatairuhusu kutoa ushindani mkubwa na bandari ambazo maumbile yao yanaziruhusu kushindana. Berth 100, Dar itazitoa wapi kwa mfano!
 
Kama Kenya kapunguza tozo kwa 50% hata ukileta uzi hapa mara mia hauwezi kuzuia hizo nchi kutumia bandari ya Kenya.
Kenya wanahangaika sana kujaribu kuzirudisha nchi hizo Mombasa, si kwa biashara ya mafuta tu, bali na mizigo mingine.
Kupunguza tozo kuvutia wafanya biashara wamefanya, lakini haikusaidia kitu. Ile ilikuwa ni 'promotion' tu ya muda kuwarudisha wafanya biashara, halafu waendelee na bei zao za zamani. Wafanya biashara hawakuwa 'impressed' hasa baada ta Dar es Salaam kuwa wamaonyesha dalili nzuri kiutendaji.

Kenya wamejejenga (karabati) bomba la mafuta ili waiteke biashara hiyo kwa mikopo yenye gharama kubwa, halafu na 'corruption' kubwa ilihusika. Mikopo hiyo ni lazima ilipwe kutokana na faida inyopatikana kutokana na bomba hilo.
Kwa hiyo, "kupunguza tozo" kwao kuna kikomo.
 
Nijuze! Mbona nasikia Rwanda na Zambia mafuta ya Petrol na Diesel ni cheap kuliko TZ? Ingawa mafuta yanapita hapa hapa DSM? Nilitegemea hapa tununue rahisi zaidi! Naomba nieleweze !
Myths, gharama za mafuta Zambia ni juu kuliko Tanzania, pale Tunduma Gari nyingi za upande wa Zambia zinajaza mafuta upande wa Tanzania
 
Tusibweteke
Mozambique wanaboresha bandari zao ili zihudumie Malawi.
Angola ameboresha bandari na reli zake na wanahudumia Zambia na DRC.
Tuwe makini wakati wote kupambana na USHINDANI.
Hawataweza kupambana na fitna za Tanzania, kwenye suala LA ushindani hao Zambia na Congo watabaki wakitumia bandari ya Tanzania
 
Tuachane na hii biashara ya kuwategemea wengine eti watumie bandari yetu kupitishia mizigo yao..

Tuongeze production sisi wenyewe ili kila kinachoingia kiwe kama malighafi kwetu na kutoa product zetu kupelekea wengine woldwide... Tufanye production ya kutosha tuuze products mbalimbali na hayo mafuta 80% iwe kwa ajili yetu kuendeshea mitambo na matumizi ya watu wetu..
 
cheusimangala,

Bandari haipanuki kwa kiwango cha kutoa huduma inayohitajika.
Berth 12 kwa miaka 60 ni utani mkubwa sana tunataka berth 100 na zaidi ndio mje na majigambo. Kichefuchefu tembelea nchi kama Singapore ujue ninalosema.
We jamaa bhana sasa bandari ya Tanzania kwani umeambiwa itàhudumia hadi nchi za Asia au?
 
cheusimangala,

Bandari haipanuki kwa kiwango cha kutoa huduma inayohitajika.
Berth 12 kwa miaka 60 ni utani mkubwa sana tunataka berth 100 na zaidi ndio mje na majigambo. Kichefuchefu tembelea nchi kama Singapore ujue ninalosema.

Berth 100 mkuu tutavunja posta yote na kigamboni pale, kifupi lile eneo sio rafiki tena na speed ya dunia.. Kama tunataka kukimbizana na uhalisia tutafute eneo lingine la kujenga bandari...
 
Mamlaka ya Bandari Tanzania (Tanzania Ports Authority) ni shirika la umma linalofanya kazi zake chini ya Wizara ya Miundombinu. Na ina jukumu zima la kuongoza na kuendesha bandari za bahari na maziwa ya nchini Tanzania. Mamlaka hiyo ipo mjini Dar es Salaam na ni bandari mwanachama wa Jumuia ya Uongozaji wa Bandari za Kusini na Mashariki mwa Afrika.

Baadhi ya nchi zimepunguza gharama za usafirishaji pamoja na gharama za mafuta na sababu za kupunguza? Ni Waagizaji waliamua kutumia bandari ya Dar kwa sababu ya efficiency na charges ni reasonable efficient na well organised on oil issues kwa sababu ya mfumo wa bulk imports pamoja na kuwepo na ulinzi mzuri na imara, tofauti na nchi za wenzetu ambazo waigizaji imewapa ugumu sana ikiwepo nchi ya Kenya ambapo waagizaji wa mafuta wanapata ugumu kutokana na kuwa umbali mkubwa kwa kuwa wasafirisha hadi Kisumu jetty.

Hivyo bandari za Tanzania bado zitabaki kuwa bora katika nchi Afrika
Sawa msbweteke sasa
 
Berth 100 mkuu tutavunja posta yote na kigamboni pale, kifupi lile eneo sio rafiki tena na speed ya dunia.. Kama tunataka kukimbizana na uhalisia tutafute eneo lingine la kujenga bandari...
Mkuu bandari yetu imejengwa kizamani na inazidi kujengwa kizamani shida ndio hiyo.wangetengeza mitaro mingi ya kufunga meli kwa kutumia eneo dogo.Waombe ushauri tuwape somo.
 
Back
Top Bottom