Bandari yetu ya Dar es salaam ni kichefuchefu

mwanatanu

JF-Expert Member
Jan 22, 2008
854
127
JJamani kweli port yetu ni uwozo naomba wabongo pale U.K mkiweza mwulizeni huyo Mhe ana mpango gani kuhusu port yetu ya Dar.(nasikia mnakutana naye 18th aprill)

Nilipeleka mzigo ili kuanzisha mradi nyumbani na hapa napoishi wakazi wengi ni wa Zaire na Wa Rwanda na walinishauri nisitumie kabisa port ya bongo bali nitumie port eti ya manyan'gau.

Mimi kwa uzalendo sikukubali...mzigo umefika mimi nipo dar na likizo ya siku 25...imenichukua 34 days ku clear a container 20ft.

Ni maajabu nimelipishwa mapesa ya ajabu mpaka najuta imenirudisha nyuma 10 yrs.....Yaani sijawahi kuona unaenda TRA unaambiwa fulani wa kusaini hayupo rudi kesho. Tutafika kweli hawa viongozi wanaona hivi au vipi
 
Kwa wale ambao hawajakumbwa na hayo matatizo hawajui UJIMA na UKABAILA huu uliopo hapo forodha na pale kitengo cha makotena geti namba 5 bandarini.Hapo bado usumbufu wa mawakala.
Duh kweli bado tuna safari ndefu.Tutaendelea kusikiliza ngoma ya kayamba hadi lini hapo bandarini?

Wengi wameona afadhali kupitishia mali zao bandari ya Mombasa maana hakuna ukiritimba.Kinachoshangaza ni kwamba haya mashirika yamekuwa ya watu na wala si kuhudumia umma tena.Hata sahihi za wahusika zinabinafisishwa kwa mtu mmoja na asipokuwepo njoo wiki ijayoooooooooooo,bul shit,kwa ukifa leo mbona kuna wengine wataweka sahihi kwa hizo docs...
 
Tanzania inatia huruma kila kitu kimeoza . Mimi najiuliza where are we heading ? Inatia huruma kuona kila mtanzania anatumia Bandari ya Mombasa badala ya Dar ! Haya yote ni matokeo ya kuweka mafisadi mbele na kuweka tax zisizo na vichwa wala miguu . Nashindwa kuelewa kwa nini tunashindwa kumanage kila kitu ...besides tuna banfdari nyingine nzuri na natural pale Mtwara tunashindwa kutumia. Kuna jaama yangu mmoja aliniambia alipeleka Truck lake Dar alipoenda kulitoa halikuta jamaa wameiba kila kitu na baadaye watu walimfuata na kumuuzia huyo jamaa zile part zilizotoka kwenye gari yake.

Tatizo nini haswa ? What about our children what are they going to inherit ? Watu wa London mtusaidie jamani muulizeni huo muungwana hayo maswali .
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom