Bandari ya Dar es Salaam

Mpangawangu

JF-Expert Member
Mar 5, 2014
802
1,000
Wadau leo Dr Harison Mwakyembe amehitimisha bajeti yake huku watanzania tukiwa tunaendelea kuibiwa bandarini.

Naomba wale wajuvi wa mambo ya bandari mnisaidie na kuwasaidia watanzania wenzangu ambao wsnaibiwa pale bandarini bila kujua nini tunapaswa kufanya.

Hivi nikiingiza gari,kwa mfano Toyota hiace van,Noah na Rav 4.gari zote zimeshapitisha miaka 10,je kwa utaratibu wa bandari yetu ,Toyota hiace itatozwa kwa kigezo cha cc kati ya 1001-2000 na kuendelea? au watatumia kigezo cha 10 pasenger and above? hebu tazama vigezo vyao.

TAX RATES
C.C Import Duty Excise duty Extra Depreciation Duty VAT 0-1000 25% - 20% 20% 1001-2000 25% 5% 20% 20% 2001 and above 25% 10% 20% 20%.

Pick ups 15% 0% 0% 20%.

Trucks (trucks for pulling semi-trailers) 0% 0% 0% 20%.

Buses (from 10 passengers) 25% 0% 0% 20%.

Land cruiser Hard tops carrying from.

Samahani sana wakuu najua haijakaa vizuri maana nime copy na kupest.

Je kodi za bandari zinatozwa je kwa kuzingatia huo mwongozo?
Je pindi mteja anapokuta gari haina vitu ambavyo awali vilikuwemo (mfano screen) Jeki ,power window,power mirrow,je nitalalamika kwa nani ili nilipwe vitu vyangu?

Naombeni mnipe mwongozo hasa wale ambao mpo hapo bandarini.

======

Nimeikuta sehemu hii
.....................
Kwa wale mnaoratajia kununua Hiace kwa ajili ya kutoa huduma ya usafirishaji maeneo ambayo usafiri huu bado ni muhimu (hususani maeneo ya miji midogo na ama kusafirisha wanafunzi maeneo ya mijini) kuweni macho na TRA.

Jamaa yangu mmoja amenunua Hiace baada ya kuona katika Calculator ya TRA (Tanzania Revenue Authority - Calculators & tools) kuwa Hiace zote ziko katika kundi la Utility ikiwa ni pamoja na magari mengine kama vile: Toyota Hilux, Canter, Nissan Hard body, Rosa, Coaster, Civilian, na kwamba magari yote katika kundi hili yana aina tatu tu za ushuru (kwa magari chini ya 2004) , yaani Import duty 25%,Excise duty 5%, na VAT 18%). Baada ya Hiace kufika BANDARINI ndipo yakampata majanga.

· Wanamwambia kwakuwa Hiace yake ina viti vyote ndani sio utility.
· Harmonised system (H.S ) code (Harmonized System - Wikipedia, the free encyclopedia) iliyopewa garin yake ni 87032399 (HS Code 87032399 | Harmonized System Code Other) badala ya H.S code 87029091 (Motor vehicles for the transport of ten or more persons, including the driver ITC HS CODE List.)

· Kwa mujibu wa TRA HIACE yake iko kwenye kundi la station wagon au racing cars (Station wagon - Wikipedia, the free encyclopedia, https://www.google.com.au/search?q=s...w=1366&bih=667) .

· Kwa maana hiyo uwepo wa viti kwenye Hiace yake umeongeza kodi kutoka wastani wa milioni 5.5 hadi milioni 9 (karibu milioni 4!!).
· Kwa maana kwamba sasa atatakiwa kulipa aina nne za ushuru (yaani Import duty 25%, uchakavu 25% ,Excise duty 10%, na VAT 18%) tofauti na calculator inavyosema.

Ushauri:
· Ili kuondoa usumbufu kwa watanzania, na kuongeza uwazi kwa taasisi hii, TRA hawana budi kuorodhesha kwenye mtandao wao gari zote zinazotambulika kama "utility" nchini Tanzania ili wananchi waweze kujua na kujiandaa. Siyo lazima na ni usumbufu kama kila anayetaka kununua kitu nje ya nchi awasiliane kwanza na TRA kujua taratibu zinasemaje.

· TRA wanatakiwa kufanya marekebisho kwenye calculator yao (hususan eneo hili) maana linapotosha jamii badala ya kuelimisha· Wale wanaotarajia kununua Hiace hakikisheni hazina viti ndani na/ama fanyeni utaratibu viti viondolewe hukokuko gari inapotoka au mara tu baada ya kufika bandari kavu. Hii ni kwa sababu marginal benefit ya Hiace isiyo na viti ni kubwa kuliko yenye viti.

TRA, HUU KAMA SIO WIZI NI UPOTOSHAJI MKUBWA
 

NYABISHABO

Member
Oct 27, 2011
50
125
Sijawahi ona mfanyakazi wa TRA mwenye nia njema na mteja wao huwa wanawaza fedha tu na ubabe ufanisi kwao zero
 

Bondpost

JF-Expert Member
Oct 16, 2011
2,070
2,000
Bandari haihusiki na kodi unazotozwa. Ndio maana wao wanakuchaji port charges, wharfage and handling hayo mengine hawahusiki.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom