Bandari ya Dar Es Salaam na soko la Kariakoo ni fursa ya dhahabu kwa watanzania

Unayoyasema yangewezekana kabisa kama tungebahatika kupata uongozi wenye maono.

Na nchi ikikosa uongozi, hata muwe na kila kitu, hamfiki popote, na ndicho kinachotokea kwa Tanzania.
 
Mkuu unajua usumbufu uliopo bandarini? Niliingiza mzigo wangu uwenye thamani ya $10,000 cif, kwenye kuutoa ndio nilipojua kuwa sijui, wakaanza hii kampuni iliyoinspect hatuitambui wakati ipo kwenye list yao ya kampuni zilizothibitishwa, kuna vikodi kibao vya ajabu nikalipishwa chemical inspection kwa kukadilia thamani ya mzigo mzima wakati hiyo so called chemical ni spray zisizofika hata kumi, niliutoa ule mzigo ila baada ya kugombana sana na wale officers na kufishishana na mabosi wao ila mwisho mwisho wakaona huyu mkuda wajarelease mzigo, thamani ya kodi nilizolipa zilijua almost 85% ya gharama ya mzigo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wengi Sana wanaonaga biashara kama ni kama wanavyo waza fanyeni biashara muone hapo bandarini watu wanavyo palalamikia!!
Kuingiza kodi za TRA duh me biashara hapa sifanyi tena nitafanya kitu kingine maana ata ukiwa na mtaji 100M usipo danganya TRA ndani ya miaka 2 unafilisika! sasa Mazingira gani haya kufikia iyo Singapore unayo sema !!
Kodi zingekuwa nafuu hakuna kitu kingenyima nchi zote ambazo hazina bahari ata zenye bahari kufanya biashara na soko la kariako!!
Kuna ma inspection kibao yaliyo zidi standard ata za ulaya ilimradi tu kumkandamiza mfanya biashara!
 
Mkuu unajua usumbufu uliopo bandarini? Niliingiza mzigo wangu uwenye thamani ya $10,000 cif, kwenye kuutoa ndio nilipojua kuwa sijui, wakaanza hii kampuni iliyoinspect hatuitambui wakati ipo kwenye list yao ya kampuni zilizothibitishwa, kuna vikodi kibao vya ajabu nikalipishwa chemical inspection kwa kukadilia thamani ya mzigo mzima wakati hiyo so called chemical ni spray zisizofika hata kumi, niliutoa ule mzigo ila baada ya kugombana sana na wale officers na kufishishana na mabosi wao ila mwisho mwisho wakaona huyu mkuda wajarelease mzigo, thamani ya kodi nilizolipa zilijua almost 85% ya gharama ya mzigo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Duh.. Mm nasubili kupigwa rungu langu mpaka sasa gharama za kodi mzigo wangu zimeshafika 60% na bado naambiwa sijui nilipie manini nini huko.. Hii nchi ngumu sana.
 
Andiko zuri .. tatizo kubwa ni kodi za bandarini na pia Kodi za frem ...from ya laki tano kwa mwezi hata stooo ya nyumbani in kubwa...alafu kuna kitu madalali wanaita kilemba yaani ni wizi mtupu. Ili ufungue biashara inayoeleweka basi jipange sawa sawa .
 
BANDARI YA DAR ES SALAAM NA SOKO LA KARIAKOO NI FURSA YA DHAHABU KWA WATANZANIA.

Leo 12:15pm 17/03/2019.

Imekuwa ni shida sana kwa watanzania wengi kung'amua fursa inayopatikana kupitia uwepo wa Bandari ya Dar es Salaam katika bahari ya Hindi na Soko la Kariakoo ambalo ni kitovu cha uuzaji wa kila aina ya bidhaa kwa jumla na rejareja.Uwepo wa Bandari na Soko la Kariakoo unakupa fursa ya kutumiwa na kupokea mzigo wako moja kwa moja toka nje ya Tanzania kwa njia rahisi ya bahari ya Hindi. Uwepo wa Bandari ni namna rahisi ya kupata mizigo bila ya kutumia gharama nyingi.Hii ni kwa kutumia makontena ya meli kuleta mzigo toka kila kona ya Dunia.

Leo kila nchi ya Kusini mwa Afrika na Afrika Mashariki,utawakuta Wananchi wake katika Hotel za Kariakoo wakingoja kukuche waingie soko la Kariakoo kununua bidhaa na kuzipeleka katika nchi zao,Kariakoo imekuwa kama Dubai, ama China,Ukipita mtaani utasikia lugha mbalimbali katika kikundi cha watu watano hadi sita wakizungumza lugha mbalimbali za Zambia, Malawi, Msumbiji, Zimbabwe, Namibia,Congo, Rwanda,Burundi,Uganda na Kenya licha ya Wachina lukuki katika Maduka ya Mtaa wa Aggrey na Sikukuu, Ukiingia katika benki utakuta raia wa kigeni zaidi ya mia wakihitaji huduma ya kubadili dola ya Marekani na fedha nyingine kama rand na rial kupata fedha ya Tanzania kwa ajili ya kwenda kununua bidhaa katika maduka mbalimbali ya Kariakoo.

-Kariakoo sawa na Dubai ama China.

Kinachofanyika Kariakoo ni sawa na Mtanzania anapokwenda China ama Dubai kununua bidhaa na kuzileta hapa Kariakoo, Sasa Waganda, Wakenya,Wazambia,Wamalawi,Wamsumbiji,Warwanda,Wakongo na Waburundi nao wanafunga Safari kuja hapa Kariakoo kununua bidhaa na kuzipeleka nchini mwao,

Kariakoo imekuwa Dubai ama China kwa ndugu zetu Wazambia,Wakongo,Wamalawi,Warwanda,Waburundi,Wakenya na Waganda, Kununua vitu China na kuuza kwenye soko la Kariakoo hapa nchini,Fursa ya watanzania ipo Kariakoo kwa kuwauzia bidhaa Wakongo, Wamalawi, Wazambia, Warwanda, Waburundi,Wamsumbiji,Waganda na Wakenya.

Sasa badala ya kuuza hapa nchi kwa soko kubwa la Watanzania mikoani pasipo na bahari, basi unaweza kuuza bidhaa kwa Wakongo, Warwanda, wazambia wanaokuja kununua bidhaa katika soko la Kariakoo.Urahisi watakaoupata Wazambia na Wamalawi ni kwamba hawaendi China wala USA/UK ama Dubai kununua.

Watatoka Zambia, Malawi, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kuja Kariakoo kununua bidhaa na kuvipeleka katika nchi zao.Fursa nyingine kwa Watanzania ni Usafirishaji, Ukishanunua vitu vyako Kariako utawasafirishia mpaka Zambia, Kongo, Malawi, Msumbiji ama Rwanda na Burundi Unaweza kuwa na ghala katika nchi hizo na kuzitunza bidhaa hizo kwenye store yako hata watakapopata wasaa wa kufuata bidhaa zao.

Unaweza pia kutumia fursa hiyo kutangaza bidhaa mbalimbali kwa jumla na rejareja katika Nchi hizo ambazo umewapelekea wanunuzi mizigo yao,unaweza kuvi list kwenye matangazo ya biashara katika nchi hizo kuonyesha picha na maelezo yake nakuanza kufanya marketing na pia unaweza kutumia wasaa huo kupata mrejesho wa bidhaa mbalimbali hitaji la watu wa mahali hapo na namna ya kutimiza haja zao,

Ni nafasi nyingine ya kutumia fursa hiyo kuzipandisha chati bidhaa zako (Kurank higher) na kuanza kupata wateja.

-Umuhimu wa Soko la Kariakoo.

Unaweza kuona potential iliyopo kwenye soko la Kariakoo. Na ukifanya marketing vizuri ukajua nchi zaidi ya kumi ambao raia wake wanakuja Kariakoo kununua bidhaa basi unaweza kuuza bidhaa nyingi na kila mwezi ukaagiza mzigo China na kuja kuwauzia Wamalawi,Wazambia,Wamsumbiji,Warwanda,Waburundi,Wakongo,Wakenya na Waganda kwa siku.

Lakini inahitaji kujifunza kutoka kwa watu hasa wazoefu na wenyeji.

-Uzoefu wa Mwenyeji Kariakoo.

Ngoja nikupe machimbo na namna ya mwenyeji anavyopaswa kuwa dira ya mahala husika, kizuri kula na mwenzio...Mfano Vitenge mara nyingi labda machimbo yake yapo Nida kule mnazi mmoja wengi wanaouza Kariakoo wanaenda kufata huko, Viatu navyo vinapatikana labda mtaa wa Narung'ombe na Mtaa wa Kongo,Kitu kingine nenda straight kwenye maduka ya wachina na sio madalali wa kati yaani sio wale machinga wanaomwaga chini,hapana,nenda kwa mchina au Mtanzania mwenye duka la jumla dukani utakuta zile raba simple wanauza 4000/pc wakati Machinga katikati ya mitaa ya Kariakoo atakuuzia 10,000/-na vile visandles wanauza 2500/pc wakati Machinga mitaani atakuuzia 3,000/ hadi 5,000/- Cheni labda nenda Mchikichini katikati kuna mchina anauza mpaka 2000-3000/ kwa dazani na hazipauki.Magauni nayo ingia ndanindani Mtaa wa Kongo na Aggrey wanauza bei chee kuanzua 6000,8000,1000 hadi 16000 kwa pc.

Labda Watu wanadhani bidhaa za China zina quality ndogo lakini siyo kweli, China wanakuuzia quality unayotaka. Kwa USA na Ulaya huwezi ingiza kama hizi zinazokuja kwetu.Lakini ukihofu basi agiza bidhaa za India ambazo wanadai hazichakachuliwi na ni original.

Watanzania wengi watafikiri ni mtaji mkubwa kuagiza bidhaa toka China ama Dubai na kuleta Kariakoo, hata unaweza kujaribu kwa kuleta sample na kuuza katika soko la Kariakoo ili bidhaa yako uijue vizuri.

Bandiko hili linaweza kusomwa na wengi naamini litaamsha usingizi wa Watanzania wengi kujua fursa ya Bandari ya Dar es Salaam na soko la Kariakoo na sio kuwaachia Wakongo,Waburundi,Warwanda,Wazambia,Wamalawi,Wamsumbiji,Wakenya na Waganda.

-Upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam.

Upanuzi wa bandari umekamilika kwa asilimia kubwa, Ujenzi wa magati na kuongeza kina cha sehemu ya kupakia na kupakua mizigo katika bandari ya Dar es Salaam.

Upanuzi wa bandari, ujenzi wa magati na kuongeza kina cha kupakia na kupakua mizigo,kwa sasa utaiwezesha bandari kuhudumia Meli kubwa zaidi kwa kina cha mita 12,Upanuzi huu sasa umeondoa foleni za Meli kushusha mzigo,na sasa bandari ina uwezo wa kushusha mizigo ya kutoka kweye Meli kubwa saba kwa wakati mmoja.

-Tanzania ya Viwanda na Biashara inawezekana.

Kunafursa nyingi sana kutegemeana na wewe mhusika unataka kufanya nini katika biashara,kwa kutumia fursa ya Tanzania ya Viwanda, uwingi wa watu na uhitaji wa vitu katika Tanzania.

fursa ni nyingi nadhani ni wewe na akili yako na mazingira uliyopo,Kwa biashara za kueleweka (za mitaji mikubwa) angalia mahali ulipo,Fahamu hitaji la watu,fungua duka la nguo na vifaa vya watoto wa dogo...labda ni Biashara nzuri sana sema inataka subira,...au kama una ufahamu katika sekta ya Umeme una utaalam fungua duka la vifaa vya Umeme na tafuta hela ya kuagiza mzigo China, kama ni mtaalam wa ujenzi basi fungua duka la jumla la vifaa vya ujenzi.(kariakoo kuna maduka kibao ya vifaa vya jumla kama utashindwa kuagiza China)

Biashara ni matangazo, jifunze namna ya kutangaza bidhaa zako,weka matangazo kwenye tv ama kwenye redio ili kuweza kuliteka soko kama ukijitangaza na ukiwa na maono mazuri basi utafanikiwa sana.

Nimalizie kwa kusema, Soko Kuu la Kariakoo jijini Dar es Salaam na Bandari ya Dar es Salaam ni fursa adimu kwa Watanzania kuna mazingira mazuri kwa wafanyabiashara ni fursa kubwa ya kuitumia Bandari ya Dar es Salaam, kwa maana nchi zote ambazo hazina bahari zinakuja hapa,Malawi,Zambia,Msumbiji,Namibia,Rwanda,Burundi,Kenya,Afrika ya Kati, Guineas na Uganda,mazingira mazuri ya biashara katika Soko la Kariakoo na Bandari ya Dar es Salaam yanatoa fursa kwa wafanyabiashara wadogo na Wakubwa kuweza kuagiza mzigo na kuupata kwa urahisi na bei nafuu,kuweza kuuza kwa jumla na rejareja katika Soko la Kariakoo ambalo ni kitovu cha Biashara kwa nchi za Kusini mwa Afrika,Afrika Mashariki na kati,

Ndugu yangu Mtanzania anza kuangalia biashara kwa mtindo tofauti wakati wa muda wa mapumziko. Tembelea Kariakoo kaa uone raia wa kigeni wanavyomiminika kuja kununua bidhaa, angalia jinsi wanavyonunua na kwenda kuuza vitu na kisha tembelea nchi zao kujua hitaji na soko halisi, pia weka hela Tembelea China ama Dubai uone wanavyozalisha. Kwa wale ambao wameishi Ulaya na Amerika wajua jinsi fursa zilizopo hapa Tanzania lakini watu wamezikalia kwa kukosa exposure ama akili ya kufikiri kuvuka mipaka na kujaribu, yupo mfanyabiashara mmoja kaenda kuwekeza Umeme huko Comoro kama ilivyokuwa Richmond hapa kwetu na hivi sasa ni tajiri mkubwa kabadili na uraia kawa Mwafrika Kusini,Biashara inayofanyika ni kupata wazo la soko jipya kwa maana ya soko ambalo halijafikika na kuendelea kuwekeza katika soko la sasa na lililopo. Naamini utabarikiwa Sana kwa kukuamsha huku kuijua fursa ya dhahabu inayopatikana Tanzania kupitia Bandari ya Dar es Salaam na Soko la Kariakoo, Ahsante Mungu kwa kuibariki Tanzania,Tupe Neema ya kuweza kuzitumia ipasavyo baraka ulizotujaalia.

Nikiishia hapa, Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854.
Msemakweli Chakubanga, asante sana, haya ndiyo matumizi sahihi ya jamii forum, na dio maana katiaka utawala huu ninachokiona kama mwelekeo sahihi ni ujenzi wa reli ya kisasa- SGR inayotumia umeme. Kuna walkati naiona nusu ya soko la kariakoo ujiji- Kigoma. Mimi ni mtu wa Kagera, lakini kila ninaposikia wahaya wanatamba kwa usomi huwa naona haya/soni. Sielewe kwanini moja ya wilaya zake haziwi nusu branch ya kariakoo. Watu wa Burundi Rwanda, Uganda na hata Sudani ya Kusini wanafuata bidhaa karikoo na kusafiri umbali mrefu. Usomi gani huo usiowezesha watu wakanufaika kiuchumi?
 
Mtoa Mada Kaeleza wazo lake vizuri. Ingawa Kuna changamoto za kodi bandarini etc..mbona still watu wanafanya biashara kariakoo...hakuna biashara rahisi utateleza tu. Kila kitu kinahitaji jitihada za nyongeza. Unaweza Nunua kariakoo ukauza nje it's possible

Habari za asubuhi mkuu
Nashukuru sana kwa huu uzi wako. Biashara/fursa ambayo kila kitu kipo okay hiyo sio biashara/fursa tena. Tusiwe watu wa kutaka mazingira yote ya kibiashara yakae sawa ndipo tuweze kuingia kwenye biashara. Tuondokane na ile dhana ya kulalamikia kila kitu wakati hatujaaanza hata kuchukua hatua. Mfanyabiashara/mjasiriamali hodari anatengeneza njia hata mazingira yawe magumu vipi. Binafsi mimi nimeona fursa.

Naomba kuuliza njia rahisi za kusafirisha mizigo midogo midogo kwenye nchi za jirani kama congo, burundi, malawi, zambia nk na pia ni utaratibu gani unaotakiwa kufuatwa.
Asante sana.
 
15 May 2023​

WAFANYABIASHARA KARIAKOO BILA UWOGA WAFUNGUKA MAZITO, "TUMEWACHOKA, HAWAELEWEKI".

Hakika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam linatakiwa kulindwa kwa wivu mkubwa ili liendelee na kuwa Dubai ya kanda ya Afrika ya Mashariki, Kusini mwa Afrika na kanda ya Maziwa Makuu. Ili hilo litimie serikali iwasikilize wafanyabiashara wa Kariakoo kwa umakini sana ili adhima hiyo itimie kuwa Kariakoo iwe kimbilio la wafanyabiashara wa Zambia, Zimbabwe, Malawi, DR Congo, Cameroon, Burundi, Rwanda, Comoros na Madagascar
 
MGUSO WA BIASHARA TOKA KARIAKOO HADI CAMEROON

Raia toka Cameroon anazungumzia bidhaa nyingi kama viatu vya ngozi, Vitenge n.k toka Kariakoo Tanzania vinapelekwa kwa wingi Cameroon

Cameroonian Touring Dar Es Salam | largest market in Tanzania 🇹🇿 | Kariakoo Market

Wafanyabiashara wa mizigo inayovuka mipaka Dar es Salaam kwenda Burundi waelezea kero za TRA kwa waziri mkuu

Wafanyabiashara wa Kitanzania wenye hela wameamua kununua vitu nchini Uganda na kuvipeleka Burundi n.k

Watanzania hao wanaikwepa Kariakoo na Dar es Salaam kutokana na kero pia ufumbufu kwani nchini Uganda mambo hayo hakuna.

Mfanyabiashara wa Kigoma anasikitika Kariakoo, Dar es Salaam na bandari biashara kusinyaa pia zingine kufa kutokana na usumbufu wa TRA na vyombo vingine vya serikali.

Hivyo kuinyima Dar es Salaam ambayo kijiografia na bandari kuwa kitovu cha biashara Afrika Mashariki na Kati.

Mbali ya kuinyima serikali kuwa na wigo mpana zaidi wa kukusanya kodi kwa wafanyabiashara wengi zaidi kama mazingira yangekuwa rafiki ya kufanya biashara za ndani na zile za kuvuka mipaka .

Hayo yamebainika katika mkutano baina ya waziri mkuu na wafanyabishara leo ktk viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam ,Tanzania.
 
Back
Top Bottom