Bandari ya Dar es Salaam, lango kuu la biashara Afrika

msuyaeric

JF-Expert Member
Dec 18, 2014
838
1,167
Kwa mujibu wa Central Corridor Transport Observatory Report (CCTOR), Wasafirishaji wa mizigo wanaotumia bandari ya Dar es salaam wanatumia fedha kidogo zaidi kuliko bandari nyingine yoyote. Mfano, Msafirishaji anayetumia Bandari ya Dar es Salaam ataepuka gharama ya dola za kimarekani 1.18 kwa kila kilometa kwa kontena la mizigo ambalo angesafirisha kupitia bandari nyingine kama vile Bandari ya mombasa.

Ubora wa miundombinu Nchini Tanzania ni kichocheo kikubwa cha urahisi na gharama nafuu ya usafirishaji wa mizigo kutumia bandari ya Dar es salaam, Serikali ya Tanzania imewekeza zaidi ya dola milioni 60 kwaajili ya kuboresha bandari hii ambayo kwa sasa ndio lango kuu la biashara kwa Tanzania na nchi jirani.

Wastani wa gharama ya kusafirisha mzigo kwa kilomita moja kwa kotena moja kutoka bandari ya Dar es Salaam kwenda Kigali nchini Rwanda ni Dola za Kimarekaani 1.9 wakati mzigo huo utatumia Dola za Kimarekani 2.1 kwa kutumia bandari ya Mombasa.

View attachment 1647160
 
Sasa kichwa cha habari na maelezo mbona haviendani?

Unajua maana ya bandari kuwa lango kuu miongoni mwa bandari zote Afrika?
 
Back
Top Bottom