Countrywide
JF-Expert Member
- Mar 2, 2015
- 18,174
- 27,223
SERIKALI YAMKANA HAYATI MAGUFULI
Waziri Mwambe amesema haya ''Kuna jambo niliweke sawa ilisemwa kuwa wachina walisema kusiendelezwe bandari yoyote kutoka Mtwara hadi Tanga,sio kweli. Hayo maneno sijui yalitoka wapi, kilichosemwa ni kwamba kuanzia Dar es Salaam hadi Pangani kusiendelezwe bandari''
Nimeona na kusikia maneno ya waziri Mwambe kuhusu ujenzi wa bandari ya bagamoyo na kilichosemwa sio Mtwara hadi Tanga bali ni Dar hadi Pangani.
Kwanza namkumbusha waziri Mwambe kuwa Pangani pia ipo Tanga.
Pia hata kama ni Dar hadi Tanga, pia sio masharti mazuri. Kwanini ndani ya nchi yako upangiwe uendeleze wapi na wapi usiendeleze?
Sababu waliyotoa ni kupata ushindani endapo bandari zitaendelezwa ukanda huo, Ila mbona wao wanakuja kuleta ushindani kwa bandari ya Dar?
Hilo lilikua moja ya sharti, vipi kuhusu mengine mbona waziri umekua kimya?
Na-support ujenzi wa bandari ila tutangulize maslahi ya taifa kwanza na naomba hata hayo masharti ya kutoendeleza Dar hadi Tanga msiyakubali.
Kazi iendelee