Bandari ya Bagamoyo hiyooo inakuja, ama tuikatae sasa au tuipokee milele!

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,109
35,092
Bila kumumunya maneno, serikali ya awamu ya sita imedhamiria kwa 100% kuhakikisha mkataba ya ujenzi wa bandari ya Bagamoyo unatekelezwa mara moja, serikali imejipanga kuhakikisha hilo linafanikiwa kwa haraka iwezekano.

Bila kusimamia upande wowote katika hili kwenye mada hii, ninapenda watanzania wote tufahamu haya kwa uchache.

1. Mpaka sasa hakuna aliyeweza kutuletea huo mkataba/mapatano hadharani tukauona au kuusoma sisi wenyewe. Kwa kipindi chote tumekuwa tunasikilizishwa maneno ya watawala tu (Kikwete alisema ni mkataba bora kabisa, Magufuli akasema ni wizi mtupu, Samia akasema ni mkataba poa). Kifupi tunauziwa mbuzi kwenye gunia.

2. Wakati pekee wa kuuhoji, kuupinga au kuurekebisha huo mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ni sasa, kinyume na hapo ni kuupokea milele!

3. Kupitia mkataba huu wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo huenda tukaja kushuhudia mvurugano na mnyukano mkubwa ndani ya serikali baina ya watawala wenyewe na ndani ya CCM ikiwa hawataafikiana vyema sasa. Fukuto linaloendelea sasa ndani kwa ndani ni kubwa sana, huenda kuna kuzungukana kukubwa!
 
Bila kumumunya maneno, serikali ya awamu ya sita imedhamiria kwa 100% kuhakikisha mkataba ya ujenzi wa bandari ya Bagamoyo unatekelezwa mara moja, serikali imejipanga kuhakikisha hilo linafanikiwa kwa haraka iwezekano...
Mkataba gani uliwahi kuletewa hadi udai wa Bagamoyo?
 
Bila kumumunya maneno, serikali ya awamu ya sita imedhamiria kwa 100% kuhakikisha mkataba ya ujenzi wa bandari ya Bagamoyo unatekelezwa mara moja, serikali imejipanga kuhakikisha hilo linafanikiwa kwa haraka iwezekano...
Kwa mujibu wa yule mzee aliyewekewaga sumu amesema kuwa walikubaliana Bagamoyo kujenga Gati na sio bandari.kwa maana iyo chama hakitatambua ujenzi wa bandari ya bagamoyo.

Wasiwasi ni kwamba kama tutakurupuka basi mwaka 2050,Bagamoyo itaweza kuwa sehemu ya ardhi ya wachina
 
Back
Top Bottom