Bandari ya Bagamoyo aka Mbeganizhou ya Wachina

Wanasiasa na wabunge wanaoshadadia hiyo bandari kama wana nia njema na wanajua wanachokifanya nilidhani hatua ya kwanza ingekua ni kuishinikiza serikali iuweke wazi huo mkataba ili terms na conditions zake zote zijulikane then waone kwa nini JPM aliukataa.

Binafsi naona ni jambo la kheri alivyoukataa maana kama mkataba ni wa hovyo still tuko salama na tuna fursa ya kuamua kwa uhuru tuachane nao au tuendelee nao kwa terms mpya, lakini vipi kama angeukubali halafu kumbe mkataba ni wa kinyonyaji na ndio tungekua tumeshauingia na kutoka si rahisi au gharama ni kubwa?

Pamoja na mapungufu lakn tulikuwa tumefika pazuri na tunaelekea pazuri na modality ya Tanzania kwanza, Tanzania kwanza, una ulazima gani wa kukimbilia vipya tena vyenye masharti magumu ilhali una vya kwako ambavyo unaweza ukavirekebisha, ukaviboresha, ukavisimamia vizuri na vikakupa matokeo mazuri. Ktk issue kama hizi hisia na mahaba ya kivyama na kiitikadi tukifanikiwa kuweka pembeni tutafanikiwa sana.
 
Then kwa miaka 70 hiyo watakuwa wanalipa kodi? Na kama ni hivyo kodi kiasi gani?

Unaweza ukaja kwangu una mradi wako, nikakupa aedhi uweke mradi wako. Terms zangu ni kuwa you will have to abide by tax regulations of my specification.

Ingiza gharama zako, mimi bila kujali unapata nini, utanilipa kodi kwa chochote utakachokifanya s per tax administration laws za kwangu.
Watu wasiojulikana VIP bado wapo wakajibu ili bango maana hata JF yawezekana wapo sio kutoa maneno huko Mie nashukuru inanipotezea muda Tu hakuna jipya

IMG-20210409-WA0013.jpg
 
Tumeukataa huu mradi kiroho na kimwili pia ni Hadi mashariti ya kijinga yatakapoondolewa!!

Tutawafurusha hao waliozoea kuweka rehani Mali zetu Kwa kujali matumbo yao
Huo mradi unajengwa na nyinyi majizi kama hamtaki maamzi ya uongozi tulio nao basi hameni nchi mrudi kwenu burundi
 
Ujenzi wa bandari ya bagamoyo umejaa uhuni wa kutisha.

Kulingana na mkataba, wachina walitaka kuingia makubaliano ya kujenga miundombinu yote ya bandari kwa gharama zao.

Serikali ya Tanzania haikutakiwa kuchangia senti yoyote kwenye ujenzi.

Wachina walitaka kujenga bandari yote kwa gharama zao.

Baada ya bandari kukamilika ujenzi wa miundombinu yake, mkataba unasema kwamba, wachina wanapaswa kuchukua mapato yote ya bandari kwa MIAKA HAMSINI.

Kwahiyo, baada ya miaka hamsini ndio watakapowaachia bandari yenu.

Baada ya wachina kukomba na kufaidi mapato yote, ninyi mtakabidhiwa bandari yenu mwaka 2070.

Huu Mradi Ni Nonsense Otherwise Kama Kuna Revision Ya Terms
 
Waulizeni wazambia na kenya Mombasa karibu iondoke !! kuona picha za video! kuwa nzuri tena kwa hela zaoa!!! sio sababu ya kukubali bali kilicho nyuma ya pazia hapo ndio weledi unatakiwa sio mvuto wa bandari mweee nanai karoga watu vichwani?
 
(wachina wanapaswa kuchukua mapato yote ya bandari kwa MIAKA HAMSINI.)
Sio 50 Ndugu 99.
2070 + 49 = 3019
Hapo tunaopiga soga hapa wote hatupo.

itakua generation ingine nayo inaweza kupigwa porojo ikapenyezewa chajuu wakasign tena mkataba Mpya miaka 50+.
 
Ilitakiwa ijengwe na wachina na waoman .
Kama ulikuwa haujui.
Na lengo NI kuujenga mji wa bagamoyo.sio bandari Tu..
Kuhusu mkataba na makubaliano hakuna raia wa kawaida aliyeuona huo mkataba..
Cha msingi mkataba uangaliwe upya.
Bandari ya bagamoyo ina umuhimu wake.
haiwezekani miaka yote tukawa na bandari moja kubwa..
Kama suala NI mkataba watazungumza.ila bandari ya bagamoyo lazma ijengwe.
 
Mataga kazi mnayo ila mnasahau kuwa tayari mama Samia ndiye rais wa JMT na hakuna mjadala.
Hili ndio tatizo lilipo, mahaba ya vyama na itikadi za kisiasa, chuki au mahaba juu ya mtu fulani.

Huu mradi nahisi kuna watu wanaweza kuukubali au kuukataa kwa sababu tu JPM aliupinga. JPM is no more na hatarudi tena kuishi kwenye hili taifa so kama kuna hasara au faida itapatikana na ya sisi tuliopo sasa na watakaokuja baadae so maamuzi yetu yawe juu ya facts sio hisia na mihemko ya sijui Mataga na Machaga.

Kwa mfano:
JPM alisema wachina wanataka wakabidhiwe kila kitu for 90 years na wasiulizwe chochote.

Pia walitaka bandari zilizopo sasa zisiendelezwe eventualy biashara ya bandari dsm, tanga na mtwara ingekuaje? Yaani unawekeza sehemu moja huku unaua sehemu nyingine.

Ktk huo mkataba misamaha ya kodi waliyotaka ni ipi na kwa muda gani.

Na yatakuweko mengine mengi, sasa haya inabidi tujue yanaishaje ishaje uwazi uwepo juu ya huo mkataba na mikataba mingine ili tuwe na nafasi ya kuwahukumu wanasiasa vizuri pale wanapotaka kutuingiza shimoni.
 
Aisee nyie Watanzania kwa kushirikiana na JWTZ chukueni nchi yenu. Hawa viongozi wa ccm na upinzani wachomwe moto na gesi ya mtwara live ikiinyoshwa tbc taifa. Nchi zote zilizoendelea viongozi wale wanaonafanana na hawa wa kwetu walipigwa risasi, kunyongwa hadharani. Ilisaidia sana kwa kuwaambia wasifanye makosa ya kuumiza vizazi vya nchi.
Mkuu wew mkataba umeuona?
 
Sina imani kabisa na serikali ya awamu ya sita

Tatizo ndani ya serikali unafiki ni mwingi sana, leo hii wanao msifia samia ni wengi sana kwakuwa inaonekana serikali yake ni dhaifutu...
Kichwa chako kimejaa matope badala ya ubongo we mganga njaa. Roho mbaya za kichawi zinakusumbueni!

Koma kabisa kutukana raisi wetu mama Samia ukiwa nyuma ya keyboard.
 
Hivi kwa akili ya kawaida tu kweli mkataba wa aina hiyo tunaoambiwa ni kiongozi gani angethubutu kuukubali hata kama yeye mwenyewe binafsi angekuwa na maslahi? Viongozi waache kupakaziana ujinga ili wapate sifa toka kwa wananchi yeye aseme tu aliamua kuupiga chini kwa vile aliona hapati kitu ,maana tuseme ukweli tu viongozi wote wa Afrika ni wezi tu hakuna cha mzalendo wala nini.Mwendazake alikuwa mtu wa hovyo sana.
Kabisa mkuu, hata mtoto mdogo hawezi kukubali mkataba wa aina hiyo, hizo ni propaganda za Jiwe.
 
Magu sijawahi muamini hata siku, tungeuona mkataba tujiridhishe, afterall majadiliano yalikuwa hayajafika mwisho ila mzee baba alipanic kwa mihemko

Nimeliokota hili andiko sehemu limetupwa;

Mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ulisitishwa kufuatia majadiliano yenye tija yaliyofanywa mwaka 2018. Serikali ilibaini masharti magumu yanayoweka rehani uchumi wa nchi na kuhatarisha uhuru wa nchi yetu. Kwa mantiki hii wajuvi wa mambo katika mimbali za "Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi" watang'amua na kuunga mkono zuio hilo la serikali.

Kupitia majadiliano hayo yaliyojikita katika viunga vya ujasusi wa kidola na kiuchumi, serikali ilibaini baadhi ya masharti yafuatayo ambao ni hatarishi kwa uchumi wetu;

1) Wachina walihitaji kuendesha Bandari hiyo baada ya ujenzi bila kuingiliwa, jukumu la kupanga bei liwe mikononi mwao.

2) Pia ukanda huo wa Bandari ya Bagamoyo (Tanga-Mtwara), kusiwe na uboreshwaji wa Bandari zingine, mathalani Bandari za Tanga, Dar es Salaam, Mafia na Mtwara zibaki kama zilivyo kitu kinachohatarisha ukuaji wake na kwa namna yoyote ile zingekufa kifo cha asili.

3) Eneo lote la ujenzi wa viwanda na mji wa kisasa wachina walihitaji umiliki wa hati kwa zaidi ya miaka 33 (zaidi ya miongo mitatu). Mbaya zaidi walihitaji kama Faida yao itakuwa haijapatikana kwa miaka 33 basi hata kwa miaka 99 wangeweza kuendelea kumiliki na kukusanya kodi.

4) Wachina walihitaji pia wawe wasajili, wasimamizi wa viwanda vyote vitakavyowekezwa eneo hilo sanjari na ukusanyaji wa kodi zote zitakazolipwa eneo huska.

Sintofahamu inaongezeka pale ambapo, ni wachina hao hao ambao wangetumika kutoa tafsiri ya kimahesabu kuhusu faida au hasara kutokana na 100% ya kumiliki au kuratibu mchakato mzima wa mapato katika eneo hilo. Hapa nalazimika kukumbuka usemi wa kiratini, "Quis Custodient, Ipsos Custodes?" Kwa tafsiri isiyo rasmi ni, "Who watches the watchers?" Au "Nani atawalinda walinzi wetu," ilihali wenye mali tumewekwa kando na wageni wamepewa fursa ya kufanya wanavyotaka.

Katika viunga vya ujasusi wa kidola na kiuchumi kwa namna yoyote ile lazima wachina wangetuchakachua ili watuvune vya kutosha. Maana wao ndio wangekuwa walinzi wa 100% wa mapato yanayoingia na hata kampuni za ukaguzi ili ionekane wamepata hasara ili kupata tiketi ya kuongezewa muda wa kumiliki na kukusanya mapato.

Aina hii ya makubaliano kandamizi ndio imepelekea Bandari ya Hambantota, Sri Lanka kuchukuliwa na kumilikiwa na China kwa 99%. Pia Uwanja wa Ndege wa Mattala Rajapaksa, Sri Lanka kumilikiwa na China kwa 70%. Ikiwa ni zao la kushindwa kulipa mikopo iliyotegwa katika mtego wa falsafa za "Quis Custodient, Ipsos Custodes."

Rejea andiko lililoandikwa na Institute for Security Studies Africa mwaka 2017 lenye kichwa cha habari, "Lessons from Sri Lanka on China's 'debt-trap diplomacy."

Aidha, rejea andiko ambalo liliandikwa na The Diplomat mwaka 2017 lenye kichwa cha habari, "Sri Lanka's Debt and China's Money," sanjari na andiko la mwaka 2018 lenye kichwa cha habari, "Does Debt Pay? China and the Politics of Investment in Sri Lanka."

Nawiwa kuwaomba watanzania wenzangu kuyatafta maarifa ambayo yamefichwa katika Vitabu au maandishi ili kubaini propaganda zinazofanywa na baadhi ya watu kutetea mradi wa Bagamoyo uendelee kwa maslahi binafsi paspo kuutizama ukweli kwa maslahi mapana ya taifa.

Aidha, niipongeze serikali ya awamu ya 5 kwa kuonyesha ukomavu wa hali ya juu katika viunga vya ujasusi wa kidola na kiuchumi. Hii ni zaidi ya tafakuri tunduizi ya kukataa makubaliano yanayotweza utu wa Taifa letu, kupoka Uhuru wa nchi na kuweka rehani uchumi wa nchi yetu kwa faida ya China.
 
Montenegro wana deni la 1$bl ambalo waliingia na wa China na wameshindwa kulilipa. Wanalazimika kulipa ardhi yao yenye thamani hiyo!
Haya mauongo manajifunziaga wapi?

Nchi ina bandari ya kisasa kama ya Bagamoyo ishindwe kulipa dola bilioni 1?

Hata hivyo kwetu sio mkopo, ni concession. Muwage mnaeleweshwa mnaelewa!
 
Swala la mradi wa bagamoyo mtu alieona mkataba huo ni Rais Magufuli tu, na huyu mtu alikua na sifa mbili kuu "MUONGO, MSIRI NA FISADI".

Hii DNA ameiacha mpaka kwa baadhi ya wateule wake waliobakia madarakani. Mmoja wao ni Waziri Mkuu (Ambaye tunatakiwa kumwanzishia amsha amsha mitandaoni AJIUZULU)...
 
Back
Top Bottom