Bandari Wagoma

Kwayus

Member
Feb 18, 2008
44
1
Jana kwa Mara Nyingine Bandari ya Dar es Salaam Upande wa Utoaji wa Mizigo Bandarini {Delivary}{ MOTOR VEHICLE SECTION}Wamegoma Kuendelea na Mgomo ambao Ulianza Jumanne Saa Kumi na jana Kuanzia Saa Nane Mchana kwa Kile Walichokidai Kuwa Hawalipwi Over time

Kitendo Cha Bandari Kugoma Kilisababisha Wakala{Clearing and Forwarding}kuandamana hadi Ofisi Za Port Manager

Kwa Wakati Huo Hawakuweza Kuonana na Port Manager ndipo Mmoja wapo Wa msaidizi wa Port Manager Kupiga Simu Kitengo Cha Magari {Motor Vehicle} na Kuruhusu Mawakala Kuendelea na Kazi

Hata hivyo Cha Kushangaza ni kwamba Hakuna Tangazo ambalo Linaonyesha Mda wa Utoaji wa Magari au Kuandika Vibali vya kutoa Magari Bandarini ambapo Imekuwa Ni taarifa tu inatolewa kuwa Mda Umeisha

Kwa Upande Mwingine Kuna Malalamiko Ambayo Yanaweza yakawa ya msingi Baina ya Makarani wa Bandari Kwa Uongozi Kuwa Wamekuwa Wakifanya Kazi Bila ya Kulipwa Over time ambapo Inaonekana Wazi Wale Wanaoingia Asubihi Wanafanya kazi hadi Jioni Wakiambiwa Kuwa Endelea na Kazi.
Shift Inayoingia Mchana Ni Ndogo Kulinganisha Na kazi watakazo Fanya
Pia inaonekana wazi Maofisa ambao Wanaingia Asubuhi Hadi Jioni wao hawana Shifti jambo ambalo wao wanadai Overtime.

Kwa Tatizo Kama hili Kumesababisha Kuwepo na Vurugu wakati Wa Kutoa Magari Hasa Pale Meli Inapofika.Maagent{Clearing and Forwarding}wanakuwa Tayari wamekamilisha Taratibu Zote za Kutoa Magari
Hatari Zaidi Hii bandari Inatumiwa Na Majirani Zetu Kutoka Congo,Zambia,Uganda,Malawi,Rwanda Nk hii Picha wanayoiona Sii nzuri.

Cha Kushangaza inachukua Siku Hadi tano{5}Bandari Kukupa gari Kwa Kile Kinachodaiwa Gari Iko SHED Haina Possition.

Upande Wa Security Wao Hawana Matatizo wamejpanga kwa Kufanya Kazi.
Upande Wa Kukusanya hela{Handlling,Warfarge,Storage,VAT}Zao Hadi saa Kumi Na Mbili wanapokea Hela
Kwa Sura Hii Litazamwe kwa Upya Tunataka Ufanisi Na Sii mazoea
 
Back
Top Bottom