Kumezuka wimbi la kujenga bandari kavu huku mbezi beach. Sasa hivi ziko mbili zinajengwa! Cha kushangaza wamiliki hawa hawana vibali kutoka manispaa lakini wanajenga usiku na mchana! Ujenzi wenyewe ni imara kabisa hii ikimaanisha kuna wataalamu wa fani zote wanaosimamia hizo kazi. Kwa hiyo inamaanisha wataalamu hao wanavunja sheria kwani hakuna bango linaloonyesha kinachojengwa.
Viwanja hivi ni kwa ajili ya makazi na hakuna kibali cha wizara ya ardhi kilichotplewa kubadilisha matumizi ya ardhi. Athari za bandari kavu kwenye makzi ya watu ni kama uharibifu wa barabara na mabomba ya maji. Malori yenye kontena kukata nyaya za umeme na vibaka. Vilevile magari mazito husababisha nyufa kwenye nyumba na hasa hasa kuta za uzio (fence).
Je mamlaka husika ziko likizo au ndio rushwa mbele kwa mbele?