Banda la maonyesho la Barrick lazidiwa na banda la wachimbaji wadogo wadogo wadogo

Slave

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2010
Messages
5,320
Points
2,000

Slave

JF-Expert Member
Joined Dec 6, 2010
5,320 2,000
Nipo kahama katika banda la maonyesho la kampuni ya uchimbaji madini barrick gold mine. Nimeona banda jinsi lilivyopendeza picha nyingi za mitambo inayotumiwa kuchimbia dhahabu,wahudumu wengi wakarimu,pamoja na vipeperushi vingi kwa ajiri ya wageni wanaotembelea banda hilo. Pamoja na hayo yote kwangu banda hili limekosa u maana kwakuwa mitambo ninayoiona hapa inanidhibitishia kwamba huwa inachimba DHAHABU pia wazungu ninao waona inanionyesha hawa wazungu walikuja kuchimba Dhahabu. Mimi binafsi nilitegemea Pengine wangeleta japo tofali moja la dhahabu ili tuone kile ambacho wa tz,wabunge na wananchi kinacho wafanya wapigie kelele. Mitaani hata bungeni. Banda la wachimbaji wadogo wadogo kwangu limekuwa na maana sana kwakuwa wao wamejitahiti anagalao kuweka dhahabu feki. Ndugu zangu wana jf pengine uelewa wangu mdogo ndio unanifanya nishangae haya hivyo naombeni mnieleweshe kwa hili.
 

Forum statistics

Threads 1,379,520
Members 525,449
Posts 33,748,059
Top