Banana Republic Ya Sitta Na Mwakyembe: Tafsiri Yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Banana Republic Ya Sitta Na Mwakyembe: Tafsiri Yangu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Jan 21, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Jan 21, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  [FONT=&quot]
  [/FONT]


  [FONT=&quot]Ndugu Zangu,[/FONT]

  [FONT=&quot]SIASA ni burudani pia. [/FONT][FONT=&quot]Siku hizi hakuna ukame wa burudani za kisiasa. Kila kukicha, tunaamka na burudani za kisiasa. Jumatano iliyopita nililikamata Tanzania Daima, nikamsoma ndugu yangu Absalom Kibanda. Akaandika; " Sitta ana bahati, Waziri Mkuu siyo Msuya leo!"[/FONT]

  [FONT=&quot]Kichwa cha makala tu kilitosha kuona kivumbi kitakachofuatia, nina uzoefu, hata kama si wa miaka mingi sana. Mwalimu wetu wa siasa pale Tambaza Sekondari alipata kutufundisha mambo yanayoweza kusababisha kivumbi kutokea katika siasa. Alisimulia kisa cha Sungura aliyeshtuka kumsikia tembo, kiongozi wao wa wanyama, akiwatangazia shughuli ya ngoma ya wanyama wote itakayokesha. [/FONT]

  [FONT=&quot] Tembo aliwahakikishia wanyama wenzake, kuwa amani ingekuwepo. Sungura mjanja aling'amua hila za akina simba kumshawishi tembo kuitisha ngoma ile . Haiyumkini, simba akakesha ngomani bila kumtafuna swala au pundamilia. Na pengine simba hajawahi kuonja nyama ya sungura![/FONT]

  [FONT=&quot]Sungura alikataa kwenda ngomani akitamka; " Patatoka kivumbi huko!" Na kivumbi kilitimka kweli![/FONT]

  [FONT=&quot]Jumatano hii, kama nilivyotarajia, Ndugu yangu Absalom Kibanda ameshuka na ukurasa mzima kwa makala ambayo, kimsingi ni kuturudia wasomaji wake na kutuomba radhi. Kumuomba radhi pia Samwel Sitta. Kibanda ameonyesha uungwana. Sote tu binadamu, hakuna aliyekamilika.[/FONT]

  [FONT=&quot]Lakini, Jumatano hii pia kwenye ukurasa wa kwanza wa Tanzania Daima kuna habari iliyosomeka; " Sitta, Mwakyembe wazibwa midomo". Na sentesi ya kwanza ikawa ya kishindo kweli; " RAIS Jakaya Kikwete amemfunga mdomo Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta aliyeingia katika mzozo na waziri mwenzake wa Nishati na Madini, William Ngeleja"[/FONT]

  [FONT=&quot]Nilipoiona hiyo nikakiona ' Kivumbi' kingine kitakachotimka. Na kimetimka bila kuchelewa. Jana Mwakyembe na Sitta 'Wamejibu mapigo!' Kama wasemavyo mitaani siku hizi. Ni burudani ya kisiasa ya kukata na jembe na kisha unashindilia kwa nyundo! [/FONT]

  [FONT=&quot]Samwel Sitta anajibu mapigo kwa kutamka haya;[/FONT] "Naomba wananchi wafahamu kuwa siwezi kufungwa mdomo kupinga malipo kwa kampuni ya kitapeli ya Dowans." Anasema Samwel Sitta .

  [FONT=&quot] Kisha anaongeza; "Haraka ya kuilipa Dowans ni ya nini? Nchi hii ina madeni ya muda mrefu kama yale ya Benki ya Dunia na IMF lakini hakuna uharaka wa kulipa kama huu, sasa kasi hii inatoka wapi?" Anahoji Sitta.

  [/FONT]
  "Sijawahi kuitwa popote wala na mtu yeyote na kuambiwa nisizungumze suala hilo, nitaendelea kupinga malipo ya Dowans. Hivyo wananchi wasifikiri nimebadili msimamo.

  "Taarifa zinazosambaa ni za kupikwa tu, zisije zikawapotosha wananchi wakadhani nimewasaliti katika hili, narudia tena sijafungwa mdomo," alisisitiza Bw.
  Sitta .

  Uwajibikaji wa pamoja?

  "Halafu kuna watu wanazungumzia nimekiuka dhana ya uwajibikaji wa pamoja, uwajibikaji wa pamoja ni lazima uamuzi ushirikishe wengine si mmoja kuamua halafu ifahamike ni uwajibikaji wa pamoja," anajibu Samweli Sitta.

  Na hapa naweza kumwelewa ndugu yangu Absalom Kibanda. Najua, kuna , kwa makusudi au kwa ushabiki, wanaoufumbia macho ukweli wa Kibanda. Ndio, kwa mtazamo wangu, baada ya kuyatamka hayo, Samwel Sitta alipaswa kuandika barua ya kuomba kujiuzuru kutoka kwenye baraza la mawaziri. Si atabaki kuwa mbunge? Aende huko bungeni na hata nje ya bunge akayeseme mengine kwa uhuru zaidi.  Anachokifanya sasa Sitta ni kumwekea vizingiti bosi wake, mkuu wa nchi. Maana, kama Sitta hakushirikishwa, Rais si ameshirikishwa? Badala ya kwenda kwenye media kutoa manung'uniko yake kwanini Sitta akwenda kwa bosi wake kwanza, au hakwendeki?

  [FONT=&quot]Na kuna habari ziliwafikia wanahabari wakati wanakwenda mitamboni . [/FONT][FONT=&quot]Zinasema ; Sitta na Mwakyembe kwa pamoja wamewasilisha nia ya kulishtaki gazeti moja la kila siku ambalo liliripoti taarifa za kunyamazishwa kwa viongozi hao, wakidai kuwa ni za uongo.

  [/FONT]
  [FONT=&quot]"Tunakuandikia barua hii upime mwenyewe utuombe radhi kwa uongo huo uliotutungia ukurasa wa mbele wa gazeti lako au usubiri tukuburuze mahakamani kukukumbusha kuwa Tanzania si "Banana Republic" bali ni nchi yenye kuheshimu utawala wa sheria." Wanasema Sitta na Mwakyembe na kuacha kivumbi kikizidi kutimka.
  [/FONT]


  [FONT=&quot]Nijuavyo, tafsiri ya ' Banana Repulic' kisiasa inatokana na nchi za Marekani ya Kati na Kusini ambapo uchumi wake ulikuwa ukitegemea sana zao la ndizi. Na Serikali za nchi hizo zilikuwa zikifanya biashara na uchumi. Ni Serikali za kupandikizwa, za vibaraka. [/FONT]

  [FONT=&quot]Katika ' Banana Republic ' sheria na taratibu hazifuatwi. [/FONT][FONT=&quot]Lakini, kuna swali; Ni 'Banana Republic' gani wanayomaanisha Sitta na Mwakyembe? Na kama yetu si ' Jamhuri ya Migombani', basi yaweza kabisa, kuwa Bongo ni ' Jamhuri ya Mihogoni'- Ndio, ' Cassava Republic!'. Ya Kibanda na akina Mwakyembe na Sitta yataisha tu, kwa kumalizana kiungwana. Naam. Ndani ya ' Cassava Republic', kuna nguruwe pia, wala mihogo![/FONT]

  [FONT=&quot]Maggid[/FONT]
  [FONT=&quot]Dar es Salaam[/FONT]
  [FONT=&quot]Januari 21, 2010[/FONT]
  mjengwa
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ukishangaa ya 6 na Mwakyembe basi kawahi hospitali haraka maana baraza litakavyomomonyoka kama nyumba ya karata, usipime!!!
   
 3. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #3
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,738
  Likes Received: 1,451
  Trophy Points: 280
  Sitta, Mwakyembe na yeyote mwenye kuitakia mema lazima afanye uamuzi rahisi wa kutoka CCM.

  Ki ukweli, majibizano ya mawaziri sio utamaduni wa kawaida. Na udhaifu wa Kikwete... hata mimi pamoja na kumfahamu kuwa ni celebrty, mbabaishaji, mhuni nk lakini he's too low than the lowest.
   
 4. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #4
  Jan 21, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  uwajibikaji wa pamoja ni lazima uamuzi ushirikishe wengine si mmoja kuamua halafu ifahamike ni uwajibikaji wa pamoja,
   
 5. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #5
  Jan 21, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  .....Ndani ya ' Cassava Republic', kuna nguruwe pia, wala mihogo! End of Quoting!

  Msg delivered!
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Jan 21, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kaka makala yako nimeikubali.

  Mi nadhani Tz is more or less a quasi-anarchy society at best. Mwenye nguvu maamuzi yake ndio sheria, na vitendo vyake ndio taratibu. Kungekuwa na sheria na nia ya kufuata sheria, hata huo uwajibikaji wa pamoja ungeeleweka mipaka yake, na hata threashold za kuidhinisha mabilioni kama hayo ya DOwans yangejulikana mamlaka gani ni ya mwisho kulisimamia hilo suala, na mamlaka gani ya ku-corss-check maamuzi kama hayo.

  Kwa maoni yangu hii ni jamhuri ya nyasi, ambapo kunguru huumla panzi vovote, wakati wowote na popote ajisikiapo..bila kuulizwa.
   
 7. N

  Nanu JF-Expert Member

  #7
  Jan 21, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  hii ndiyo TZ filme kila kukicha!!!!
   
Loading...